Naapa kuwa sirudii tena kumsaidia Mtanzania -- never!

Huyo atakuwa sio mtanzania wa asili.Itakuwa ni mchanganyiko na makabili ya wakimbizi,waliongia Tanzania.Watanzania ni waaminifu sana.Fikiria wapo waliofanyakazi kwa wahindi,wazungu na waarabu,na wanawachiwa nyumba zenye vitu vya thamani kubwa,na wenyewe wanasafiri nje ya nchi,hata mwaka mzima,wakirudi wanakuta kila kitu kiko,kama walivyokiwacha.Chunguza vizuri hao wasio waaminifu,watakuwa Wana asili ya wahamiaji,wakimbizi kutoka nchi nyingine.
 
Nyimyi watanganyika kazi zenu ni wizi na ujambazi ndio maana uaminifu kwenu ni zero tofauti na wazanzibar wanavoaminiwa ndani ya nchi yao mpaka njee ya nchi yao
Huyo sio mtanganyika. Mtanganyika ni mtu mwaminifu sana.Tatizo Tanganyika inapakana na nchi nyingi, huwa wanaingia wahamiaji,na wakimbizi kutoka nchi jirani, wakishazaana na kuloea, ukikutana naye kokote duniani ,wanajitambulisha ni Watanzania.
Watanganyika wameachiwa majumba, na wazungu, wahindi, waarabu, wakiwa safari nje ya Tanzania, wakirudi wanakuta lila kitu kiko kama walivyokiacha.
 
Huyo uliyekutana naye siye mtanganyika wa asili.Umekutana na watu wenye asili ya ukimbizi kutoka nchi jirani.Huwezi kupata mtu mwaminifu duniani kama mtanganyika.Wengi wanaachiwa majumba,mali za thamani,na wenye mali wakasafiri nje ya nchi,wakirudi mali,majumba yao,yako kama walivyoyaacha.
 
South Africa ya siku hizi ina watu wema hivyo? Yani umkute mtu analia uende kumuuliza analia nini unamsemesha kizulu then unagunduwa ni Mtanzania unampeleka kwako.

Konda tafadhali nishushe hapahapa nimefika, mwendo wa dereva ni hatarishi.
Teh teh teh teh...dah!...noma sana
 
Kwa namna ulivojibu hapa unaonesha busara kubwa sana,nami niliposoma hapa niliwaza sana na nikangoja utajibu nini,binafsi nimeishi sana SA na hapo park station napajua kidogo ukweli ni kwamba watanzania hatuna sifa njema SA binafsi nilijulikana kama mrundi Capetown tangu naingia hadi naondoka
 
Labda atuelekeze hapo park station jamaa alikua kakaa analia kajiinamia. Labda sio SA
Absolutely his lie. Labda Kama Kuna code kwenye hili andiko lake
Labda code kwa mbali sana ni kuwa jamaa yuko SA ana roho nzuri na anaweza kukusaidia kukutafutia kazi ila kwa Park Station kumsaidia mtu na ukaenda nae hadi kwako na kuishi nae kama ndugu jamaa anastahili tuzo ya nobel
 
Pole sana mkuu kumbe tupo wengi tulio amua kusaidia wenzetu baadae wakatutenda vibaya, da nimeamini Allah (Mungu) mjuzi wa kila kitu Kama alivyotamka kwenye maandiko,

kwakuwa aliamua kutuumba binaadamu kisha akaumba moto akijua kabisa wapo Wapumbavu ambao adhabu yao ni kuwaingiza kwenye huo moto wa jehanamu kwa sababu ya yale maovu waliyo yatenda wakiwa duniani.

Kisha Mungu akasema kwa yule aliyetendewa mabaya na binaadamu mwenzake basi manung'uniko yake au huzuni alizopata baada ya kutendwa basi hayo manung'uniko yako ni Dua tosha itakayomfanya mtendaji asifike popote ikiwezekana kuangamia, mwisho wa kunukuu;
 
Mkuu kuwa makini unaweza kupigwa pia...nenda Malawi bado wamelala ukiwa na hiyo hela utachanga bila pressure nenda Lilongwe au Brantire nadhani pale utaanza kuuza vitu kutoka SA wapo watanzania wanaenda kununua vitu SA ukiwa na mtaji uliosimama unaenda mwenyewe sasa hivi SA sio kuzuri kwa kutafutia maisha kama huna mwenyeji alieanza ila ni rahisi kwa kutokea kwa kuuza bidhaa zake Nchi zingine...
 
Shukran sana mkuu.. Ukweli ni kwamba kati ya watanzania watano basi watatu matapeli, afu wawili waliobaki ndio waaminifu.
 
Mungine alijifanya kunizoea akawa anakuja kila siku dukani nimuungie hela ya kula kwa madai kwamba anaumwa, hana nguvu za kufanya kazi. Siku moja akaniomba nimpe nauli arudi bongo maana kwa hali yake asingeweza kuendelea kuishi Kaburu. Nikaona wazo lake zuri, nikaingia masikani kuwachangisha wabongo wenzetu na baada ya week ikapatikana R1800, na mimi nikaongezea 1200 ikawa R3000. Nikamkatia ticket ya kutoka Kaburu hadi Zambia na pale Zambia nikampa maelekezo ya jinsi atapata usafiri wa kutoka pale Lusaka hadi Dar. Nikampa na vijichenji vilivyobaki kwa ajili ya kula, kunywa na mambo mengine madogo madogo njiani (hiyo ilikuwa kitambo kidogo kabla ya hili gonjwa corona) kwahiyo gharama za usafiri zilikuwa za chini sana. Siku hiyo nikamshindikiza jamaa hadi kwenye stand ya mabasi ya Zambia, tukaagana nikarudi mtaani. Baada ya week kama mbili kuna wana fulani kati ya wale waliomchangia wakaja kunambia kuwa msela wamemuona Durban anazurura tu (nahisi aliiuza ile ticket yake fasta fasta pale stand akajichenga kabla ya gari kuondoka), jamaa alipowaona wale washkaji akajifanya kujificha na wao wakampotezea kama hawakumuona vile. Hao ndio wabongo bwana. Ukitenda wema, wanalipa ubaya.
 

Kuna mmoja alizimiwa simu na mshkaji wake akabakia airport basi simu huku Simu kule akapata mwenyeji alikaa kwa mwenyeji wake baada ya mwezi anataka kumtomb…a mke wa mwenyeji wake akatimuliwa.



Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Watanzania kichomi mimi nimenyosha mikono juu

Rafiki yangu kipenzi baada ya kusikia natafuta mtu wa kuniwekea nguzo ( alama za kiwanja ) aliniletea jamaa yake anayemtumia kwenye kazi mbalimbali. Kwa jinsi nilivyokuwa namwamini rafiki yangu ikapelekea nimwamini hata yule jamaa, nikampa 90K cash za nguzo lakini mpaka Leo hakuna nguzo wala kurudisha pesa.

Mzee mmoja aliniuzia kiwanja hivyo nikamwamini mwanae kwa kumpa pesa asafishe hadi leo shamba halikusafishwa na pesa ikapigwa.

Mwingine alilia shida vibaya sana nimkopeshe 1.5M basi nikaamua kumsaidia cha ajabu mwaka sasa pesa yangu haijalipwa karibu tunapelekana mahakamani.


KAMWE SIJI KUMWAMINI MTANZANIA ...NEVERR
 
Sister.. ma gape kama haya tuna watu wana uhitaji nayo sana sana, nikuombe usikate tamaa kwa ajili ya watu wachache unaweza ukawa msaada kwa watu wengi sana

Mie tena?

Hapana kwa kweli

Mtu anakuchafulia na kukushushia reputation kwa watu wa faida
 
Konda anamroga dereva ili aachiwe gari.
House girl anatamani kuwa mama mwenye nyumba.
Ukimpa mchongo wa kazi, asipokuibia, kukuchafulia cv au kukuumiza basi atataka awe boss wako.

Roho za kimaskini tabu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…