Naapa kuwa sirudii tena kumsaidia Mtanzania -- never!

Naapa kuwa sirudii tena kumsaidia Mtanzania -- never!

Habar zenu ndugu zangu. Ama baada ya salam ningependa kuendelea na kile kilichonifanya niandike uzi huu. Ndugu zangu kama ilivyo ada au kama tulivyofunzwa na misingi yetu ya Taifa kwamba watanzania popote tulipo haijalishi ni ndani au nje ya nchi, sisi ni watu wamoja. Kwahiyo kwa misingi hiyo sisi tulio nje huwa na desturi au utamaduni wa kusaidiana bila kujali tofauti zetu za kikabila, dini, rangi, jinsia au kanda ya mtu anayotokea ilimradi sote ni watanzania na tunatokea kwenye ardhi ya Tanzania basi ni ndugu.

Sasa basi miezi 3 iliyopita kuna kijana aliingia Kaburu akitokea bongo kwa lengo la kuja kutafuta maisha. Kijana anadai kuna rafiki yake wa kitaa, kwa sasa anaeishi Capetown ndio alimshawishi kuja maisha haya, lkn alipoingia tu "Kaburu" yule rafiki yake akamzimia simu na kumkosa kabisa online.

Kijana akachanganyikiwa asijue wapi pakwenda wala nini cha kufanya. Nikiwa katika mizunguko yangu mitaa ya park station Johannesburg, ghafla nikapita sehem na kumuona kijana akiwa kajiinamia na begi lake huku machozi yakimtoka. Nikamsogelea taratibu na kujaribu kumuuliza kwa lugha ya wenyeji, ghafla nikasikia jamaa akiongea kiswahili, hii ikanipa nguvu ya kumsogelea na kumuuliza zaidi baada ya kugundua kuwa naongea na mtu anaetoka nchini kwetu. Baada ya maongezi ya hapa na pale nikagundua kuwa jamaa ameingizwa cha kike na mwenyeji wake, kwahiyo nikachukua jukumu la kumsaidia.

Nikaondoka na jamaa hadi nyumban, akaoga, akala, baada ya kula nikampa sehem ya kupumzika akalala. Kwa kuwa mimi nina familia ikanibidi niende kuongea na homeboy fulan ambae ni single ili ampe hifadhi ya miezi kadhaa wakati nikiendelea na mchakato wa kumtafutia shughuli ya kufanya, mshikaji akakubali lkn kwa masharti ya kumsaidia kulipa rent.

Kwa kuwa nilikuwa nimeamua kumsaidia kijana, basi nikaona poa tu acha nimsadie kulipa rent ili aweze kuishi nae. Kijana tumekaa nae mwezi wa kwanza, wa pili na sometimes nilikuwa naenda nae kwenye mishe zangu ili kumzoesha mazingira ya nchi, na mishe za hapa na pale. Mwezi mmoja uliopita kuna rafiki angu Mkenya ambae tuliwahi kufanya nae kazi huko Gezina, Pretoria.

Mkenya alikuwa anatafuta mtu wa kumuachia saluni yake kubwa na ya kisasa iliyopo nje kidogo ya jiji la Pretoria huko Nellmapius, kwa malipo ya R600 kwa week (sawa na sh elfu 85 au elf 90) kula na kulala bure. Kwa vile nilikuwa na kijana na tayari alishanambia kuwa bongo kazi yake kubwa ilikuwa ni ukinyozi, nikaona YES maji ya mvua yameangukia juu ya mgongo wa bata. Nikampanga kijana, kesho yake mapema nikampeleka mpaka Pretoria kwa yule Mkenya na kumkabidhi.

Kweli bwana baada ya siku mbili kijana akaanza kazi huku Mkenya akiniomba nimtafutie vijana wengine ambao wataenda kusaidizana nae, maana saluni ni kubwa ilihitaji vinyozi zaidi ya watano, lkn pia kijana lugha ni tatizo, so alitaka ambao wangeweza pia kusaidiana hata katika mambo ya lugha za wenyeji ili kuwateka vizuri wateja wa kizawa.

Nikamuahidi jamaa kumtafutia hao vijana. Wakati namuacha kwa yule Mkenya kijana wang nilimuachia sim kwa ajili ya mawasiliano yetu, au ndugu zake wa bongo, au boss wake (Mkenya). Dogo tukawa tunawasiliana ananipa taarifa za kazi na mimi nampa mpa moyo kuwa akomae ili atimize malengo ya kile kilichomleta hapa nk. Siku tatu zilizopita sikumpata online, nikajua labda simu imepata tatizo ghafla.

Sasa jana yule rafiki angu Mkenya amenipigia simu na kuniambia kuwa jamaa amemuibia kila kitu cha saluni, na hela ambazo yule Mkenya anaendaga kuzichukua kwa week jamaa katimka nazo. Simu yake haipiti na hatujui tutamtoa wapi. Nilipotaka kumlipa yule Mkenya nusu ya hasara ya vitu alivyoiba jamaa, Mkenya amkataa amesema nisijali kwa vile sio kosa langu ni kosa la mtu mungine kwahiyo mimi sistahili kumlipa na ukizingatia na rafiki yangu.

Hiki kitendo cha huyu jamaa kimenisononesha na kunivunja nguvu. Imenifanya sasa niwachukie wabongo wenzangu, maana hii ni mara pili sasa nawasaidia wabongo afu wanaharibu na kutimkia kusikojulikana, japo kwa huyu sikutegemea hata kidogo kutokana na upole na muonekano wake.

Najua binadamu tunatakiwa tusamehe, lkn kwa mikasa hii sioni sababu ya kusamehe kwa lengo la kurudi kumsaidia mungine labda yule nimjuae A to Z. Ndugu zangu wabongo tubadilike, hii dunia tunapita tu. Kumuharibia mtu anaekusaidia sio ujanja bali ni ujinga wa mwisho. Hii ni tahadhari nimetoa kwa vijana wengine kuwa makini sana. Asanteni


Niliwahi kutoa tahadhari ya kuwa Wabongo hawasaidiki sababu ya tabia za kuharibiana. Pole sana
 
Honestly speaking waTanzania wengi wanapenda shortcut

Siyo kwenye kazi
Kwenye biashara
Mpaka kwenye mambo ya kijamii

Kuna mmoja nilimpeleka godown fulani akapiga mzigo imekuja julikana too late na deni nikalibeba

Mimi nikisikia opportunity nakausha tu kuepuka lawama. Kisha utasikia waTanzania hatupendani.
Kuna jamaa alikuja home akidai ni yatima hana wazaz amekuja daslam kuhustle maana wadogo zake walikuwa wanamtegemea(first born) alikuwa analia kwa uchungu sana. Sister akamuonea huruma akamuweka kwenye biashara yake akimchukulia kama mdogo wake..... Lakini mwisho wa siku aliondoka na kila kitu
 
Honestly speaking waTanzania wengi wanapenda shortcut

Siyo kwenye kazi
Kwenye biashara
Mpaka kwenye mambo ya kijamii

Kuna mmoja nilimpeleka godown fulani akapiga mzigo imekuja julikana too late na deni nikalibeba

Mimi nikisikia opportunity nakausha tu kuepuka lawama. Kisha utasikia waTanzania hatupendani.
nipe na mm mchongo bas mwanang
 
Mr Dudumizi huyo mshikaji uliyemsaidia kupata kazi kauawa kwa kutolewa kafala/biashara ya viungo, na mkenya kasingizia kamuibia. Huyo mkenya hiyo itakuwa ni side business kwa ajili ya viungo etc. Muepuke huyo Mkenya hata wewe atakuja akuue auze viungo.
Taarifa zako zinaogopesha sana...! Zinautafiti wa kutosha ? Embu funguka zaidi...!
 
Mtu haanzi wizi mkubwa hivyo mara moja tena nchi ya ugeni huwa wanaogopa. Jina lake ni nani? Weka na picha yake hapa. Na police taarifa mmetoa wakasemaje? Kama kweli imetokea huyo ni jambazi mkubwa sana na mwisho wake ni kifo tu. Hata hio story utakuta alitunga. Alikuwa south africa muda mrefu akakulia njari akijua ww ni mtz nk. Dunia ina mambo ya ajabu sana.
Uko sahihi kabisa
 
Mtaumiza akili na vichwa vyenu bure, South Africa ndio chimbo pekee ambalo ni rahisi kwa hawa Notorious wetu wa Bongo kukimbia Bongo na kuingia huko kwa njia za panya na wengine hufia njiani kwa kuuliwa na viboko wakati wa kuvuka mito hatari.

Haiwagharimu kiasi kikubwa cha pesa kuingia huko maana hawahitaji hata kupita official borders au airport, wao ni waruka fence ( South Africa border yote wamepiga wire fence.)

Kwahiyo chimbo hilo tegemea tabia zote za kishenzi unazozijuwa wewe Bongo utakutana nazo huko, dawa ni kukaa mbali na Wabongo kama una mishe zako na wazungu au mataifa mengine.

Hii ni tofauti na Europe na USA, process za kuingia hicho hizo zinawanyima fursa wajinga wengi kutobowa huko unless aingie kwa kuzamia meli, na kwa teknolojia inavyoshamishiri nadhani hata uzamiaji meli utafika tamati.
Duuh mkuu haid sasa kuna watu wanazamia Europe na US kwa meli...! ? Si itakuwa rahisi kukamatwa?
 
wanijeria wanaosifika kwa wizi na mtandao mkubwa wa kitapeli duniani. Sehem wanayopigia mishe zao, wakiona kuna wabongo wawili watatu wamejisogeza eneo hilo basi wanajeria wanaihama hiyo sehemu ili kunusuru biashara zao.
Hahahahha.. 😃😃😃🇹🇿wanaogopa nini sasa??
 
Mkuu nataka kuja SA naomba nisaidie ila mimi nakuja na kianzio ili nisiwe mzigo kwako nimejichanga changa nmepata 1.5M ya kiTz na hela ya nauli pemben ila nmekua mzito kuja huko maana sijawahi kufika huko na sina ninae juana nae huko na nmeskia wa Tz weng wa huko unaweza ukafikiri n msaada kumbe umejipeleka kwenye mdomo wa mamba ila ww nahisi utakua tofaut kutokana na moyo wa kusaidi nataka nianzishe hata kuuza matunda tu ila nahitaji masaada wako unipe muongozo tu.
Ukipata connection nzuri ya watu wanaojitambuwa na wewe ukiwa humble, plus muongeaji mzuir na watu ya mwepesi kumwin mtu.. utafanikiwa haraka huko
 
Lakini SA mbona hakuna complications kuingia?? Kinachowafanya hawa ndugu zetu kupita hizo njia za hatari mpaka wengine kuliwa na viboko ni nini??
Complications zinaaznia kwenye PASSPORT...hahaha vijana wengi wanozamia una kuta wakifika pale uhamiaji zile process zinawashinda vigezo na masharti!

Mwingine hiyo 150 anaona bora aitumie kama nauli safarini.. so unakuta hawana papers
 
Hahahahha.. 😃😃😃🇹🇿wanaogopa nini sasa??
Wanaogopa kupigwa mazima mkuu. Mbongo akipata mwanya kidogo wa kujua unga ulipo, basi kitachofuata ni maumivu kwa wanijeria.
 
Mkuu kuwa makini unaweza kupigwa pia...nenda Malawi bado wamelala ukiwa na hiyo hela utachanga bila pressure nenda Lilongwe au Brantire nadhani pale utaanza kuuza vitu kutoka SA wapo watanzania wanaenda kununua vitu SA ukiwa na mtaji uliosimama unaenda mwenyewe sasa hivi SA sio kuzuri kwa kutafutia maisha kama huna mwenyeji alieanza ila ni rahisi kwa kutokea kwa kuuza bidhaa zake Nchi zingine...
Mfano wa bidhaa unazoweza kutoka nazo SA na kuuza Malawi?
 
Kuna mmoja alizimiwa simu na mshkaji wake akabakia airport basi simu huku Simu kule akapata mwenyeji alikaa kwa mwenyeji wake baada ya mwezi anataka kumtomb…a mke wa mwenyeji wake akatimuliwa.



Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Daah we jamaa unazingua bana 😂😂😂😂🇹🇿👍🏾
 
Back
Top Bottom