Hawa manabii na wafuasi wao ni watumiaji wazuri wa usemi wa "Fuata maneno yangu usifuate matendo yangu"
Mama ananiambia nikitaka maisha yanyooke nianze kwenda kanisani lakini ninapoishi nipo karibu na kanisa kiasi kwamba wakihubiri au wakiwa wanafanya mazoezi ya kwaya nasikia.
Naingiaje kanisa ambalo mahubiri yake ni juu ya coincidences? Juu ya kumuaminisha muumini kwamba hata kama haufanyi kazi Yesu anakufanyia njia kuelekea mafanikio? Jamaa anakuambia "Umekuja hapa hauna pesa lakini ukirudi nyumbani utashangaa unaitwa ukale na mtu usiyemjua. Muamini Mungu unaweza kutembea ukaenda kuokota pesa ukiwa njiani"
And this guy ni anaweza kunena kwa lugha akiamua yaani sekunde hii unamsikia "Wachawi wakukalie mbali, nautuma moto ulio mkuu" sekunde inayofuata ni "Araeahsj akdkfjdjs aufifkdhs gyudjdisjshydj" and then next second anatoka kwenye kunena anarudi kwenye kiswahili.
Kisha akiamua anaanza tena kunena kwa lugha.
Hizi dini za mlima wa moto wakati zinaanza ilifika kile kipindi cha kunena kwa lugha, nakumbuka aliyeanzisha hii tabia ni marehemu, na wengine wakaidakia. Ikawa kwamba kama hauongei vitu visivyoeleweka basi wewe siyo nabii.
Ni upuuzi tu. Now katika saikolojia inaelezwa kwamba ukiukumbatia sana uongo mwisho unaanza kuuamini. Hivyo Gwajima kuamini ana uwezo wa kufufua watu mpaka kujitangaza siyo bahati mbaya actually a nigga believes anaweza fufua mtu akija pigwa kibao cha shavu na reality ndiyo unaona hizo drama zimepungua ameswitch kwenye kuchamba watu.