kwa kawaida, sijawahi kwenda pale kwa flora. nimekuwa mbali na dsm kwa kitambo. lakini hapa duniani kuna manabii wengi tu, wengine kweli wanaweza kuwa manabii wa Mungu, hatukatai wapo. ila wengine pia wanaweza kuwa hawajatumwa na Mungu hao pia wanaweza kuwepo.
however, naomba kila atakayesoma hapa anisikilize vizuri. SIO KILA NABII, HATA KAMA AMETUMWA NA MUNGU ANAWEZA KUKUBALIWA NA WATU WOTE. ukiangalia sifa za manabii karibia wote, huwa wanachukiwa na kusemwa mengi. nabii ambaye hasemwi na hana maadui, huyo unaweza hata kumtilia shaka, iweje asiwe na maadui wakati shetani yupo?
anayejua kuwa mtu fulani ni nabii, ni Mungu, na anayejua kuwa yeye ni nabii ni yeye yule aliyetumwa. mfano, leo hii mimi nikiitwa na Mungu kuwa mtumishi wake, ni mimi ndiye nitakayejua na nitakuwa na a hundred percent ya uhakika kuwa mimi ni mtumishi wa Mungu, hivyo hata watu waseme vipi, sitawasilikiza na sitawaogopa kwasababu nina uhakika.
hivyo kwa manabii na mitume, wao ndio wanaojua kama wametumwa na Mungu au la, hatukuwepo siku wanaitwa na Mungu kuwa watumishi wake, hatujui waliitwa kwa njia ya maono ya mchana au ya usiku au walikutana vipi na Mungu hata wakaanza kufanya huduma hizo.
cha muhimu kwako wewe mwanadamu ni kunyamaza kimyaaa tu kwasababu haukuwepo siku ile wao wanaitwa. hivyo hauna uhakiki wa unachosema zaidi ya kuguess tu. hata kama tunatakiwa kuwatambua kwa matunda yao, desturi zilizotujaa wanadamu wakati mwingine utakuwa watu wanawepa Bible pembeni wana value mtu kwa kupitia desturi na mapokeo. cha muhimu ni kumwomba Mungu akufunulie wewe binafsi kabla hauja comment, usijekuwa unacomment negative ukawa kumbe unamsema mtumishi wa Mungu. ili uwe na uhakika, nenda mbele za Mungu mwulize akufunulie, utapata jibu. ukiona unapapenda mahali nenda kasali, ukiona haupapendi, usiende, neda kule unakokupenda, ila wale ambao wanasali mahali usipopapenda waache waendelee bila kuwasema, kwasababu haina maana ya kuwasema wanaosali mahali ambapo wewe hausali wakati pengine wao hawapasemi mahali ambapo wewe unasali.
Mungu atusaidie tuwe na busara kuchagua wapi tusali, na tusali mahali pale tu ambapo Mungu yupo, na watumishi kweli ni wa Mungu. jambo hili ni la muhimu sana. ukisikia sehemu kuna dhahabu ukawa mbishi wenzio wanaenda kuchimba wewe hauendi, siku itakapoisha ile dhahabu utaenda na utakuta haipo tena, cha muhimu ni kwenda ukaone kama dhahabu ipo kweli, na uchukue mercury utest kama ni dhahabu au feki, ndipo utakuwa na ujasiri wa kuwadhihaki na kusema kule hakuna dhahabu bali ni feki, na ukiona ni dhahabu safi, utakuwa umeipata kabla haijaisha.....Mungu ibariki tz. bofya hapa
www.sheriakwakiswahili.blogspot.com