Wanabodi
Tukubali tukatae watu hatulingani, kuna watu wana nguvu kama za upako fulani, baadhi ya kauli zao ama zina umba, ama zina maono.
Mmoja wa watu hawa ni Godbless Lema, ila kama kawaida nabii huwa hakubaliki nyumbani!, inawezekana huyu Godbless Lema ni kama nabii fulani ?.
Alianza na ile ndoto yake fulani, ikatimia!, akaja na issue ya Sabaya, ikatimia!, Sasa amekuja na issue ya Makonda, je Itatatimia?
Msikilizeni hapa
View: https://youtu.be/nGgpxUj3JLc?si=QckVGgJFSWHoypzM
Nashauri, asipuuzwe, ila kama wana ushahidi, si wa upeleke kunakohusika ili uchunguzi wa kijinai uanze.
Paskali