Nabii kiboko ya wachawi, naona anafanya maigizo

Nabii kiboko ya wachawi, naona anafanya maigizo

Ni kweli...
Lakini unapokuwa mkubwa na kuwa na utashi, unaruhusiwa kuutafuta ukweli na kuambatana nao...
Ni vile tu sema wengi wetu ni casual au shallow believers, tukizaliwa tu dini fulani basi tunashika hicho hicho hadi ukamilifu wa maisha yetu...



Mkuu ukiona mkristo anadharau au kumsema vibaya yule asiye wa imani yake, basi ujue huyo si mfuata neno la Yesu Kristo...kama ilivyoandikwa na nanukuu mafunzo ya Kristo mwenye

Luka 10
27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.
We mtu! nilikuwa sijakujua vizuri!safi sana na hii ndio amri mpya"Upendo"
 
Samahani nabii Kiboko ya uchawi, mbona nakusikiliza hapa hii kama futuhi?

Aiseee huu ni mchezo wa kuigiza kabisaaa. Eti bibi katoka kijijini amefikia Kwa mwanae, Kuna watoto watatu wamefariki, wawili walishazikwa na Sasa Kuna msiba wa mtoto mwingine,baada ya kumpigia simu nabii ndio anasema bibi anaua watoto wa mwanae.

Basi eti mke analia, mume ambaye ndio mtoto wa mama mkwe anajifanya haelewi Kwanini mama yake anakula watoto, hiyo drama Sasa ya huyo bibi mla wajukuu sasa anavyoongea🥺

Basi nabii akapiga maombi kwenye simu , mtoto wake anasema kwenye simu bibi kala mweleka, damu zikaanza Toka puani, nabii ananena Kwa lugha na kumpa option mbili, afe au aseme ukweli, bibi ndio kuanza kusema Samahani, nimekumbuka Leo,Basi anaambiwa arudishe mtoto.
Sasa basi mtoto aliyefariki kaombewa na nabii Ili afufuke, basi mtoto si kafufuka bwana,
was a Nice Drama! Hiiii kuchelewa kulala Kuna mengiii.....

Anyways, naomba tukipata muda tutafakari mstari huu

MATHAYO7:15-29.
😅😅😅😅😅
Kuna wimbo aliwahi kuuimba Rev.Jangalason unaitwa Dini kabuli ...kautafute usikilize 🤣🤣🤣🤣
 
Ukiwa umeokoka haupaswi kuwa na mashaka na huduma yoyote ya kiroho , au mtumishi yoyote usiwe na mashaka nae
Hapana sio kweli, bibilia inatutaka tuyachunguze maandiko, tusiziamini kila roho bali tuzijaribu na kuzichunguza kama zimetokana na Mungu au la.Ukiwa mtu wa kila kitu ruksa, hata kafara watakutoa hawa manabii.
 
Nasikia kila mtu ana ndoo ya maji hapo kanisani, pamoja na kitambaa chake...

Maana mtu anaangalia wachawi wake kwa ndoo na hicho kitambaa...

Hata wanaopiga simu pia wanatakiwa wafanye hivyo...
Usanii mtupu, watu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa sahihi ya neno la Mungu. Kanisa limegeuka pango la majizi badala ya nyumba ya sala.
 
futuhi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] ilo neno limenichekesha sana mpka kamasi likatoka kama pulizo mbele za watu.
 
Mungu alishasema tusitegemee wanadamu, Wa kumtegemea ni Mungu tu. Hao manabii washakuwa kama waganga wa kienyeji.
 
Back
Top Bottom