Nabii Malisa aelezea jinsi alivyomfufua mama yake mzazi mara 3

Ubwege huu
 
Sishangai kwa prophet kumfufua mtu.. lakini kwa jinsi alivyo wasilisha shuhuda yake inaleta utata... But tusikatae wala kukosoa.. Tuendelee kuyaishi maisha, kwani Mungu ni wakwetu sote.. kuna nabii mmoja anakauli yake anasema "Mungu anawatu wengi"
Mungu angekuwepo, isingehitajika kumfufua mtu.

Mtu asiyetaka kufa, asingekufa.

Mtu asiyetaka kufa akifa, huo ni ushahidi Mungu hayupo.

Umeelewa?
 
Haya ahsante nabii haya wenye dini yenu hongereni kwa kufufua watu kweli omba mungu akupe akili hii dini ni ya mazwazwa kama MK254
 
Unataka kusema mungu hayupo??
Mungu ni hadithi iliyotungwa na watu.

Mungu huyo mnayemsoma kwenye Biblia na Quran (muweza yote, mjuzi wa yote, mwenye upendo wote) ukimpima kimantiki unaona kabisa hayupo, kuna contradictions za kimantiki zinaonesha kirahisi tu kwamba huyo Mungu hayupo na hawezi kuwepo.

Tatizo watu wamerithishwa uongo kwamba yupo kwa vizazi na vizazi inakuwa vigumu kukubali kwamba hayupo.

Kwenye saikolojia hiki kitu kinaitwa "cognitive dissonance".
 
Angekuwa Rwanda, Kagame asingemuacha uraiani
Malisa anatekeleza haki yake ya kikatiba na kibinadamu. Uhuru wa kuabudu. Hii ni haki ya kikatiba, pia ni haki ya kibinadamu iliyopo katika Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Hakuna kosa alilofanya hapo.

Kagame anakosea sana kuingilia haki za watu za kibinadamu.

Huwezi kufuta ujinga kwa sheria na ubabe.

Ujinga unafutwa kwa elimu.

Haya makanisa ya kina Malisa ukitaka kiyafungia, yataenda underground usiyaone, yafanye mambo yao sirini, ukose hata kujua kinachoendelea.

Kanisa lina uzoefu mkubwa sana wa kufanya kazi underground, ndipo lilipoanzia, Ufalme wa Kirumi ukalifungia, mpaka Mfalme Constantine mwenyewe akalokuhali.
 
Kwa akili hizo ndio maana mnaambiwa Abdul ni delegate wa serikali kwenye msafara ulioenda Dubai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…