Nabii Mashimo amtaja Malisa GJ kama mrithi wa Paul Makonda

Nabii Mashimo amtaja Malisa GJ kama mrithi wa Paul Makonda

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Huko kwenye viunga vya Instagram tayari Mchungaji wa taifa na nabii komandoo Mashimo ametamka wazi kwamba kijana na kada wa CHADEMA, kamanda Malisa GJ kuwa mrithi wa RC mstaafu Baba Keagan. Mimi kama mwanafunzi wa shule ya uongozi chini ya mwalimu mkuu Komredi POLEPOLE nimefurahishwa na tamko hili la kinabii.

Ikumbukwe Nabii Mashimo ametamka hayo wakati akimtakia heri ya kuzaliwa kamanda Malisa (Happy birthday to you). Nabii ameweka wazi kwamba kwa jinsi Malisa anavyojitolea maisha yake kusaidia watu wenye shida mbalimbali wanaomfikishia shida zao basi anapaswa kuitwa mrithi wa RC mstaafu Makonda ambaye enzi za uongozi wake alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kila shida inayopelekwa kwake basi inapatiwa ufumbuzi.

Mimi naunga mkono hii kauli ya kinabii kwa sababu wote ni mashahidi wa alama za upendo ambazo Baba Keagan aliziweka kwa watu wa mkoa wake kipindi chote cha uongozi wake. Malisa GJ nae anapita mulemule alikopita RC mstaafu. Huyu kijana kafanya mambo makubwa mno kwenye kugusa maisha ya wengine.

Nampongeza Mchungaji komandoo Mashimo kwa hili suala la kiroho alilopost. Nampongeza sana pia kamanda Malisa kwa moyo wake pia namtakia mema kwenye siku yake ya kuzaliwa. RC mstaafu nampongeza kwa kuonyesha njia.

Mashimo.jpg
 
Mashimo wasitake kumchafua huyu kijana

Mashimo alitajwa kwenye kesi ya Sabaya ya kutesa watu
 
Kumfananisha Shetani Bashite na Mtumishi wa Mungu Malisa ni Sawa na kumfananisha Shetani na Malaika

Kumbukeni Mashimo pia ni Shetani wa kutupwa
 
Ila mashimo amekomaa hadi amefikia level ya unabii?😂.

Yaani sasa hivi nabii mashimo ni level moja na kina musa, isaya, yakobo, suleimani, Daudi, enock na manabii wengine wa kiyahudi wa zamani😂😂.

Wakristo, wayahudi na waislamu hua wanasoma maandiko ya hao manabii wa zamani, Mashimo atoe maandishi yake yasomwe kwenye makanisa na misikiti yote watu tufuate maelekezo yake nambii mkuu Mashimo😂
 
Back
Top Bottom