Nabii Mkuu Dkt. Geordavie kuwashika mkono wafanyabiashara zaidi ya 5000 soko la Samunge, Arusha

Nabii Mkuu Dkt. Geordavie kuwashika mkono wafanyabiashara zaidi ya 5000 soko la Samunge, Arusha

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
468
.
Zaidi ya wafanyabiashara 5,000 wanaofanya biashara katika soko la Samunge jijini Arusha wanataraji kupatiwa mitaji ya kuendesha biashara zao na mhubiri maarufu nchini Nabii Mkuu Dkt GeorDavie.

Mbali na kupatiwa mitaji hiyo pia mhubiri huyo anataraji kutoa msaada wa kukarabati miundombinu ya malango ya kuingilia ndani ya soko hilo kama njia mojawapo ya kusaidia jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la Samunge,Joram Miraji amesema kuwa uongozi wa soko hilo hivi karibuni ulimwandikia barua ya maombi ya kuwasaidia mitaji wafanyabiashara ndani ya soko hilo pamoja na kusaidia kukarabati miundombinu ambapo ombi lao limekubaliwa.

Miraji amesema kuwa baadhi ya wafanyabiashara ndani ya soko hilo hawana mitaji kufuatia soko hilo kuungua mwaka 2019 na kuteketeza mali zao.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa wafanyabiashara wengi ndani ya soko hilo wanaishi kwa mateso kufuatia kudaiwa mikopo na baadhi ya benki nchini hali ambayo imepelekea kero na usumbufu kwa uongozi wao.

Miraji amesisitiza kuwa hatua ya kumuandikia barua Nabii Mkuu Dkt GeorDavie imekuja baada ya kuona anasaidia makundi mbalimbali kwenye jamii hivyo na wao waliona wamuandikie barua na tayari wameshapatiwa majibu kuwa atawatembelea.

Naye mweka hazina wa soko hilo ,Amos Julius amesema kwamba soko lao linakabiliwa na changamoto ya miundombinu hususani malango ya kuingilia na kupelekea baadhi ya wafanyabiashara kuibiwa bidhaa zao.

“Soko liko wazi sana na hii imepelekea baadhi ya wezi kupenya na kuchukua bidhaa za wafanyabiashara hivyo tunamuomba Nabii Mkuu Dkt GeorDavie atusaidie katika hili “amesema Julius

Mfanyabiashara Upendo Remy amesema kuwa pindi moto ulipounguza soko hilo alijikuta akipata hasara ya sh 500,000 na sasa anaishi kwa mikopo.

Naye Agripina Kawalla amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mitaji ya kuendesha biashara zao na endapo Nabii Mkuu Dkt GeorDavie akiwashika mkono watainuka kiuchumi.

Hivi karibuni akiwa katika ibada katika huduma yake ya Ngurumo ya Upako Nabii Mkuu Dkt GeorDavie alitoa kauli ya kufanya ziara ya kutembelea soko la Samunge na kuwasaidia changamoto mbalimbali kama mitaji wafanyabiashara waliopo ndani ya soko hilo.

B67D875E-6D00-45DA-82C3-A4C6B2A7647B.jpeg

Mwisho.....
 
Sasa naona utitiri wa wasanii , sio wa mziki wa kizazi kipya sio wa bongo fleva , wakimiminika kwà wingi kwenda kwake. Je ni ile misaada ya pesa ndiyo inawavuta huko au ni neno la Mungu?


Nashauri Nabii Jo' awe makini sana katika hili. Target yake ni vyema ikawa kwenye kufocus ktk kuyafanya mapenzi ya Mungu na kuyahuisha. ( Doing the will of God & Upholding it)

"MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA".


IMG_20220930_070401.jpg


Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Sasa naona utitiri wa wasanii , sio wa mziki wa kizazi kipya sio wa bongo fleva , wakimiminika kwà wingi kwenda kwake. Je ni ile misaada ya pesa ndiyo inawavuta huko au ni neno la Mungu?


Nashauri Nabii Jo' awe makini sana katika hili. Target yake ni vyema ikawa kwenye kufocus ktk kuyafanya mapenzi ya Mungu na kuyahuisha. ( Doing the will of God & Upholding it)

"MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA".


View attachment 2374726

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
Washauri wa namna gani nabii Mkuu atumie pesa zake mmeanza , mshauri basi na namna ya kupata pesa.
Acha wamiminike wewe unadhurika na nini hadi uwe mshauri wa huyo nabii?
Unajua anazipataje?
 
Back
Top Bottom