Pre GE2025 Nabii Sanga: Mgawanyiko mkubwa utaikumba CCM mwaka 2024 na 2025, tuiombee

Pre GE2025 Nabii Sanga: Mgawanyiko mkubwa utaikumba CCM mwaka 2024 na 2025, tuiombee

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM wakifarakana itakuwa ni ahueni kwa Taifa. Hii CCM ya nyakati hizi ni shetani anayewatesa sana Watanzania.

Tuombe wafarekani bila ya kuleta madhara kwa nchi.
Yaani kifo Chao kiwe Cha kimya kimya,

Wasife kifo Cha punda Cha kurusha mateke!!
 
hakuna umuhimu wowote kwa chadema kuichunguza ccm, kwasababu hakuna kitu chadema wasichokijua kwa ccm, na hata kujua kwao hakuna madhara yeyote kwa ccm. ukweli uliopo ni kwamba msigwa na yeyote anayeondoka wamechoka na umwinyi wa mbowe na soon hata Lisu ataondoka ama la, atakuwa kimyaaa harakati zote ataziacha. why? baada ya kulamba asali.
CCM ina hazina kubwa sana ya wapumbavu ndiyo maana wanachukua watu toka Chadema kwenda kuwapa teuzi huko
 
Ndicho watu wanachoomba! Chama pendwa kigawanyike vipande vipande kife kabisa.
 
Amesema pia kuwa, mgawanyiko na mtikisiko utakaokikumba chama Cha MAPINDUZI CCM, haitakuwa Siri, itakuwa ni mtikisiko wa wazi ambao hata raia wa kawaida watajua.

Amesema Mungu amemwambia awaase raia kukiombea Chama Cha MAPINDUZI CCM Kwakuwa mtikisiko wa chama tawala utaathiri pia Nchi Kwa ujumla, na ujumbe wa kukiombea CCM ni Ishara kuwa Mungu BADO anapenda CCM iendelee kuongoza Nchi na amesema kuwa, adui amepanga kutumia mgawanyiko huo kuivuruga Amani ya nchi.
Mbona mtikisiko ni kawaida hata 2010, 2015 na 2020 ilitokea lakini chama chetu kikavuka kwa magoli ya mkono
CC Lucas Mwashambwa
 
Kuwatumbua wale vigogo si ni kujipalia mkaa?
Nguvu ya Mamba kumayi 😅🙏
Nje ya system watakuwa hoi bin raanan kama Mzee wetu wa karibu na Kibaigwa !
Mzee ametulia tuli kama maji mtungini !
 
Mtikisiko ukitokea ndani ya CCM itakuwa ni jambo jema kwa Tanzania. Tukipata vyama viwili, kambi mbili, at least mojawapo inaweza kuanza kujali maslahi ya taifa na kuacha kuishi kwa mazoea.
Hayati Mwalimu Nyerere ndio aliyasema haya. Kuwa upinzani wa kweli utatokea pale CCM itakapopasuka katikati. Hivyo maombi yawe kinyume na maneno ya huyo mtumishi wa mungu.
 
Hakuna mwenye akili na hofu ya Mungu atapoteza muda wake kuwaombea hawa CCM kwa haya waliyowafanyia wananchi wasio na hatia.

Wapambane tu na mkono wa Mungu kama zamu imeshafika.
 
Salaam, Shalom.

Katika Unabii wa mwaka 2024, Nabii Sanga ametoa ujumbe Kwa Watanzania kuingia katika maombi kukiombea chama tawala CCM, amesema ameambiwa kuwa mwaka huu 2024 kutakuwa na mgawanyiko mkubwa utakaokikumba chama hiki.

Amesema pia kuwa, mgawanyiko na mtikisiko utakaokikumba chama Cha MAPINDUZI CCM, haitakuwa Siri, itakuwa ni mtikisiko wa wazi ambao hata raia wa kawaida watajua.

Amesema Mungu amemwambia awaase raia kukiombea Chama Cha MAPINDUZI CCM Kwakuwa mtikisiko wa chama tawala utaathiri pia Nchi Kwa ujumla, na ujumbe wa kukiombea CCM ni Ishara kuwa Mungu BADO anapenda CCM iendelee kuongoza Nchi na amesema kuwa, adui amepanga kutumia mgawanyiko huo kuivuruga Amani ya nchi.

Amesema pia, amepata ujumbe kuwapa Marais wote wa Africa kuwa Waaminifu Kwa Nchi zao na kuwatumikia wananchi Kwa HAKI, la sivyo, patakuwako maandamano katika Nchi nyingi Afrika ikiwa hawatakuwa Waaminifu.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni.🙏

Source: POG family Tv.
"Expired date" ya Chama Cha Makafara ilikuwa toka mwaka 1999, lakini kikaendelea tu kuwepo kwa "user by date" mpaka mwaka 2015. Toka 2016 kimegeuka kuwa "reject" ila kipo kipo tu ndani ya mbeleko ya vyombo vya dola.

CCM ni muflisi na hakijachoka tu kama chama dhoofu kifikra na kimaono, bali pia kimechokwa na Watanzania waliokuwa wengi. Ukiona kauli ya kiongozi mwandamizi ambaye ni waziri na mNEC akijinasibu na mbinu haramu za kubakia madarakani, basi tambua kuwa kimegeuka kuwa siyo tu "reject" bàli pia ni "poison par excellence"

Kufanya maombi kwa chama hiki ni kama vile ni kujitakia kuonja sumu. Kukichagua chama hiki ni sawa kabisa na kunywa sumu. Gen Z kazi kwenu, ni lazima mjihamasishe ili kuliondoa zimwi hili.
 
Back
Top Bottom