Nabii Shilla afanye unabii wake bila uchochezi. Yaliyoamriwa kijeshi asiyatumie kama mtaji wa kujipatia waaumini

Nabii Shilla afanye unabii wake bila uchochezi. Yaliyoamriwa kijeshi asiyatumie kama mtaji wa kujipatia waaumini

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Mimi kama mwanainchi nimesikitishwa sana na moja ya unabii wa kijana anayejiita Nabii shilla!

Katika sehemu ya unabii wake akiwa madhabahuni Nabii huyo anasikika akimtabilia mtu mmoja (muumini wake) kuhusu namna alivyofukuzwa kazi katika jeshi la polisi huko Moshi.

Ukimsikiliza vyema nabii huyo utagundua hakuna unabii anaoufanya pale zaidi ya kueleza taswira aliyosimuliwa na muumini wake namna alivyofukuzwa kazi ndani ya jeshi la polisi kwa tuhuma za Rushwa na makosa mengine.

Miongoni mwa maelezo ya unabii wa kijana Shilla, anadai mtu huyo (muumini) alionewa kwa kubambikiwa tuhuma za rushwa kutoka kwa wakubwa kwa kuwataja baadhi ya makamanda akiwemo aliyekuwa kamanda wa mkoa wa Kilimanjaro miaka 6 iliyopita!

Hivyo nabii huyo anatumia video hiyo kuwaomba viongozi wakuu wa kitaifa kuingilia kati maamuzi ya kufukuzwa kazi ya upolisi kijana huyo pasipo ushahidi wa kukamatika na rushwa ya 5.4mil. (Kwa maelezo ya unabii wake)

Kwa maoni yangu kama mwanaichi naomba anaemjua nabii huyu!

Mwambieni huu siyo unabii Bali ni uchochezi!

Tukio zima la kijana huyo nabii shilla kalieleza yeye kwa mgongo wa unabii, kwasababu yule kijana anafaham wazi kabisa angeeleza yeye tukio hill waziwazi kinidhamu ya kijeshi angeonekana kama mhaini. (Hivyo alimusimulia Nabii wake na kufanyika kama unabii kwa maslahi yao)

Mwambieni kama nabii azingatie mipaka, yaliyoamriwa kijeshi asiyaingilie kwa mihemko kutafta waumini jambo linaloweza kuleta taharuki jeshini na kuhatarisha Amani!

Mwambieni nabii shilla! Siyo lazima kamanda anayefukuzwa kazi ya upolisi au jeshini lazima akamatwe handled akiwa na ushahidi mkononi, Bali kitendo cha tuhuma nzito kujirudia kwa kamanda mmoja kinatosha kumfukuzisha kazi!

Halafu isitoshe makamanda kwasababu wanaelewa kupoteza ushahidi hivyo si rahisi matukio kama hayo ya rushwa ukawakamata na fedha, lakini kijeshi zipo njia zingine za kuangalia namna ya ukiukwaji wa utekelezaji wa majukumu yao yanayodhibitisha rushwa kufanyika!

Mfano:
Ukiona daktali kafukuzwa kazi kwa tuhuma za kubaka wagonjwa, siyo lazima ukutwe akiwa kiunoni mwa mgonjwa, au si lazima mgonjwa akutwe na shahawa, kwasababu wataalam wetu hawa wanajua kupoteza ushahid yamkini anaweza kuvaa condom ili kupoteza ushahidi wa shahawa, au akamdunga mgonjwa sindano ya usingizi ili afanye yake!

Hivyo mtu huyo anapofukuzwa kazi anaweza kulalamika kuwa kafukuzwa kazi pasipo ushahidi.

Mwambieni nabii shilla aache kabisa kufanya uchochezi wa namna hii! Kwanza anahatarisha hata maisha ya waumini wake kwa kueleza uchochezi kama huo!

Akumbuke maelekezo na kanuni wanayopewa wakati wa usajili wa huduma/kanisa yanasemaje, kama hajasajiliwa basi akafanye hivyo haraka apate usajili wa huduma wizara ya mambo ya ndani ili azingatie miiko katika mafundisho yake ili asifanye uchochezi wa namna hii tena kwa makamanda.

Kuna kosa la rushwa na makosa ya kutengeneza mazingira ya rushwa n.k hata huko barabarani mnajionea! Lakini jeshi linapobaini huwa linawafukuza makamanda wengi tu kimya kimya! Haiwezekani kila siku mtu yule yule alalamikiwe na watu tofauti halafu mkuu wake ashindwe kuchukua hatua!

Nitawawekea vidio ya unabii wake bado video ina upload!
 
Baba yake atakua amemhakikishia kwamba kwa jinsi hiyo kesi ilivyo ni lazima huyo Polisi afukuzwe.

Kumbuka kuwa baba wa huyo mnayrmuita nabii Shira ni kati ya ma RPC katika moja ya mikoa nchini
 
Baba yake atakua amemhakikishia kwamba kwa jinsi hiyo kesi ilivyo ni lazima huyo Polisi afukuzwe.
Kumbuka kuwa baba wa huyo mnayrmuita nabii Shira ni kati ya ma RPC katika moja ya mikoa nchini
Baba yake kama kashindwa kumkanya basi wasamalia watamkanyia!
 
Umeandika mengi lakini nakataa hatua ya kutaka kumnyamazisha nabii.

Ikiwa amedanganya mshtakini, kama ameongea ukweli basi kijana apate haki yake. Tutumie sheria na si vitisho.

Tupendane wabongo.
 
Umeandika mengi lakini nakataa hatua ya kutaka kumnyamazisha nabii.
Ikiwa amedanganya mshtakini, kama ameongea ukweli basi kijana apate haki yake. Tutumie sheria na si vitisho.

Tupendane wabongo.
Namba za makamanda ziko wazi, yule kijana analijua hilo, hata konstepo wa polisi aliyeajiliwa Leo hashindwi kupiga simu ya malalamiko.

Alichokifanya nabii ni uchochezi kupitia Imani, ile video haiwezi kufutika ikithibitika yule kijana alifukuzwa kihalali!
 
Naamini kama nabii kafanya uchochezi( kesi maarufu zamani zile) hashindikani kushtakiwa. Basi mashtaka yafunguliwe na hakimu aamue.
 
Tupendane wabongo.
Upendo unauwaza kwa kijana huyo, je umewaza wale walionewa kwa ubambikaji wake? Umemuwazia yule aliyetoa rushwa ilikuwaje!
Unafahamu inchi inapoteza pesa nyingi kuendesha kesi za kubambikia watu ambazo chanzo ni hao polisi wa namna ile?

Unafaham wanaosota mahabusu kwa kubambikiwa?

Unajua jeshi la polisi linachafuliwa na polisi wasiokuwa weledi?

Huo upendo unaotamka ni UPI?

Au unataka RAIA wakipigwa virungu bila hatia ndiyo upendo?
 
Tatizo elimu kaka. Mwerevu angejua kuwa kufanya stunt kama hzo ni kujiweka pabaya na dola..na hata mwisho wa siku hyo biashara yake anaiweka rehani..sasa upeo huo wa kuona atapata wap. Elimu na akil hana.zaid ana akil za utapel na ujanja ujanja
 
Adhabu ya kufukuzwa ni moja ya njia ya kuondoa uchafu wa tuhuma kwa polisi!

Polisi ni kazi ya kuaminika!

Ukionekana unatuhumiwa kula sana rushwa au wake za watu dawa yake ni kuondolewa kikosini kwa kufukuzwa ili ukafanye hayo huko uraiani!

Na kama utakamatika laivu utafungwa kijeshi!

Zote ni adhabu, kufungwa au kufukuzwa kwa tuhuma
 
Upendo unauwaza kwa kijana huyo, je umewaza wale walionewa kwa ubambikaji wake? Umemuwazia yule aliyetoa rushwa ilikuwaje!
Unafahamu inchi inapoteza pesa nyingi kuendesha kesi za kubambikia watu ambazo chanzo ni hao polisi wa namna ile?

Unafaham wanaosota mahabusu kwa kubambikiwa?

Unajua jeshi la polisi linachafuliwa na polisi wasiokuwa weledi?

Huo upendo unaotamka ni UPI?

Au unataka RAIA wakipigwa virungu bila hatia ndiyo upendo?
Kwanini msimshtaki huyo nabii ikiwa kweli amefanya uchochezi?

Kuleta mada kama hiyo hapa ni kama kujaribu kutafuta uungwaji mkono kwa hatua mtakayochukua isiyo ya kisheria.

Nawashauri mumpeleke mahakamani huyo nabii na kama dogo ana madai ya msingi apate haki yake.

Mimi huwa sipendi mtu kuonewa ,hivyo nikihisi uonevu najikuta nipo against.
 
Hapa shida ni nini? Ni 'nabii' kuvuka mpaka au polisi aliyefukuzwa? Mpaka ni upi kwa 'nabii'?
 
Huyo sio nabii ni mjanja janja anayetumia dini kuishi janja janja nyingi kweli mwenzie ni frank anajiita nabii frank .....
 
Ila huyo jamaa anavuka mipaka sasa kwa kuanza kujiingiza kwenye mambo ya ndani ndani ya vyombo vya dola

Mwanakulitafuta mwanakulipata
 
Back
Top Bottom