Nachukiwa na bosi wangu bila sababu

Nachukiwa na bosi wangu bila sababu

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
938
Reaction score
1,540
Toka nimeajiriwa miaka mingin iliyopita. , nimegundua boss wangu ananichukia sana, na anaonekana anapenda na kupendelea watu wengi bila sababu, hata wale ambao si watendaji wazuri.

Sio kwamba Mimi ni mchapa kazi, Wala sio kwamba Mimi ni mvivu, ni kawaida tu, bosi wangu amekuwa akieneza uzushi kuhusu Mimi kwenye vikao vyao vya juu, amekuwa akinisigina na kuongea uongo mwingi unaniathiri ninaposikia maneno hayo Kwa watu.

Watu wengi ofisini hawapendi bosi huyo, Kwa maana ni mtu wa kutunga maneno na uzushi mwingi. Chuki zake sizielewi kwasababu sina vigezo au utishiaji wa aina yoyote ya kuchukua cheo chake. Bosi huyu amekuwa akifurahi Kuona Mimi nikiwa na matatizo na kuteseka.

Na Sasa nimeamini huku maofisini Huwa Kuna unafiki mwingi, majungu mengi, bila sababu, mtu unaweza kuwa umekaa unajifanyia zako kazi zako, ila bado mtu akakuchukia na Ili Hali kakuzidi Kila kitu, pesa, cheo, mke Bora.

Nimegundua pia huku ofisini Kuna watu wanapenda kunyeyekea mabosi na kujipendekeza pasipo na sababu, lakini Kuna chuki nyingi na fitina katika maofisi yawe ya umma au binafsi.

Kiuhalisia imefika mahali Sasa, nataka kwenda kumloga huyo basi wangu mana naona chuki zimezidi kupita kiasi.

Na Mimi ni Sala zangu huyo boss abadilike ,lakini ni mtu asiyekubalika hata na baadhi ya watu wanapenda Haki.
 
Hiyo Hali ninl kawaida sio tu serikalini hata kwenye private institutions, muhimu
1. Usipige stori zozote na wafanyakazi wenzio, wewe uwe msikilizaji tu.
2. Usihoji masuala ya pesa kwenye vikao.
3. Mwoneshe kama hujali na huumii kwa mahusiano yenu mbaya. Japo unaumia kwa ndani.
4. Mwendee nyumbani kwake, omba uende kwake. Jioni akiwa ametulia. Mweleze kuwa mahusiano yenu sio mazuri, muyaweke Sawa
5. Usifanye KAZI zake, Fanya zile zilizo kwenye job descriptions zako tu.

Kuna mengi. Ila muda haunitoshi
 
Nahisi tatizo lipo kwako ZAIDI na wewe ndo unaweza kuliondoa kwa haraka.

Hakuna dawa au uchawi unaoweza kukusaidia kufanya WATU wasikuchukie zaidi ya kujifunza njia bora za kuondoa hilo tatizo lako.

Mimi ntakupa njia za uhakika na lazima utafurahia kazi yako.
 
Toka nimeajiriwa miaka mingin iliyopita. , nimegundua boss wangu ananichukia sana, na anaonekana anapenda na kupendelea watu wengi bila sababu, hata wale ambao si watendaji wazuri.

Sio kwamba Mimi ni mchapa kazi, Wala sio kwamba Mimi ni mvivu, ni kawaida tu, bosi wangu amekuwa akieneza uzushi kuhusu Mimi kwenye vikao vyao vya juu, amekuwa akinisigina na kuongea uongo mwingi unaniathiri ninaposikia maneno hayo Kwa watu.

Watu wengi ofisini hawapendi bosi huyo, Kwa maana ni mtu wa kutunga maneno na uzushi mwingi. Chuki zake sizielewi kwasababu sina vigezo au utishiaji wa aina yoyote ya kuchukua cheo chake. Bosi huyu amekuwa akifurahi Kuona Mimi nikiwa na matatizo na kuteseka.

Na Sasa nimeamini huku maofisini Huwa Kuna unafiki mwingi, majungu mengi, bila sababu, mtu unaweza kuwa umekaa unajifanyia zako kazi zako, ila bado mtu akakuchukia na Ili Hali kakuzidi Kila kitu, pesa, cheo, mke Bora.

Nimegundua pia huku ofisini Kuna watu wanapenda kunyeyekea mabosi na kujipendekeza pasipo na sababu, lakini Kuna chuki nyingi na fitina katika maofisi yawe ya umma au binafsi.

Kiuhalisia imefika mahali Sasa, nataka kwenda kumloga huyo basi wangu mana naona chuki zimezidi kupita kiasi.

Na Mimi ni Sala zangu huyo boss abadilike ,lakini ni mtu asiyekubalika hata na baadhi ya watu wanapenda Haki.
Pole mkuu . Ungejua anakuchukia kwa sababu gani pengine ungerekebisha hapo.

Au mtembelee Muulize namna gani unafanya kazi na namna gani unataka msaada zaidi
 
Nazn kama mnasifa ya kielimu saw na boss wako au juu zaid inawez kuw ni sababu pia , don't be smart than your boss
 
Back
Top Bottom