BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 6,373
- 16,073
Mabosi wengine wanaweza kutambua kama unawaigizia.Maboss wanapenda kunyenyekewa, kujipendekeza kwao na uchawa. Fanya hivyo
Baada ya kusoma na kuhitimu chuo na kupata kazi, huwa bado kuna kipengele kingine tena, cha kumchekea chekea Boss.
Mimi nilijaribu ikafeli, kila nikimchekea naona kabisa midomo haitanuki ipasavyo, nakuwa kama roboti, halafu komwe pia linagoma kutoa ushirikiano unakuta unakenua huku komwe limekunja ndita za hasira. HUO NI MPISHANO.
Na ndo vile tena bosi akigundua unamchezea akili anakunyuka MIJELEDI YA KIKAZI, anakufanyia visa na vituko vya kushtukiza.
Lakini mie yule nilimshinda, alitoroka ofisi akakimbia.
Cc Lamomy Extrovert