Nachukua nafasi hii kuiomba Serikali yetu imsamehe Lissu

Ungeiomba Serikali irejee kwenye hekima na misingi ya haki, iondoke kwenye ushetani.

Lisu hana kosa lolote. Yeye anataka tuwe na Taifa la haki ambalo watawala na vyombo vyote wanafuata haki, sheria na katiba. Bahati mbaya, muovu hapendi aambiwe kuwa ni mwovu, hataki aambiwe abadilishe njia zake.

Tumpongeze sana Lisu, na tumshukuru Mungu kwa kutujalia watu kama Lisu, wanaoweza kusimama hadharani na kukemea mambo ya hovyo kabisa yanayoendwa na watawala kwa tamaa ya madaraka. Fikiria tunaongozwa na watu ambao wapo tayari kuwaua watu wasio na hatia ili tu wasihojiwe wanapofanya ushetani wao.

Mungu Mkuu, Mungu wa rehema uendelee kumjalia afya, uzima tele, na moyo usiotetereka, anapotetea haki za wanaodhulumiwa na watawala walioamua kumgeukia shetani, kuwa kinyume nawe Mungu wa haki. Mkono wako wenye nguvu, tunakuomba Nana ukawafikie viongozi hawa wenye kiburi.
 
Lissu apate haki yake. Yeye mwenyewe alisema kuwa hataki huruma. Haki itendeke.
 
KWANI AMEKOSA NINI NA AMEMKOSEA NANI?
 
Mleta mada sijui hata kama unajua Lissu anapigania nini?
Lissu hapiganii Uhuru wake hapo alipo,halafu akiachiwa arudi nyumbani kufanya nini?kulala au?Lissu anapigania mustakabali wa nchi hii,kama ni Uhuru wake Lissu akiamua hata leo anatoka tu

Umesikia alichosema Leo mahakamani?anasema yupo tayari kukaa gerezani muda mrefu akisubiri rufaa atakayopeleka mahakama ya Rufani ili kubatilisha sheria ya kuficha mashahidi kwa sababu hili jambo likiruhusiwa kutumika kwenye kesi hii basi Tunatudi maiaka 400 nyuma katika utoaji haki maana kuna watu watahukumiwa kunyongwa wasijue hata sura za nani kawashtaki,hataki hili litokee
 
Ana kiburi sana, ngoja akae kidogo mpaka January
 
Naunga mkono hoja Kama gaidi alisamehewa licha ya kukutwa na Prima Facie, mhaini pia anaweza kusamehewa. Tumuombee msamaha wa 'Kusameheana Kupo' au akomae nao mpaka?
P
 
Naunga mkono hoja hii.
 
Aombe msamaha kwa kosa lipi
 
Nina kiu ya damu yake.
 
jitazame pamoja anatumia dawa zakila siku kwamajeraha ya wenyekesi Hii pamoja alikufa na kufufuka akili zake ziko Bora kuliko ambazo hata nyasi hazijawahi kuwachoma

kashasema hataki msamaha Wala kuombewa huo msamaha na mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…