Nachukua nafasi hii kuiomba Serikali yetu imsamehe Lissu

Ametenda kosa gani? Lissu anastahili kuombwa radhi na Serikali.
 

Imsamehe kwa kosa gani? Acheni zenu, imwachilie bila masharti yoyote maana jamhuri inatumia sheria kama nyenzo za kukomoa, na sio kutoa haki.
 
Kajengekaje kwa mfano?
Anazidi kuonekana kuwa mtu ambae yuko tayari kuifia nchi yake. Mmejenga nyumba juu ya msingi wa yeye kuepuka kifo. Kila anaposimama mahakamani anazidi kujengeka kama mtu asiye iogopa serikali. Hata asiposema kitu na kuishia kuwasalimia kwa tabasamu waliomo Mahakamani.

Amandla...
 
Watu weusi sijui tumemkosea nini Mungu!
Vichwa kama Lissu si vya kupitia mateso kama haya🚮🚮

Mtu anakuwa kwenye trial ordeal bila proceedings 😔 🙌
 
Imsamehe kwani alikosea Nini? Acha kuwa na akili nyepesi. Uoga wako ndiyo mtaji wa matapeli
 
kama kesi hii inamjenga zaidi, kwanini mnasema anaonewa?
 
Hizi ndizo points ulizomaanisha au zipo zengine?
 
Siyo imsahehe, bali itende HAKI. Lissu anajitaji Justice na si huruma ya mtu yoyote yule
 
kama kesi hii inamjenga zaidi, kwanini mnasema anaonewa?
Wakristu tunaamini kuwa Yesu hakutendewa haki na wayahudi. Lakini kusulubiwa kwake kuliwafanya wengi wamuamini na kumfuata. Mandela, Martin Luther King, Patrice Lumumba n.k. wote walionewa lakini hamna yeyote kati ya wale waliowaonewa anae heshimiwa kama hawa mashujaa. Muhammad Ali alifungwa ili kumkomoa. Matokeo yake yalikuwa kumjenga zaidi.

Amandla...
 
Chadema walimkatalia Zitto alipomuombea msamaha Mbowe. Nyerere alikataa kuomba msamaha aliposhtakiwa kwa uchochezi. Hakutaka hata kulipa faini lakini wenzake wakamlipia. .

Amandla...
 
Undeni kikosi kama M23 kamwe hamtusumbuliwa.
Ni ujinga kusajiri chama mkategemea kuwakomboe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…