DOKEZO Nadai Tsh. Milioni 440 kwa Mkandarasi wa SGR. Naomba Serikali inisaidie, napigwa danadana tangu Desemba 2022

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
kwani mtaji wangu niliowekeza hapo haunisaidii peke yangu, kuna Watanzania wenzangu wengi wanaofaidika kupitia ajira hiyo
Wewe pigania haki yako tu, utaeleweka. Sote tunajua hii aya ni ya kisiasa/uongo. Ukiacha Hayati Magufuli, Watanzania hatuna desturi ya kupambania haki za wengine.
 
Ngoja tuwatag waliyo karibu
Na mfumo FaizaFoxy Lucas mwashambwa
Watasaidia kukufikishia ujumbe

Ova
Unajuwa hapo kuna tatizo, tunalisikiliza upande mmoja tu.

Anasema hajalipwa toka mwaka jana, lakini cha kushangaza anasema bado gari zake zipo kazini.

Anafanyaje hiyo kazi bila malipo muda wote huo?

Mwamba ngoma huvutia kwake.
 
Unajuwa hapo kuna tatizo, gtunalisikiliza upande mmoja tu.

Nahisi akiondoa gari zake kazini yeye ndio atakuwa amevunja mkataba isivyo halali na atakuwa amehalalisha kutolipwa haki yake.

Kuna walimu wa shule private unakuta anafundisha huku anaidai shule pesa nyingi tu. Ukimwambia kwanini usiache kazi, anakwambia nikiacha nitakuwa nimevunja mkataba na hivyo sitalipwa kwa mujibu wa mkataba tulioingia.
 
Nami nimejiuliza swali hilo, kwa nini aendelee kuongeza deni wakati hilo dogo linawashinda? Hapo iko namna, logically its imposibble.
 
Mimi sio mtu wa mitandao sana lakini nimeona malalamiko kadhaa yanayoandikwa na Jamii Forums kuhusu mambo mbalimbali yanafanyiwa kazi hasa kuhusu huku kwenye shughuli zetu tunazozifanya kwenye miradi.

Mimi ni mmoja wa Wakandarasi wadogo ambao tumekuwa tukifanya kazi na Mkandarasi Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Kampuni ya Yapi Merkezi tangu Februari 2022.

Hadi kufikia leo naandika andiko hili, kupitia Kampuni ya Mzamiru Development Ltd namdai Mkandarasi huyo kiasi cha Tsh. Milioni 440 (fedha za Kitanzania), nimekuwa nikidai malipo yangu tangu Januari, Mwaka huu (2023) lakini nazungushwa kulipwa.

Nilianza kufanya nao kazi kuanzia Lot 1 (awamu ya kwanza), nawakodisha magari ya maji yanayotumika kwenye mradi, ikaendelea hivyo pia Lot 2.
View attachment 2778659
Nimeambatanisha na sample ya mkataba wa ukodishaji vifaa.

Huko siku za nyuma nilikuwa nalipwa japo sio katika kiwango ambacho tumekubaliana, mfano unaweza kudai Milioni 100 lakini wakakupa Milioni 10 na kuahidi kuendelea kukulipa baada ya muda.

Utaratibu tuliowekeana ni kuwa kila mwezi tunatakiwa kulipwa kiasi fulani, lakini ilipofika mwezi wa kumi na mbili mwaka jana (2022) ndipo malipo yalipoanza kukwama.

Mpaka sasa naendelea nao kwenye Awamu ya Tatu yaani Lot 3, hakuna malipo na magari yangu niliyowakodisha bado yapo kwenye kazi.

Nimesumbuka sana kufuatilia malipo yangu lakini sioni dalili za kulipwa, hofu yangu ni kuwa inawezekana mambo yakawa magumu zaidi siku za mbele hivyo kunipa hasara kubwa.

Naomba Serikali isaidie watu kama sisi ambao ni Wakandarasi tunaopambana kujiweka kwenye mstari, kwani mtaji wangu niliowekeza hapo haunisaidii peke yangu, kuna Watanzania wenzangu wengi wanaofaidika kupitia ajira hiyo.
Mkandarasi wenu kafilisika na very unfortunately hata akilipwa na Serikali anaenda ku settle madeni yake huko Uturuki nyie anawatelekeza.

Kama hajawalipa Wafanyakazi wake salary Wala nssf ndio aje akulipe wewe?

Mkuu huyo mkandarasi wa mchongo aliletwa na wale Wazalendo na nyie Wazalendo mkaunga Juhudi ,wewe fanya kama.hiyo.kazi ni uzalendo wako kitaifa 🤪🤪🤪🤪

Pole
 
Pole sana mkuu.

Kwanza hawa YAPIMARKEZI wapo katika hali ngumu kiuchumi kutokana na serikali ya MAMA (ANAYE UPIGA MWINGI).

Haki yako ipo palepale kulingana na mkataba wenu ulivyo.

Ila inaweza chukua muda.. kwasababu ya serikali mkuu. Kuwa na subira
Mkiambiwa Dunia nzima Kuna mtikisiko WA DOL muwe mnaelewa,huko Uturuki Hali ni Tete.

Mkandarasi wa mchongo kafilisika akilipwa na Serikali anaenda kulipa Madeni Uturuki badala ya kulipa subcontractors na staff kazi iende.

Kuvunja mkataba mnaanza kesi Mahakamani ambazo haziishi Leo Wala kesho.

Kwa mazingira kama haya ni kuvumilia ,hii nayo ndio hasara ya kukimbilia mamiradi makubwa wakati Nchi ni maskini na Cha kuwafanya hatuna.
 
Unajuwa hapo kuna tatizo, gtunalisikiliza upande mmoja tu.

Anasema hajalipwa toka mwaka jana, lakini cha kushangaza anasema bado gari zake zipo kazini.

Anafanyaje hiyo kazi bila malipo muda wote huo?

Mwamba ngoma huvutia kwake.
Mali Kauli lakini anakuwa kakodishiwa na pia yeye amepewa kazi Kama fundi maana hapo vifaa vya kazi vipo yakiwemo magari yake ,Wafanyakazi wake na materials kutoka Kwa main contractor kazi atafanya ila kulipwa ndio inakuwaga mtoto.

Na Kwa jinsi ambavyo mkandarasi kafilisika bila shaka Serikali Kwa Sasa itakuwa na hofu ya kumpa pesa maana unaweza mlipa pesa au mkopesha akaenda kulipa Madeni Uturuki harafu nyie kazi inakwama.

Kule Mbeya Kuna mturuki mwingine amelipwa advance payments na Serikali lakini mwaka unaisha eti ameagiza mitambo 😁😁 wakati kbla ya kazi lazima uoneshe una mitambo Ili advance payments ikusaidiie kuanza kazi ya awali.
 
Unfortunately nasikia huyo mkandarasi kafilisika I smell hatari ya kutolipwa kabisa.

Nenda mahakamani mahakama ikupe order ya kushika mali za hiyo Kampuni kama fidia. Napo utahangaika kuzitafutia wateja which takes quite some time as well.
 
Mimi sio mtu wa mitandao sana lakini nimeona malalamiko kadhaa yanayoandikwa na Jamii Forums kuhusu mambo mbalimbali yanafanyiwa kazi hasa kuhusu huku kwenye shughuli zetu tunazozifanya kwenye miradi.

Mimi ni mmoja wa Wakandarasi wadogo ambao tumekuwa tukifanya kazi na Mkandarasi Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Kampuni ya Yapi Merkezi tangu Februari 2022.

Hadi kufikia leo naandika andiko hili, kupitia Kampuni ya Mzamiru Development Ltd namdai Mkandarasi huyo kiasi cha Tsh. Milioni 440 (fedha za Kitanzania), nimekuwa nikidai malipo yangu tangu Januari, Mwaka huu (2023) lakini nazungushwa kulipwa.

Nilianza kufanya nao kazi kuanzia Lot 1 (awamu ya kwanza), nawakodisha magari ya maji yanayotumika kwenye mradi, ikaendelea hivyo pia Lot 2.
View attachment 2778659
Nimeambatanisha na sample ya mkataba wa ukodishaji vifaa.

Huko siku za nyuma nilikuwa nalipwa japo sio katika kiwango ambacho tumekubaliana, mfano unaweza kudai Milioni 100 lakini wakakupa Milioni 10 na kuahidi kuendelea kukulipa baada ya muda.

Utaratibu tuliowekeana ni kuwa kila mwezi tunatakiwa kulipwa kiasi fulani, lakini ilipofika mwezi wa kumi na mbili mwaka jana (2022) ndipo malipo yalipoanza kukwama.

Mpaka sasa naendelea nao kwenye Awamu ya Tatu yaani Lot 3, hakuna malipo na magari yangu niliyowakodisha bado yapo kwenye kazi.

Nimesumbuka sana kufuatilia malipo yangu lakini sioni dalili za kulipwa, hofu yangu ni kuwa inawezekana mambo yakawa magumu zaidi siku za mbele hivyo kunipa hasara kubwa.

Naomba Serikali isaidie watu kama sisi ambao ni Wakandarasi tunaopambana kujiweka kwenye mstari, kwani mtaji wangu niliowekeza hapo haunisaidii peke yangu, kuna Watanzania wenzangu wengi wanaofaidika kupitia ajira hiyo.
Mawakili Wasomi wamejaa kibao mtaani. Na hata humu jukwaani wapo wa kutosha tu. Wauzie hiyo kesi ili ulipwe hela yako, na fidia juu.
 
Huyo mkandarasi ana hali ngumu sana kiuchumi , na selikali inaweza kutafuta mkarasi mwingine , jambo lako lipo pagumj wahi mapema mahakama inaweza kuamuru kushikia mali za makandarasi mpaka akulipe
Ndio maana nimekwambia hata Mimi kwamba waungane waende Mahakamani washike Mali zake vinginevyo akisepa kuja kupata Haki ni ishu.

Nadhani Serikali inachotaka kufanya ni watafute mkandarasi wa kumuizia hiyo kazi badala ya Yapi maana keshafilisika.
 
Nahisi akiondoa gari zake kazini yeye ndio atakuwa amevunja mkataba isivyo halali na atakuwa amehalalisha kutolipwa haki yake.

Kuna walimu wa shule private unakuta anafundisha huku anaidai shule pesa nyingi tu. Ukimwambia kwanini usiache kazi, anakwambia nikiacha nitakuwa nimevunja mkataba na hivyo sitalipwa kwa mujibu wa mkataba tulioingia.
Inabidi wapeleke malalamiko yao kwa ngazi za kisheria. Watalipwa tu. Wasisubiri, makampuni kushitakiwa malipo ni kitu cha kawaida, unaweza kuwa na kesi nao mahakamani na huku wanakupa kazi zingine.
 
Mimi sio mtu wa mitandao sana lakini nimeona malalamiko kadhaa yanayoandikwa na Jamii Forums kuhusu mambo mbalimbali yanafanyiwa kazi hasa kuhusu huku kwenye shughuli zetu tunazozifanya kwenye miradi.

Mimi ni mmoja wa Wakandarasi wadogo ambao tumekuwa tukifanya kazi na Mkandarasi Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Kampuni ya Yapi Merkezi tangu Februari 2022.

Hadi kufikia leo naandika andiko hili, kupitia Kampuni ya Mzamiru Development Ltd namdai Mkandarasi huyo kiasi cha Tsh. Milioni 440 (fedha za Kitanzania), nimekuwa nikidai malipo yangu tangu Januari, Mwaka huu (2023) lakini nazungushwa kulipwa.

Nilianza kufanya nao kazi kuanzia Lot 1 (awamu ya kwanza), nawakodisha magari ya maji yanayotumika kwenye mradi, ikaendelea hivyo pia Lot 2.
View attachment 2778659
Nimeambatanisha na sample ya mkataba wa ukodishaji vifaa.

Huko siku za nyuma nilikuwa nalipwa japo sio katika kiwango ambacho tumekubaliana, mfano unaweza kudai Milioni 100 lakini wakakupa Milioni 10 na kuahidi kuendelea kukulipa baada ya muda.

Utaratibu tuliowekeana ni kuwa kila mwezi tunatakiwa kulipwa kiasi fulani, lakini ilipofika mwezi wa kumi na mbili mwaka jana (2022) ndipo malipo yalipoanza kukwama.

Mpaka sasa naendelea nao kwenye Awamu ya Tatu yaani Lot 3, hakuna malipo na magari yangu niliyowakodisha bado yapo kwenye kazi.

Nimesumbuka sana kufuatilia malipo yangu lakini sioni dalili za kulipwa, hofu yangu ni kuwa inawezekana mambo yakawa magumu zaidi siku za mbele hivyo kunipa hasara kubwa.

Naomba Serikali isaidie watu kama sisi ambao ni Wakandarasi tunaopambana kujiweka kwenye mstari, kwani mtaji wangu niliowekeza hapo haunisaidii peke yangu, kuna Watanzania wenzangu wengi wanaofaidika kupitia ajira hiyo.
Pole sana mkuu, sio wewe pekee mwenye muda mrefu haujalipwa na wapo wengine wenye gari kama zako hapo hapo manyoni na itigi hawajalipwa muda mrefu wengine wamesimamisha gari kufanya kazi, japo zipo eneo la mradi, na hili la sasa la kupunguza wafanyakazi kwa njia ya likizo ya miezi mitatu isiyo na malipo bado ni kitendawili kwa wadai wote wa kampuni hiyo.
 
Back
Top Bottom