Nadandia kwa mbele hoja ya Rais kuhusu bima ya afya kuwekeza kwenye viwanda vya madawa

Nadandia kwa mbele hoja ya Rais kuhusu bima ya afya kuwekeza kwenye viwanda vya madawa

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Mh. Raisi J.P. Magufuli nakusalimu na kukupongeza kwa wazo au ushauri wako kwa Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (NHIF) wa kuwekeza makusanyo yao ya michango ya wateja kwenye sekta ya afya hasa kwenye viwanda vya madawa n.k.

Mimi nilikuwa na ombi moja ktk kuboresha wazo lako. Naomba NHIF itangaze kupokea miradi ya watu au taasisi binafsi zinazo taka kuwekeza kwenye viwanda vya madawa kwa lengo la kupata mikopo kama mtaji wa miradi yao.

Ipo wazi kabisa kama tukisema NHIF ndio imiliki hii miradi hakika haitakuwa na ufanisi. Sababu ya kuzidiwa mzigo wa majukumu na pia uzoefu unaonesha taasisi za serikali nyingi hazina ufanisi sana zinapokuwa zinajiendesha kibiashara.

Na hii pia inatokana na mzunguko mrefu wa taratibu za kutekeleza mipango flani. Urasimu(Bureaucracy) ni adui wa biashara , timing is everything, kitu kizuri kikifanyika nje ya muda wake kinakuwa hakifanikishi lengo na huenda kinasababisha hasara kibiashara.

Naomba NHIF ikopeshe miradi binafsi lakini ifuatilie kwa ukaribu na ihakikishe pesa yao haipotei kwa mikopo chefu chefu.

Nahisi mahali pa kuanza kujifunza kuhusu ufanisi wa sekta za uwekezaji za umma uanzie kwenye mradi kama wa kiwanda cha maji cha Suma JKT. Je unafanya vizuri kwa kasi kama ya viwanda binafsi vilivyo anzishwa muda unao fanana au vilivyo fuata baada ya mradi huo wa SUMA?

Kuna wakati kutokana na vita vyetu vya kiuchumi tunaweza kujikuta sisi kama nchi tunawekewa vikwazo flani hasa taasisi za kibiashara zinazo milikiwa na umma. Mfano wa hili ni sakata la HUAWEI na vikwazo vya kibiashara vya USA dhidi ya CHINA.

Sasa tukiwa tunahitaji masoko ya nje au mali ghafi za kemikali za hivi viwanda toka nje tunaweza kukuta vikawekwa kwenye orodha ya taasisi zilizo kwenye vikwazo.

Lakini kama zikiwa chini ya umiliki wa sekta binafsi zinaweza kukwepa vikwazo hivi na bado vikatuokoa kwenye pato letu la taifa kipindi cha hali ngumu ikitokea tatizo kama hilo.

Mwisho nakutakia kazi njema Mh. Raisi J.P. Magufuli.

Wadau wengine wa JF naomba mmchangie hoja zaidi huenda Mh. raisi atasoma hapa yeye mwenyewe au wasaidizi wake.

Watu wa itifaki: Mkimshauri Mheshimiwa juu ya hili nipeni credit huko huko kwa kumuambia imetoka wapi. Wala msije hapa JF kunipa credit na wala msiniambie kama ameona ushauri wangu, wala sihitaji teuzi, it's just a love for my country.

Mimi najua akijua kuna ushauri unapatikana JF basi haitafungwa kwa makosa ya wachache wanao tumia vibaya jukwaa hili.

TANZANIA MBELE DAIMA, TANZANIA KWANZA.
 
Kwa hiyo pesa za wanachama wa NHIF mkiziwekeza kwenye viwanda vya madawa,wanachama ambao pesa zao zinakatwa mtawagawia hisa?
Kwani pale unachangia hisa kwenye PLC au unalipia gharama za huduma?
Unaitwa ni mchango sababu huduma wanayopata wengi ni ya gharama kubwa kuliko pesa walizo lipa au walizo changia.
Wengi wanatumia pesa za wanachama wenzao, na hao wasiotumia pesa zao wanachangia tu kwa wenye shida.

Kadai gawio kwenye bima binafsi au bima za huduma zingine kama bima ya gari au ya moto au ya maisha.

Kuna wakati kwenye mambo nyeti inabidi mtu ujipime ukiona mada ipo nje ya mambo unayo elewa au fani yako unaacha wengine wachangie, wewe unafuatilia mjadala ujifunze kitu.

Hii sio mada ya siasa au ya kupunguzia hasira makali ya maishaTusiharibu mjadala tunasogeza mbele hoja za watu amkini na kuzifanya zisionekane kurasa za mwanzo, walengwa wanaweza kuchoka kusoma wakaishia kwenye hoja kama yako hii.
 
Wewe muulize kwanza alifikiri wakati anashauri manake alishauri NSSF bado gharama zake tunabeba sie wagonga nyundo, NHIF wafanye kile ambacho wanaweledi nacho na nakubaliana kabisa na wazo lako la sekta binafsi ndio zikope sasa tatizo unayemshauri hashauriki na NHIF kukopesha sekta binafsi ndio msala mwingine hawatolipa.

Viwanda vya madawa watu walishaanza kujenga tatizo ni hao watoa ushauri hawakawii kuwakamata, kuwadhulumu na kuwawekea masharti meeeeengi. Soko liamue sio warasimu kwanza hawana record yeyote za accomplishment mpaka sasa wape muda.

Sie huku hatuna haja ya kuogopa katika kusema ukweli
 
sasa tatizo unayemshauri hashauriki na NHIF kukopesha sekta binafsi ndio msala mwingine hawatolipa.
Why are you so pessimist?
Why are you getting ahead of yourself?
How do you know he will not take our advice?

What i have provided in my argument is just a mere opinion.
Being an opinion as it is, I could be right or wrong depends on the facts obtained after thoroughly analysis of the subject in hand.

Yeye ana washauri na wataalamu wengi waliobobea kwenye uchumi na biashara na sheria pia. Kwa hivyo anazo nyenzo nzuri za kumfanya afanye mahamuzi sahihi baada ya tafiti. Wakati wewe na mimi tunaweza kufanya uhamuzi kwa hisia binafsi yeye anaweza kufanya kutokana na matokeo ya tafiti za wataalamu.
 
Titicomb,

Ni yeye mwenyewe ndio alisema ashahuriki, yeye ni Jiwe na dereva wa Lori. Mie nimekupa fact. Tafiti za wataalamu wapi huyu bwana amekuwa kiongozi kwa muda mrefu na ni predictable katika matendo yake, hasa yale mazuri yenye kuboresha maisha ya watu na sekta binafsi ana allergy nayo ungeshauri kujenga daraja usingetumia msuli, as long as umetupa fursa tuchangie utuwie radhi wengine tunafikiri tofauti.
 
Napingana nawe kuwa kuwakopesha sekta binafsi kutaua mfuko kwani hiyo pesa haitarudi huko NHIF; mfano mzuri ni Tanzania Pharmaceutical Industry ya Madabida walivuta hela za mifuko ya hifadhi ya jamii na hakuna ufanisi wala malipo ya huo mkopo
 
Napingana nawe kuwa kuwakopesha sekta binafsi kutaua mfuko kwani hiyo pesa haitarudi huko NHIF; mfano mzuri ni Tanzania Pharmaceutical Industry ya Madabida walivuta hela za mifuko ya hifadhi ya jamii na hakuna ufanisi wala malipo ya huo mkopo
Hayo yalitokea enzi hizo taarifa za kumuwezesha mtu kukopa hazikuwa sahihi na rushwa iliwawezesha wakopaji kama hao kufanikisha kupata mikopo wasiyo stahili.

Sasa hivi vyombo vya dola vinasimamia vizuri kwenye udanganyifu kama huu usitokee, nani anapenda kesi ya uhujumu uchumi isiyo kuwa na dhamana?
 
Private Sectors areProfit Oriented....

Kwenye issue sensitive profit is secondary, core issue ni peoples welfare...

Nyie sector binafsi kwanini mgonjee kupata mikopo ? kwanini msianzishe viwanda muweke dawa sokoni na huduma nyingine sokoni hence mu-compete na hao state ?, Madawa mpaka yaingie sokoni research inacost billions of money, production not so much .....
 
Titicomb, Anachosema sio michango ya bima. Anachohoji ni uwekezaji unaotaka kufanywa na NHIF (kwa maagizo ya rais) kwenye viwanda. Ukianzisha kiwanda maana yake unafanya biashara kwa kutumia michango ya wana-NHIF. Huko kuna siku utasikia serikali inapata dividend wakati wanachama wachangiaji hawapati chochote. Nadhani hapo kuna hoja ya msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo yalitokea enzi hizo taarifa za kumuwezesha mtu kukopa hazikuwa sahihi na rushwa iliwawezesha wakopaji kama hao kufanikisha kupata mikopo wasiyo stahili.

Sasa hivi vyombo vya dola vinasimamia vizuri kwenye udanganyifu kama huu usitokee, nani anapenda kesi ya uhujumu uchumi isiyo kuwa na dhamana?
Titicomb unataka kutuaminisha kuwa NHIF ina pesa nyingi za kuwekeza kuliko kutibu wanachama wake? Kuna madawa na vipimo havilipiwi na mfuko hapo hapo wana pesa ya kuwekeza? Ufahamu wangu ni kuwa wewe Titicomb michango yako usipougua itatumika kunitibu mimi Ndachuwa
 
Titicomb unataka kutuaminisha kuwa NHIF ina pesa nyingi za kuwekeza kuliko kutibu wanachama wake? Kuna madawa na vipimo havilipiwi na mfuko hapo hapo wana pesa ya kuwekeza? Ufahamu wangu ni kuwa wewe Titicomb michango yako usipougua itatumika kunitibu mimi Ndachuwa
Labda wewe na mimi hatuuji na mkuu anajua akaunti za NHIF zinasomaje kwenye vitabu vya hesabu za mapato na matumizi.
Ndio maana kaongea vile.
Let's assume he know what he is talking.
 
Anachosema sio michango ya bima. Anachohoji ni uwekezaji unaotaka kufanywa na NHIF (kwa maagizo ya rais) kwenye viwanda. Ukianzisha kiwanda maana yake unafanya biashara kwa kutumia michango ya wana-NHIF. Huko kuna siku utasikia serikali inapata dividend wakati wanachama wachangiaji hawapati chochote. Nadhani hapo kuna hoja ya msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unapojengewa barabara au hospital ndio unakula gawio hivyo!
Mbona watanzania tuko hivi jamani?

Mbona haudai gawio la NMB?
 
Back
Top Bottom