Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unafikiri viwanda vingi vya dawa hapa Afrika vinafanya tafiti za kutengeneza dawa mpya?Madawa mpaka yaingie sokoni research inacost billions of money, production not so much .....
Wamezoea na mazoea hujenga tabia.Tumeyaona yaliyotokea kwa NSSF,PPF,LAPF na Kidogo GEPF ya wakubwa.Hii mifuko inafahamika ni ya wanachama kisheria lakini maamuzi na faida za uwekezaji ni Government na kuinusuru kufilisika wakaiunganisha.Mapato na raslimali kama faraja LA Kigamboni,majengo na kiwanda cha sukari yamekuwa ya wanachama?Kwa hiyo pesa za wanachama wa NHIF mkiziwekeza kwenye viwanda vya madawa,wanachama ambao pesa zao zinakatwa mtawagawia hisa?
Embu fungukeni kidogo kimtazamo..Wamezoea na mazoea hujenga tabia.Tumeyaona yaliyotokea kwa NSSF,PPF,LAPF na Kidogo GEPF ya wakubwa.Hii mifuko inafahamika ni ya wanachama kisheria lakini maamuzi na faida za uwekezaji ni Government na kuinusuru kufilisika wakaiunganisha.Mapato na raslimali kama faraja LA Kigamboni,majengo na kiwanda cha sukari yamekuwa ya wanachama?
Hio ilikuwa second point kwamba production sio gharama kama research, point ya kwanza ni kwamba, kwanini hizo private sectors zisianshishe hivyo viwanda wakati soko lipo kuliko kusubiri pesa za wachangiaji ndio uwe mtaji wa wao kuingia sokoni ili waendelee kuwauzia hao hao wachangiaji..., si waingie sokoni kuanzia sasa...Unafikiri viwanda vingi vya dawa hapa Afrika vinafanya tafiti za kutengeneza dawa mpya?
Nyingi zinanua hakimiliki ya kutengeneza dawa iliyo maarufu tayari sokoni.
Coca Cola tanzania hawapo kwenye kubuni soda mpya bali kuzalisha under license products za nje.
Nadhani hata ukifuatilia hivi viwanda vitengo vyao vya tafiti vinafanya tafiti nyingi kama sio zote za masoko tu.
Kwani ukisikia "Government empowerment programs" unajua ndio nini mfano wake?Hio ilikuwa second point kwamba production sio gharama kama research, point ya kwanza ni kwamba, kwanini hizo private sectors zisianshishe hivyo viwanda wakati soko lipo kuliko kusubiri pesa za wachangiaji ndio uwe mtaji wa wao kuingia sokoni ili waendelee kuwauzia hao hao wachangiaji..., si waingie sokoni kuanzia sasa...
Wasio kuwa wanachama wa NHIF nao wamewekeza wapi?Hivi unafahamu kuwa wachangiaji wa Bima hawaugui wote,na wanaougua pia wana limitations za huduma wanazostahili kupata?Vile vile ni walipa kodi ya PAYE na VAT through purchase of goods & services?Tuache kushabikia kila wasemacho wanasiasa.Embu fungukeni kidogo kimtazamo..
Hizo taasisi ulizotaja ukiwekeza pesa yako kuna huduma unapewa kupitia pesa yako kwa maana hiyo tayari unafaidika na pesa yako.
Lakini ukinunua hisa kwenye PLC kama mabenki au taasisi nyingine za kibiashara hakuna faida unapata zaidi ya kusubiria gawio lako la faida kutokana na hisa zako.
Kwa hivyo ukitaka faida ya uwekezaji wa michango yako kwenye hii mifuko uliyotaja utakuwa unataka kupata faida mara mbili zaidi.
Jambo jingine la msingi mnasahau kuna huduma za kijamii mnapata bila kujali umechangaia nini.
Mfano, huduma za miundo mbinu, elimu, ulinzi, n.k.
Huku ndio gawio lenu linaenda kutumika.
Kwani wewe unajua umma ndio akina nani kama sio wewe na mimi?
Kwa hivyo viwanda vitamilikiwa na wewe na mimi isipokuwa hatutapewa pesa taslimu (cash) kama faida ya uwekezaji wetu. Tutapewa huduma za kijamii mbadala wake.
Kwani ukiwekeza pesa yako kwenye biashara kwa mfumo wa hisa hiyo biashara hailipi kodi?Wasio kuwa wanachama wa NHIF nao wamewekeza wapi?Hivi unafahamu kuwa wachangiaji wa Bima hawaugui wote,na wanaougua pia wana limitations za huduma wanazostahili kupata?Vile vile ni walipa kodi ya PAYE na VAT through purchase of goods & services?Tuache kushabikia kila wasemacho wanasiasa.
Mifuko ya Pension inakusanya fedha kutoka kwa watumishi,hizo fedha zao zikiwekezwa walitakiwa wapewe faida kupitia uwekezaji husika.
siafiki NHIF kujitosa kwenye viwanda hela itazama na madawa mengi ni trade mark za nje gharama za kulipia royalities na kadhalika ni kubwa mno tena kwa pesa za kigeni.Hayo yalitokea enzi hizo taarifa za kumuwezesha mtu kukopa hazikuwa sahihi na rushwa iliwawezesha wakopaji kama hao kufanikisha kupata mikopo wasiyo stahili.
Sasa hivi vyombo vya dola vinasimamia vizuri kwenye udanganyifu kama huu usitokee, nani anapenda kesi ya uhujumu uchumi isiyo kuwa na dhamana?
Kama soko au mahitaji ya madawa ni kubwa sana kuliko viwanda vilivyopo na serikali imeona pesa nyingi sana ipo kwenye akaunti ya NHIF kwanini isiwekezwe kiasi na kikabakizwa kiasi ambacho mzunguko wa shughuli za mfuko hazitakwama?siafiki NHIF kujitosa kwenye viwanda hela itazama na madawa mengi ni trade mark za nje gharama za kulipia royalities na kadhalika ni kubwa mno tena kwa pesa za kigeni.
serikali ikilitaka hlilo ianzishe kampuni separate iipe mtaji usitoke NHIF .lakini serikali ilishakuwa nayo na ilikufa.
mfuko ubaki kama mfuko usiguswe
sekta binafsi viwanda vya madawa vipo mfano mansoor daya nk wao hukopa kwenye mabenki ,yeyote wa sekta binafsi anayetaka kuanzisha kiwanda chochote kiwe cha madawa au la aende benki za biashara akakope huko pesa ya NHIF ibaki ilivyo
hao wana ubia na makampuni ya madawa ya kimataifa na wana sole manufacturing license kwenye madawa mengi tu .Wewe ukiingia wamiliki license watakwambia Kwa Tanzania tunaye mansoor daya au shellys hatutoi leseni kwa mwingine hawakupi leseni ya kuzalisha hao wabia wao.Kwanini tunawaza lazima hakutakuwa na faida kwa shirika binafsi likiendesha biashara hiyo?
Kwanini unafikiri lazima pesa yote ya mradi itatoka NHIF?
Hapa yakaribishwe hadi mashirika ya nje lakini kwa ubia na wenyeji.
Kama gharama za kulipia royalties kwa wenye haki miliki ya madawa flani zingekuwa kubwa hivyo kiasi cha kuhesabu hasara tu basi akina Mansoor Day na Shelys wasingekuwepo sokoni.
Nashukuru kwa mchango wako mzuri sana.hao wana ubia na makampuni ya madawa ya kimataifa na wana sole manufacturing license kwenye madawa mengi tu .Wewe ukiingia wamikiki license watakwambia Kwa Tanzania tunaye mansoor daya au shellys hatutoi leseni kwa mwingine
yupo ma hawakupu leseni ya kuzalisha hao wabia wao.
sio rahisi kama unavyofikiri.Mfano mdogo ukitaka ku import dawa Tanzania uwe distributor hupati ma sole distributor wengi wa dawa Africa mashariki wapo kenya.Wenye kiwanda watakwambia kanunue kupitia kwa agents wao kenya
Ndio maana watanzania wengi ni wauza maduka tu ya reja reja ya madawa hata ukikuta anauza jumla ni ki stock kidogo tu
ndio maana napinga sekta binafsi kukopeshwa hela za NHIF wakakope benkii zikizama wajuane na benki sio zizame pesa za wanachama
Sawa mkuu, inabidi tu niheshimu mawazo yako.Ni yeye mwenyewe ndio alisema ashahuriki, yeye ni Jiwe na dereva wa Lori. Mie nimekupa fact. Tafiti za wataalamu wapi huyu bwana amekuwa kiongozi kwa muda mrefu na ni predictable katika matendo yake, hasa yale mazuri yenye kuboresha maisha ya watu na sekta binafsi ana allergy nayo ungeshauri kujenga daraja usingetumia msuli, as long as umetupa fursa tuchangie utuwie radhi wengine tunafikiri tofauti.
halifai watu binafsi wanaoweza wakope banki watengeneze hizo drip wauzie mahospitali bima ya afya ilipie wagonjwa tukuenda kienyeji hivi itafika Imahali hata hospitali zitatakiwa ziwe na viwanda vya drip au gloves!!!! kisa wanapata hela za wagonjwa .Huduma zitadorora hosputalini.Hospitali zibaki kama hospitali,bima za afya zibaki kama bima za afya ,na viwanda vya dawa vibaki kama viwanda vya dawa vinavypjitegemea visivyo chini ya bima ya afya wala visivyotumia pesa za bima ya afya kama mtaji wakeNashukuru kwa mchango wako mzuri sana.
Kwa hivyo hitimisho wazo la pesa ya NHIF kuwekeza kwenye viwanda vya madawa halifai kabisa hata zile drip za maji(IV sijui)?
Sijui nikuchangie kifupi au kirefu mada yako hii nzuri mkuu Titicomb.Mimi nilikuwa na ombi moja ktk kuboresha wazo lako. Naomba NHIF itangaze kupokea miradi ya watu au taasisi binafsi zinazo taka kuwekeza kwenye viwanda vya madawa kwa lengo la kupata mikopo kama mtaji wa miradi yao.