Nadandia kwa mbele hoja ya Rais kuhusu bima ya afya kuwekeza kwenye viwanda vya madawa

Nadandia kwa mbele hoja ya Rais kuhusu bima ya afya kuwekeza kwenye viwanda vya madawa

Kwani ukiwekeza pesa yako kwenye biashara kwa mfumo wa hisa hiyo biashara hailipi kodi?
Au ukiwekeza bank na ukifungua account bank hiyo hiyo haulipi kodi za miamala na nyinginezo?

Kwanini haudai double dividend?

Hivi haufahamu sio kila anaelipia bima ya gari lazima gari inapata ajali na kuitumia pesa yake aliyo lipia bima?
Kwanini haudai watu wa bima ya gari wakupatie gawio la faida kama fedha mnayolipia wateja wanawekeza ktk biashara nyingine kama kukopesha fedha na kupata faida?

Ikiwa kila anaelipia bima lazima akutwe na shida inayolipiwa na bima hadi pesa zake ziishe basi hiyo haitakuwa bima.
Na shirika husika la bima litafilisika, kwanza hilo shirika halitastahili kupewa leseni ya kufanya shughuli za bima sababu itakuwa limefanya vibaya hesabau zake.

Bima lazima kuwe na kuchangiana kwa namna moja au nyingine, na pia lazima mmfuko/shirika lazima liwekeze pesa inayo kusanya ili kuweza kupata fedha ya kulipia fedha za ziada walizo lipiwa/lipwa wateja. Vinginevyo basi ungelipiwa mwisho sawa na kiasi ulicho changia tu.
Kuhusu Bima ninafahamu biashara zao zilivyo,ila hapa tunaongelea bima ya afya kuwekeza kwenye kiwanda/viwanda vya dawa,Big No.Tanzania tayari tuna viwanda vya dawa na msd hawanunui huko,je hiki kiwanda kitamuuzia nani?
Napingana na ushauri wa NHIF kujiingiza katika biashara hiyo kwa sababu hats viwanda vilivyopo nchini havifanyi vizuri na vingine ni vya umma.Tusibadili NHIF na kufanya ifanye nje ya lengo LA kuanzishwa kwake.
 
siafiki NHIF kujitosa kwenye viwanda hela itazama na madawa mengi ni trade mark za nje gharama za kulipia royalities na kadhalika ni kubwa mno tena kwa pesa za kigeni.

serikali ikilitaka hlilo ianzishe kampuni separate iipe mtaji usitoke NHIF .lakini serikali ilishakuwa nayo na ilikufa.

mfuko ubaki kama mfuko usiguswe

sekta binafsi viwanda vya madawa vipo mfano mansoor daya nk wao hukopa kwenye mabenki ,yeyote wa sekta binafsi anayetaka kuanzisha kiwanda chochote kiwe cha madawa au la aende benki za biashara akakope huko pesa ya NHIF ibaki ilivyo
Umenena vema,tusiivuruge NHIF kama tulivyofanya kwa mifuko ya hifadhi ya jamii.
 
Unafikiri viwanda vingi vya dawa hapa Afrika vinafanya tafiti za kutengeneza dawa mpya?
Nyingi zinanua hakimiliki ya kutengeneza dawa iliyo maarufu tayari sokoni.

Coca Cola tanzania hawapo kwenye kubuni soda mpya bali kuzalisha under license products za nje.
Nadhani hata ukifuatilia hivi viwanda vitengo vyao vya tafiti vinafanya tafiti nyingi kama sio zote za masoko tu.

Tena hii viwanda hakuna haja sana ya kuingiza pesa nyingi kwenye tafiti za dawa mpya wakati kuna taasisi kama NIMR.
Wanaenda kuomba vibali vya kutumia matokeo ya tafiti za hizi taasi tu.

Huko NIMR kuna pesa za wahisani kibao zinawekwa, na hata NHIF ikianzisha kiwanda itakuwa sio faida kiuchumi kama wataenda kupoteza pesa kwenye tafiti ambazo NIMR wanafanya tayari.
Usipende kuchukulia Mambo kirahisi rahisi hivyo
 
Usipende kuchukulia Mambo kirahisi rahisi hivyo
Sawa mkuu.
Ningefurahi zaidi kama elezea zaidi wapi nimeongea ndivyo sivyo nijifunze kitu.
Mimi sijui chchite ndio maana nimekaribisha hoja zenu wadau wengine.

Au kuhusu kuuona huu ushauri Mh. Raisi?
Hii inaistwa unarushia kunde ukutani nyingi iwezekanavyo huenda moja inaweza kunasa ukutani.
 
Kuhusu Bima ninafahamu biashara zao zilivyo,ila hapa tunaongelea bima ya afya kuwekeza kwenye kiwanda/viwanda vya dawa,Big No.Tanzania tayari tuna viwanda vya dawa na msd hawanunui huko,je hiki kiwanda kitamuuzia nani?
Napingana na ushauri wa NHIF kujiingiza katika biashara hiyo kwa sababu hats viwanda vilivyopo nchini havifanyi vizuri na vingine ni vya umma.Tusibadili NHIF na kufanya ifanye nje ya lengo LA kuanzishwa kwake.
Sawa mkuu.
Mawazo yako lazima yaheshimiwe, hakuna mawazo yasiyo na maana.
 
Sasa niambie, hii ni "Kifupi au Kirefu"? Mimi naona ni kifupi!
Hahaa hii ni katikati.
Maana mambo kadhaa umajadili ukaachia katikati, lakini nayaona muhimu sana.
Yanaweza kutunza kitu.

Mfano hapo chini
Historia ya Tanzania kuwa nauwezo wa kutengeneza madawa yake kwa matumizi yake na biashara ilipamba moto sana kwenye miaka ya 60; hapo ndipo serikali ikishirikiana na UNIDO (United Nations Industrial Development Organization) ilipoombwa kutengeneza ramani ya namna kazi hiyo itakavyotekelezwa.

Bila shaka Wizarani (Afya) mafaili hayo bado yapo.

Huo ndio uliokuwa mwanzo wa mafunzo ya wataalam katika utengenezaji wa madawa. Chuo cha mafamasia Muhimbili kikianzishwa maksudi 1975 (?) nadhani kwa lengo hilo.

Chuo hicho madhumuni yake hayakuwa kupata wauza maduka ya dawa. Lengo mhimu lilikuwa ni kupata watengeneza dawa.

Na ni wakati huo huo, viwanda kama Keko, na Arusha vilijengwa na kuanza kufanya kazi

Hiyo ni historia bila kugusa ni vipi tulishindwa kwenda mbele tokea hapo. Sababu zipo.
Sababu zilizo changia kushindwa kwa huu mradi ni zipi?
Nahisi zilikuwa urasimu na mambo ya bajeti.
Ikilazimu anzisha mada inayo jitegemea (thread) itakayo elezea vizuri wapi tulikwama. Uninukuu (quote) tu nami nije nijifunze.
Ni swala la nidhamu tu, hata nidhamu ya shurti ikilazimu, why not?
Mkuu unataka watu waende nje kulia kwamba sasa bwana mkubwa ameshakuwa dikteta kamili?
Hatuchelewi kusahau tulikuwa tunataka nini mambo yanapo pamba moto.
Kabla ya 2015 yalisikika sana maoni ya kutaka raisi mkali ikibidi mwenye udikteta kidogo, hata Mh. Kikwete aligusia hili aliposema "si mlikuwa manataka raisi mkali ? sasa nimewaletea huyu ni tinganga kweli".
Watu wamekwishaingia sasa kwenye viwanda tofauti kabisa na tunavyovizungumzia hapa. Watu wpo sasa kwenye "individualized treatment" - Biotechnology na Genetic engineering.
Nafikiri hii ingekuwa hatua ya pili (Phase II) au ya tatu ya mradi.
Tuanze na mambo rahisi kutekelezeka kisha tunaenda hatua moja mbele zaidi baada ya kufanikiwa hatua tulizo anza nazo.
 
Hilo la kusema "serikali ikiwekewa vikwazo", umelivuruga. Tanzania ikiwekewa vikwazo ni pamoja na sekta binafsi iliyomo ndani yake.
Hapana mkuu.
Inategemea na hatua ya vikwazo, kuna wakati inawekewa serikali na wabia au washirika wake toka sekta binafsi.
Kwa mfano Huawei alikuwa kwenye vikwazo lakini Tecno hakuweko.

Najua iuna wakati nchi au taifa zima linawekewa vikwazo taasisi zote za umma na binafsi au watu mmoja mmoja binafsi.
Kuna wakati ni baadhi tu ambazo zinafanya biashara moja kwa moja na serikali.

Sasa kwa kesi yetu NHIF inakopesha taasisi binafsi na hakuna mambo ya ubia wala ushirikiano wa aina yeyote ktk umiliki au ugawanaji faida za kiuchumi na hao watakao kopa.

Mtu akisha lipa deni lote na uhusiano unaishia hapo, isipokuwa wawekewe mashariti ya kutobadili biashara ili yasitokee kama ya awamu ya tatu viwanda vya nguo vinageuka warehouse (ghala) za biashara za samani au vioo kama pale Urafiki na kwingineko, Hapa malengo ya serikali sekta ya afya hayatafanikiwa.

Mwisho haya ni mawazo tu mimi na wewe hatupo ktk nafasi ya washauri wa Mh.Raisi.

Nimefurahi sana umeonesha mahali pa kuanzia pale chuo cha ufamasia MNH na blueprints zote za mradi wa viwanda vya dawa na UNIDO lazima zitakuwa kwenye makabati wizarani.
 
Labda wewe na mimi hatuuji na mkuu anajua akaunti za NHIF zinasomaje kwenye vitabu vya hesabu za mapato na matumizi.
Ndio maana kaongea vile.
Let's assume he know what he is talking.

Umetoa ushauri kwa jambo usilolijua. Huyo jamaa ni muongo wa kutupa.
 
Huyo jamaa ni muongo wa kutupa.
This is so negative.
Kwani waongo hawafanyi miradi au vitu flani vikafanikiwa?
Kwanza uongo ni ralative, unachoona wewe uongo kinaweza kuwa sio uongo kwa mwingine kutegemeana na kiwango cha taarifa za jambo husika ulizonazo muda huo.
 
Mh. Raisi J.P. Magufuli nakusalimu na kukupongeza kwa wazo au ushauri wako kwa Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (NHIF) wa kuwekeza makusanyo yao ya michango ya wateja kwenye sekta ya afya hasa kwenye viwanda vya madawa n.k.

Mimi nilikuwa na ombi moja ktk kuboresha wazo lako. Naomba NHIF itangaze kupokea miradi ya watu au taasisi binafsi zinazo taka kuwekeza kwenye viwanda vya madawa kwa lengo la kupata mikopo kama mtaji wa miradi yao.

Ipo wazi kabisa kama tukisema NHIF ndio imiliki hii miradi hakika haitakuwa na ufanisi. Sababu ya kuzidiwa mzigo wa majukumu na pia uzoefu unaonesha taasisi za serikali nyingi hazina ufanisi sana zinapokuwa zinajiendesha kibiashara.

Na hii pia inatokana na mzunguko mrefu wa taratibu za kutekeleza mipango flani. Urasimu(Bureaucracy) ni adui wa biashara , timing is everything, kitu kizuri kikifanyika nje ya muda wake kinakuwa hakifanikishi lengo na huenda kinasababisha hasara kibiashara.

Naomba NHIF ikopeshe miradi binafsi lakini ifuatilie kwa ukaribu na ihakikishe pesa yao haipotei kwa mikopo chefu chefu.

Nahisi mahali pa kuanza kujifunza kuhusu ufanisi wa sekta za uwekezaji za umma uanzie kwenye mradi kama wa kiwanda cha maji cha Suma JKT. Je unafanya vizuri kwa kasi kama ya viwanda binafsi vilivyo anzishwa muda unao fanana au vilivyo fuata baada ya mradi huo wa SUMA?

Kuna wakati kutokana na vita vyetu vya kiuchumi tunaweza kujikuta sisi kama nchi tunawekewa vikwazo flani hasa taasisi za kibiashara zinazo milikiwa na umma. Mfano wa hili ni sakata la HUAWEI na vikwazo vya kibiashara vya USA dhidi ya CHINA.

Sasa tukiwa tunahitaji masoko ya nje au mali ghafi za kemikali za hivi viwanda toka nje tunaweza kukuta vikawekwa kwenye orodha ya taasisi zilizo kwenye vikwazo.

Lakini kama zikiwa chini ya umiliki wa sekta binafsi zinaweza kukwepa vikwazo hivi na bado vikatuokoa kwenye pato letu la taifa kipindi cha hali ngumu ikitokea tatizo kama hilo.

Mwisho nakutakia kazi njema Mh. Raisi J.P. Magufuli.

Wadau wengine wa JF naomba mmchangie hoja zaidi huenda Mh. raisi atasoma hapa yeye mwenyewe au wasaidizi wake.

Watu wa itifaki: Mkimshauri Mheshimiwa juu ya hili nipeni credit huko huko kwa kumuambia imetoka wapi. Wala msije hapa JF kunipa credit na wala msiniambie kama ameona ushauri wangu, wala sihitaji teuzi, it's just a love for my country.

Mimi najua akijua kuna ushauri unapatikana JF basi haitafungwa kwa makosa ya wachache wanao tumia vibaya jukwaa hili.

TANZANIA MBELE DAIMA, TANZANIA KWANZA.
Tunarudi katika miaka ya ujamaa.Tunaweza anzisha viwanda kwa mifuko ya umma lakini nani ajuaye rais atayekuja baada ya Magufuli atakuaje? Je akiwa mpenda rushwa? Na je akiwa mzembe na viwanda vikafa? Au tunajuaje serikali ijayo itaamua nini? Isije ikawa tunajenga halafu raisi ajaye akaamua kuvidhoofisha halafu akawauzia marafiki hivo viwanda kwa being chee! Mnakumbuka viwanda vya nyerere vimeishia wapi? Ni akina nani wamepewa buree na wametajirika na viwanda vilivyojengwa na nyerere?

Ushauri...
NHIF waingie ubia na sekta binafsi katika kuwekeza katika viwanda.Wasimiliki viwanda kwa asilimia zote.Wala wasimkopeshe MTU kujenga viwanda.Waende kutafuta watu wenye viwanda popote pale duniani,halafu waingie nao ubia katika kuwekeza kwenye viwanda vya madawa TZ.Hilo litaepusha kuuzwa au kugawiwa bure viwanda vya umma kwa utawala wowote ule ujao.Nafikiri serikali isimiliki viwanda kwa asilimia Mia kwa sector yoyote ile.
 
Kwani pale unachangia hisa kwenye PLC au unalipia gharama za huduma?
Unaitwa ni mchango sababu huduma wanayopata wengi ni ya gharama kubwa kuliko pesa walizo lipa au walizo changia.
Wengi wanatumia pesa za wanachama wenzao, na hao wasiotumia pesa zao wanachangia tu kwa wenye shida.

Kadai gawio kwenye bima binafsi au bima za huduma zingine kama bima ya gari au ya moto au ya maisha.

Kuna wakati kwenye mambo nyeti inabidi mtu ujipime ukiona mada ipo nje ya mambo unayo elewa au fani yako unaacha wengine wachangie, wewe unafuatilia mjadala ujifunze kitu.

Hii sio mada ya siasa au ya kupunguzia hasira makali ya maishaTusiharibu mjadala tunasogeza mbele hoja za watu amkini na kuzifanya zisionekane kurasa za mwanzo, walengwa wanaweza kuchoka kusoma wakaishia kwenye hoja kama yako hii.

umeelezea sjui kwa hisia! ila nice explanations
 
BOOS ahsante kwa maoni yako mazuri.
Nina ombi moja kwako na kwa wachangiaji wengine tusinukuu (quote) maelezo yote ya madaa kuu.
Wewe tiririka tu hapo chini, unaweza kunukuu vipande vipande au una nukuu post za michango ya chini sio mada kuu.
 
This is so negative.
Kwani waongo hawafanyi miradi au vitu flani vikafanikiwa?
Kwanza uongo ni ralative, unachoona wewe uongo kinaweza kuwa sio uongo kwa mwingine kutegemeana na kiwango cha taarifa za jambo husika ulizonazo muda huo.

Ni muongo fullstop.
 
Kwa hiyo pesa za wanachama wa NHIF mkiziwekeza kwenye viwanda vya madawa,wanachama ambao pesa zao zinakatwa mtawagawia hisa?
Mkuu hivi fedha zinazoenda NHIF ,huwa zigawiwa Tena kwa wachama au zinatumika kwenye matibabu nafikili hoja yako Ni dhaifu sana Wala Haina mantiki yeyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri hii ingekuwa hatua ya pili (Phase II) au ya tatu ya mradi.
Tuanze na mambo rahisi kutekelezeka kisha tunaenda hatua moja mbele zaidi baada ya kufanikiwa hatua tulizo anza nazo.
Ngoja niku-'quote' kwenye kipande hiki pekee kwa sasa. Sikubaliani kabisa na mawazo haya.
 
Akili dogo pita hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huyo Stuxnet asikusumbue kichwa, mimi sioni mapumba pumba yake na matusi.
Nishambonyezea kitufe cha IGNORE zamani sana baada ya kuona anaumia sana na comment zangu utafikiri tunagombea mke.
Namshauri tu na yeye aniweke kwenye IGNORE list yake hataona post zangu, hatapungukiwa na kitu bali atajipunguzia aibu ya kuonekana hana busara, maana yaonekana hekima kwake ni msamiati mpya.
 
Akili dogo pita hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
Inabidi niweke ushahidi ili huyu Stuxnet asijisumbue kunujibu kitu sitaona.
Stuxnet-MentalCase.JPG
 
Back
Top Bottom