Mimi nilikuwa na ombi moja ktk kuboresha wazo lako. Naomba NHIF itangaze kupokea miradi ya watu au taasisi binafsi zinazo taka kuwekeza kwenye viwanda vya madawa kwa lengo la kupata mikopo kama mtaji wa miradi yao.
Sijui nikuchangie
kifupi au kirefu mada yako hii nzuri mkuu Titicomb.
Ngoja nijaribu, nitakapoishia ndio hapo, iwe kirefu au kifupi.
Historia ya Tanzania kuwa nauwezo wa kutengeneza madawa yake kwa matumizi yake na biashara ilipamba moto sana kwenye miaka ya 60; hapo ndipo serikali ikishirikiana na UNIDO (United Nations Industrial Development Organization) ilipoombwa kutengeneza ramani ya namna kazi hiyo itakavyotekelezwa.
Bila shaka Wizarani (Afya) mafaili hayo bado yapo.
Huo ndio uliokuwa mwanzo wa mafunzo ya wataalam katika utengenezaji wa madawa. Chuo cha mafamasia Muhimbili kikianzishwa maksudi 1975 (?) nadhani kwa lengo hilo.
Chuo hicho madhumuni yake hayakuwa kupata wauza maduka ya dawa. Lengo mhimu lilikuwa ni kupata watengeneza dawa.
Na ni wakati huo huo, viwanda kama Keko, na Arusha vilijengwa na kuanza kufanya kazi
Hiyo ni historia bila kugusa ni vipi tulishindwa kwenda mbele tokea hapo. Sababu zipo.
Wewe umegusia habari ya serikali kutoweza kufanya kazi inayoweza kufanikishwa na sekta binafsi. Mimi hili sikubaliani nalo, nikikupa mfano wa China.
Serikali zetu hizi zinaposhindwa kufanya kazi vizuri, tusiwe wepesi wa kukimbilia sababu rahisi rahisi kama unazoziangukia wewe. Tunakosa nidhamu inayotakiwa kwa watumishi kuwa nayo ili kufanikisha kazi hizo. Na hapa tunaweza kujadili kirefu kwa nini inakuwa hivyo. Sasa hivi siendi huko.
Kwa hiyo nihitimishe kwa hili kwa kusema kuwa sio kweli kabisa kwamba serikali haina nafasi yake katika viwanda vya namna hiyo.
Utengenezaji madawa una sehemu nyingi sana unazoweza kuzichambua. Baadhi ya hizo serikali hasa ndiyo yenye jukumu ya kuzisimamia.
Mfano mmoja ni huo wa kuwaandaa wataalam katika nyanja hiyo.
Kwa hiyo, unapomshauri rais, mwambie aweke mkazo zaidi na zaidi kuwapata wataalam walioiva vizuri katika utengenezaji madawa hayo.
Curriculum (kiswahili chake kimegota) iliyopo hapa nchini siku hizi katika eneo hilo inakazia zaidi katika kuhudumia wagonjwa mahospitalini; kuuza madawa madukani. Utengenezaji kwa sehemu kubwa umetupiliwa mbali.
Hilo ni moja linaloweza kufanywa na kusimamiwa naserikali kwa lengo maalum.
Kama serikali inavyosimamia baadhi ya mambo mhimu yanayoihusu nchi, serikali inaweza ikasimamia, tena kwa ufanisi kabisa kuanzisha viwanda vya 'Chemical Industry' ambako ndiko mali ghafi inakotokea. Nchi kama Taiwani wamethubutu na wakaweza. Nasi tukidhamiria tutaweza tu. Eneo hili ukisubiri "private sctor" wakujengee, utasubiri sana, kwa sababu zinazoeleweka kabisa.
Hilo ni la pili.
Utengenezaji wa dawa ulioukazia wewe, ni huo wa 'kuchanganya chemikali mbalimbali na kutoka na kidonge, sindano au mafuta ya kupaka n.k. Eneo hili hao "Binafsi" wanalipenda sana, ndio maana unawaona hao walioko Nyerere Road, karibu na uwanja wa ndege kule, na sehemu zinginezo.
Lakini hata katika eneo hili, serikali ingetaka, na ikawa na nia kweli ya kuifanya hiyo kazi ipasavyo, hakuna sababu yoyote ya kuzuia isiweze kuifanya kazi hiyo. Ni swala la nidhamu tu, hata nidhamu ya shurti ikilazimu, why not?
Maeneo haya ndio mimi binafsi ningependa aelekeze ukali wake rais bila ya kupepesa macho, hata mimi ningemuunga mkono.
Yooote niliyoeleza hapo juu, hii ni kazi za kizamani. Watu wamekwishaingia sasa kwenye viwanda tofauti kabisa na tunavyovizungumzia hapa. Watu wpo sasa kwenye "individualized treatment" - Biotechnology na Genetic engineering.
Viini alivyonavyo mgonjwa, tuseme kwenye damu yake, vinakusanywa kwenye 'testtube' na kutengenezwa kuwa dawa; vinarudishwa tena mwilini mwake vinapambana na ugonjwa unaomsumbua.
Usiseme sisi hatuwezi sasa hivi kujiandaa kwenda huko. Huo mfuko unaweza kuanza kupanda mbegu, na kama tunayo 'discipline' kama ninavyokazia hapa, miaka mitano hadi kumi hutatambua kwamba tulikuwa hatuna chochote tulipoanzia.
Ngoja nimalizie kwa kusema haya.
Nguvu kazi yetu mhimu tokea kianzishwe kile chuo pale Muhimbili ni kama tuliipoteza bure tu. Wale walioanza kwenye programu ile, wengi wao watakuwa wamestaafu au wamo njiani kustaafu. Elimu waliyoipata hawakuitumia ipasavyo. Ni kama unajenga barabara nzuri, halafu usiitumie, liwe pambo tu!
Ungekuwa ni mshauri wa Rais kama unavyosema hapo juu, ungeweza hata kumshauri awakusanye baadhi ya hawa watu awaweke kambini kama akitaka na kuwapa jukumu la kuhakikisha katika miaka miwili watoke na mpango kabambe wa namna ya kuanzisha viwanda vyetu vya dawa hapa nchini- si hivyo tu, hata waanze wao, kama kundi la wataalamu, au kama kazi wanayoifanyia serikali.
Hilo la kusema "serikali ikiwekewa vikwazo", umelivuruga. Tanzania ikiwekewa vikwazo ni pamoja na sekta binafsi iliyomo ndani yake.
Sasa niambie, hii ni
"Kifupi au Kirefu"? Mimi naona ni kifupi!