Nadandia kwa mbele hoja ya Rais kuhusu bima ya afya kuwekeza kwenye viwanda vya madawa

Kuhusu Bima ninafahamu biashara zao zilivyo,ila hapa tunaongelea bima ya afya kuwekeza kwenye kiwanda/viwanda vya dawa,Big No.Tanzania tayari tuna viwanda vya dawa na msd hawanunui huko,je hiki kiwanda kitamuuzia nani?
Napingana na ushauri wa NHIF kujiingiza katika biashara hiyo kwa sababu hats viwanda vilivyopo nchini havifanyi vizuri na vingine ni vya umma.Tusibadili NHIF na kufanya ifanye nje ya lengo LA kuanzishwa kwake.
 
Umenena vema,tusiivuruge NHIF kama tulivyofanya kwa mifuko ya hifadhi ya jamii.
 
Usipende kuchukulia Mambo kirahisi rahisi hivyo
 
Usipende kuchukulia Mambo kirahisi rahisi hivyo
Sawa mkuu.
Ningefurahi zaidi kama elezea zaidi wapi nimeongea ndivyo sivyo nijifunze kitu.
Mimi sijui chchite ndio maana nimekaribisha hoja zenu wadau wengine.

Au kuhusu kuuona huu ushauri Mh. Raisi?
Hii inaistwa unarushia kunde ukutani nyingi iwezekanavyo huenda moja inaweza kunasa ukutani.
 
Sawa mkuu.
Mawazo yako lazima yaheshimiwe, hakuna mawazo yasiyo na maana.
 
Sasa niambie, hii ni "Kifupi au Kirefu"? Mimi naona ni kifupi!
Hahaa hii ni katikati.
Maana mambo kadhaa umajadili ukaachia katikati, lakini nayaona muhimu sana.
Yanaweza kutunza kitu.

Mfano hapo chini
Sababu zilizo changia kushindwa kwa huu mradi ni zipi?
Nahisi zilikuwa urasimu na mambo ya bajeti.
Ikilazimu anzisha mada inayo jitegemea (thread) itakayo elezea vizuri wapi tulikwama. Uninukuu (quote) tu nami nije nijifunze.
Ni swala la nidhamu tu, hata nidhamu ya shurti ikilazimu, why not?
Mkuu unataka watu waende nje kulia kwamba sasa bwana mkubwa ameshakuwa dikteta kamili?
Hatuchelewi kusahau tulikuwa tunataka nini mambo yanapo pamba moto.
Kabla ya 2015 yalisikika sana maoni ya kutaka raisi mkali ikibidi mwenye udikteta kidogo, hata Mh. Kikwete aligusia hili aliposema "si mlikuwa manataka raisi mkali ? sasa nimewaletea huyu ni tinganga kweli".
Watu wamekwishaingia sasa kwenye viwanda tofauti kabisa na tunavyovizungumzia hapa. Watu wpo sasa kwenye "individualized treatment" - Biotechnology na Genetic engineering.
Nafikiri hii ingekuwa hatua ya pili (Phase II) au ya tatu ya mradi.
Tuanze na mambo rahisi kutekelezeka kisha tunaenda hatua moja mbele zaidi baada ya kufanikiwa hatua tulizo anza nazo.
 
Hilo la kusema "serikali ikiwekewa vikwazo", umelivuruga. Tanzania ikiwekewa vikwazo ni pamoja na sekta binafsi iliyomo ndani yake.
Hapana mkuu.
Inategemea na hatua ya vikwazo, kuna wakati inawekewa serikali na wabia au washirika wake toka sekta binafsi.
Kwa mfano Huawei alikuwa kwenye vikwazo lakini Tecno hakuweko.

Najua iuna wakati nchi au taifa zima linawekewa vikwazo taasisi zote za umma na binafsi au watu mmoja mmoja binafsi.
Kuna wakati ni baadhi tu ambazo zinafanya biashara moja kwa moja na serikali.

Sasa kwa kesi yetu NHIF inakopesha taasisi binafsi na hakuna mambo ya ubia wala ushirikiano wa aina yeyote ktk umiliki au ugawanaji faida za kiuchumi na hao watakao kopa.

Mtu akisha lipa deni lote na uhusiano unaishia hapo, isipokuwa wawekewe mashariti ya kutobadili biashara ili yasitokee kama ya awamu ya tatu viwanda vya nguo vinageuka warehouse (ghala) za biashara za samani au vioo kama pale Urafiki na kwingineko, Hapa malengo ya serikali sekta ya afya hayatafanikiwa.

Mwisho haya ni mawazo tu mimi na wewe hatupo ktk nafasi ya washauri wa Mh.Raisi.

Nimefurahi sana umeonesha mahali pa kuanzia pale chuo cha ufamasia MNH na blueprints zote za mradi wa viwanda vya dawa na UNIDO lazima zitakuwa kwenye makabati wizarani.
 
Labda wewe na mimi hatuuji na mkuu anajua akaunti za NHIF zinasomaje kwenye vitabu vya hesabu za mapato na matumizi.
Ndio maana kaongea vile.
Let's assume he know what he is talking.

Umetoa ushauri kwa jambo usilolijua. Huyo jamaa ni muongo wa kutupa.
 
Huyo jamaa ni muongo wa kutupa.
This is so negative.
Kwani waongo hawafanyi miradi au vitu flani vikafanikiwa?
Kwanza uongo ni ralative, unachoona wewe uongo kinaweza kuwa sio uongo kwa mwingine kutegemeana na kiwango cha taarifa za jambo husika ulizonazo muda huo.
 
Tunarudi katika miaka ya ujamaa.Tunaweza anzisha viwanda kwa mifuko ya umma lakini nani ajuaye rais atayekuja baada ya Magufuli atakuaje? Je akiwa mpenda rushwa? Na je akiwa mzembe na viwanda vikafa? Au tunajuaje serikali ijayo itaamua nini? Isije ikawa tunajenga halafu raisi ajaye akaamua kuvidhoofisha halafu akawauzia marafiki hivo viwanda kwa being chee! Mnakumbuka viwanda vya nyerere vimeishia wapi? Ni akina nani wamepewa buree na wametajirika na viwanda vilivyojengwa na nyerere?

Ushauri...
NHIF waingie ubia na sekta binafsi katika kuwekeza katika viwanda.Wasimiliki viwanda kwa asilimia zote.Wala wasimkopeshe MTU kujenga viwanda.Waende kutafuta watu wenye viwanda popote pale duniani,halafu waingie nao ubia katika kuwekeza kwenye viwanda vya madawa TZ.Hilo litaepusha kuuzwa au kugawiwa bure viwanda vya umma kwa utawala wowote ule ujao.Nafikiri serikali isimiliki viwanda kwa asilimia Mia kwa sector yoyote ile.
 

umeelezea sjui kwa hisia! ila nice explanations
 
BOOS ahsante kwa maoni yako mazuri.
Nina ombi moja kwako na kwa wachangiaji wengine tusinukuu (quote) maelezo yote ya madaa kuu.
Wewe tiririka tu hapo chini, unaweza kunukuu vipande vipande au una nukuu post za michango ya chini sio mada kuu.
 
This is so negative.
Kwani waongo hawafanyi miradi au vitu flani vikafanikiwa?
Kwanza uongo ni ralative, unachoona wewe uongo kinaweza kuwa sio uongo kwa mwingine kutegemeana na kiwango cha taarifa za jambo husika ulizonazo muda huo.

Ni muongo fullstop.
 
Kwa hiyo pesa za wanachama wa NHIF mkiziwekeza kwenye viwanda vya madawa,wanachama ambao pesa zao zinakatwa mtawagawia hisa?
Mkuu hivi fedha zinazoenda NHIF ,huwa zigawiwa Tena kwa wachama au zinatumika kwenye matibabu nafikili hoja yako Ni dhaifu sana Wala Haina mantiki yeyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri hii ingekuwa hatua ya pili (Phase II) au ya tatu ya mradi.
Tuanze na mambo rahisi kutekelezeka kisha tunaenda hatua moja mbele zaidi baada ya kufanikiwa hatua tulizo anza nazo.
Ngoja niku-'quote' kwenye kipande hiki pekee kwa sasa. Sikubaliani kabisa na mawazo haya.
 
Akili dogo pita hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huyo Stuxnet asikusumbue kichwa, mimi sioni mapumba pumba yake na matusi.
Nishambonyezea kitufe cha IGNORE zamani sana baada ya kuona anaumia sana na comment zangu utafikiri tunagombea mke.
Namshauri tu na yeye aniweke kwenye IGNORE list yake hataona post zangu, hatapungukiwa na kitu bali atajipunguzia aibu ya kuonekana hana busara, maana yaonekana hekima kwake ni msamiati mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…