Hoja yangu ni hii kweli corona ipo na rais amesema na amekiri.
lakini kusema sisi ni nchi hatari si kweli maana hakuna anaweza kuficha vifo vya watu wote tupo hapa tunatembea na tuna ndugu zetu na marafiki zetu lakini tatizo siyo kubwa kiasi hicho...
Kila kitu kinawezekana...kujitegemea kunawezekana...latin Amerika wako imara,walau wanajisimamia kwa kiasi kikubwa ila wametoka mbali, walieleza haswaaa hususan kwa RASILIMALI WATU. waliwekeza katika elimu kwa watu wao,wakawekeza ktk umoja....ulikua ni. Mpango maridhawa wa muda mrefu wa kujisimamia.... Ndio maana kina comrade Fidel na rafiki yake kipenzi comrade Hugo Chaves, wapumzike panapowastahili waliandaman sana na wamagharubi.
Nasema lazima tuwekeze ktk nyanja zote yakwanza ni RASILIMALI WATU (ELIMU, ELIMU, ELIMU). Tutaweza kubuni, kugundua, walau tuwe washindani ktk dunia hii ya ushindani ila sio kwa staili hii ya kukataa vibaya ilhali hatuwezi kuwa na. Mbadala. Tutumie manyanyaso hayo vyema,tuchukie manyanyaso hayo kwa kufanya jambo la muda mrefu la kudumu bila kutunushiana misuli ktk majukwaa na ktk media. Mkubwa ni mkubwa tuu
Na historia ni mwalimu mzuri, ni kweli bado Afrika na nchi zinazotiwa za dunia ya 3 zina sifa zile zile za enzi za ukoloni mf.sehemu ya kuwekeza, soko la bidhaa za magharibi, ni jalala la bidhaa,teknolojia na huduma zisizo na ubora.
Historia hiyo hiyo ya mapambano ya matumizi ya nguvu na majibizano ya hadhara hawajawahi kuwa na matokeo chanya sana kwa mataifa na viongozi wanaoonesha kuwa na misimamo hii ya kijamaa/kujitegemea/kuchukizwa na ubeberu. Kule Latini Amerika wamekufa zaidi ya marais Watano wenye misimamo mikali dhidi ya mabeberu kwa kupandikizwa Kansa.
Kati yao ni Hugo Chaves aliyekumbuka maneno na wosia wa Fidel wa kujilinda si tu kwa nguvu za Atomic au nyuklia bali kwa silaha za kibaiolojia toka kwa mabeberu baada ya kuwa hoi kitandani kule clinic CUBA. Kina Gadafi, Mugabe n.k.
Ni kweli si watu wema hata kidogo ila lazima tujipange, hakuna haja ya kulumbana majukwaani na mabwana wakubwa hawa. Si wakati wa kuropokeana,kupimana ubavu.... Simply hatuwawezi kwa ubavu, lazima tutafute suluhisho endelevu. Sisi tunapita ila Tanzania itakuwepo daima.