Nadhani hatuna shida kubwa kwa kiwango cha kutangazwa kuwa Tanzania ina maambukizi makubwa sana ya corona

Nadhani hatuna shida kubwa kwa kiwango cha kutangazwa kuwa Tanzania ina maambukizi makubwa sana ya corona

Kwani haufahamiki au kila mtu anaogopa kusema? Hata huyo Maalim Seif kama sio chama chake na yeye kuweka wazi, isingefahamika maana serikali wameficha. Sasa kama watu wanaficha hata hayo yasiyopaswa kufichwa, wengine kwanini wasituweke kwenye nchi hatarishi?
Maalim Seif na mkewe ni watu wawili Kati ya mamilioni ya Watanzania, haiwezekani kipimo cha Maalim kitumike kuwa ndiyo kigezo cha Tanzania kuwa nchi hatari Kwa maambukizi, huo ni upumbavu wa wazungu na tukiendelea kukubali ni kujidhalilisha!
 
Hoja yangu ni hii kweli corona ipo na rais amesema na amekiri.

lakini kusema sisi ni nchi hatari si kweli maana hakuna anaweza kuficha vifo vya watu wote tupo hapa tunatembea na tuna ndugu zetu na marafiki zetu lakini tatizo siyo kubwa kiasi hicho...
Wewe mjinga sana na huenda una uwendawazimu.

Juzi nimepoteza ndugu yangu aliyekuwa mfanyakazi wa Hospitali kwa Covid 19. Tumepoteza ndugu wengine wawili ambao wamefariki kwa kupishana siku 2, mmoja alizikwa juzi, mwingine leo.

Rafiki yangu amepoteza jamaa wa karibu 4 ndani ya wiki 3, halafu wewe unaleta huu upuuzi.

Kama hujafiwa, ungekaa kimya, umshukuru Mungu lakini usiseme kuwa **** kiwango kidogo cha maambukizi. Labda unataka ufe wewe ndiyo uamini kuwa kuna tatizo kubwa la maambukizi ya Covid 19 nchini mwetu.

Watu wengine mnatia hasira sana!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maalimu Seifu na mkewe ni watu wawili Kati ya mamilioni ya Watanzania, haiwezekani kipimo cha maalimu kitumike kuwa ndiyo kigezo cha Tanzania kuwa nchi hatari Kwa maambukizi, huo ni upumbavu wa wazungu na tukiendelea kukubali ni kujidhalisha

Waliopata ni wengi, ila huyo Maalim Seif kutokana na nafasi yake ndio maana katangazwa. Mimi nina watu watatu ninaowajua mpaka sasa wenye huo ugonjwa, na mmoja kutolewa oxgen juzi jumamosi jioni. Ni kwamba huo ugonjwa unaambukiza sana, ila unaleta vifo vichache maana wengi wanapona.
 
Waliopata ni wengi, ila huyo Maalim Seif kutokana na nafasi yake ndio maana katangazwa. Mimi nina watu watatu ninaowajua mpaka sasa wenye huo ugonjwa, na mmoja kutolewa oxgen juzi jumamosi jioni. Ni kwamba huo ugonjwa unaambukiza sana, ila unaleta vifo vichache maana wengi wanapona.
Asante Mungu Kwa kuwaponya hao ndugu zetu, lakini Ukweli Bado unabaki palepale kuwa hizi ni poropaganda zinazoletwa illi kuleta taharuki tu
 
Asante Mungu Kwa kuwaponya hao ndugu zetu, lakini Ukweli Bado unabaki palepale kuwa hizi ni poropaganda zinazoletwa illi kuleta taharuki tu

Propaganda wakati wagonjwa nimewaona kwa macho yangu, achia mbali waliokufa kwa ghafla? Alichopatia Magufuli kwenye huu ugonjwa ni kutokutuweka watu lockdown tu na sio kingine chochote. Ninashukuru kwa hilo maana angetuweka lockdown ningempinga sana hatimaye kuzidi kuonekana napinga kila kitu chake.
 
Swala la chanjo tumeshakubaliana. Watakaotaka watachanjwa na wasiotaka watajifukiza.
 
Naikataa hoja yako,kwanini tulikataa tatizo hili halipo, hatutakihata kuwaelimisha watu wachukue tahadhari, Tumekataa kutoa takwimu muda mrefu, kinyume na mikataba ya kimataifa tuliyoingia. Lete hoja kinzani tusonge mbele.
Umemsikia Jaffo?, Jifukize, kunywa matangawizi, fanya mazoezi na kazi mwili uwe imara, kula vizuri maisha yasonge, wakufa watakufa tuu, wakubaki watabaki wacheni kusema watangaze ili watu wasioingia JF na mitandaon nao waanze kuhara tumbo la uoga mapema
 
Hoja yangu ni hii kweli corona ipo na rais amesema na amekiri.

lakini kusema sisi ni nchi hatari si kweli maana hakuna anaweza kuficha vifo vya watu wote tupo hapa tunatembea na tuna ndugu zetu na marafiki zetu lakini tatizo siyo kubwa kiasi hicho...
Kila kitu kinawezekana...kujitegemea kunawezekana...latin Amerika wako imara,walau wanajisimamia kwa kiasi kikubwa ila wametoka mbali, walieleza haswaaa hususan kwa RASILIMALI WATU. waliwekeza katika elimu kwa watu wao,wakawekeza ktk umoja....ulikua ni. Mpango maridhawa wa muda mrefu wa kujisimamia.... Ndio maana kina comrade Fidel na rafiki yake kipenzi comrade Hugo Chaves, wapumzike panapowastahili waliandaman sana na wamagharubi.

Nasema lazima tuwekeze ktk nyanja zote yakwanza ni RASILIMALI WATU (ELIMU, ELIMU, ELIMU). Tutaweza kubuni, kugundua, walau tuwe washindani ktk dunia hii ya ushindani ila sio kwa staili hii ya kukataa vibaya ilhali hatuwezi kuwa na. Mbadala. Tutumie manyanyaso hayo vyema,tuchukie manyanyaso hayo kwa kufanya jambo la muda mrefu la kudumu bila kutunushiana misuli ktk majukwaa na ktk media. Mkubwa ni mkubwa tuu

Na historia ni mwalimu mzuri, ni kweli bado Afrika na nchi zinazotiwa za dunia ya 3 zina sifa zile zile za enzi za ukoloni mf.sehemu ya kuwekeza, soko la bidhaa za magharibi, ni jalala la bidhaa,teknolojia na huduma zisizo na ubora.

Historia hiyo hiyo ya mapambano ya matumizi ya nguvu na majibizano ya hadhara hawajawahi kuwa na matokeo chanya sana kwa mataifa na viongozi wanaoonesha kuwa na misimamo hii ya kijamaa/kujitegemea/kuchukizwa na ubeberu. Kule Latini Amerika wamekufa zaidi ya marais Watano wenye misimamo mikali dhidi ya mabeberu kwa kupandikizwa Kansa.

Kati yao ni Hugo Chaves aliyekumbuka maneno na wosia wa Fidel wa kujilinda si tu kwa nguvu za Atomic au nyuklia bali kwa silaha za kibaiolojia toka kwa mabeberu baada ya kuwa hoi kitandani kule clinic CUBA. Kina Gadafi, Mugabe n.k.

Ni kweli si watu wema hata kidogo ila lazima tujipange, hakuna haja ya kulumbana majukwaani na mabwana wakubwa hawa. Si wakati wa kuropokeana,kupimana ubavu.... Simply hatuwawezi kwa ubavu, lazima tutafute suluhisho endelevu. Sisi tunapita ila Tanzania itakuwepo daima.
 
Kimsingi huwezi ukatatua changamoto yoyote iliyopo katika level yoyote kama kwanza hujakuikubali changamoto hiyo kuwa ni ya kwako na inakuhusu wewe. Sasa huwezi kushauri hatua gani ichukuliwe na serikali ilihali viongozi wa serikali wanasema "Hatuna Korona"
 
Back
Top Bottom