Nehemia Kilave
JF-Expert Member
- Jan 9, 2022
- 1,414
- 3,118
Hebu tulia kama dakika tatu fikiri kwamba una binti yako ambae kiumri bado ana hitaji malezi kutoka kwako unamtoa kwenda kufanya kazi za ndani kwenye familia nyingine .
Nadhani kuna ugumu fulani labda kuwe na sababu inayo kulazimu kama hasa hali mbaya ya kimaisha/kiuchumi .
Sasa uwaze unachukua binti wa kazi ambae bado anahitaji malezi kutoka kwa wazazi , kutoka maisha magumu na mzazi wake anahitaji pesa sio kumuona kakimbia kazi kurudi nyumbani.
hivyo hizi nadhani ndizo sababu kuu zinafanya kumekuwa na matukio ya kikatili kutoka kwa hawa wadada wa kazi .
1. Shida ya Afya ya akili , kutokana na maisha na mazingira ya awali yameharibu afya ya akili ya mtoto/binti husika
2.Unyanyasaji kutoka kwa wenye nyumba - haya pia yanaweza leta Changamoto ya afya ya akili

>Inaweza kuwa mzigo wa kazi mkubwa sana
>Malipo hakuna au madogo sana kulingana na kazi
>Mateso
>Migogoro inayo husiana na mahusiano ya kimapenzi na baba wenye nyumba
Nadhani kabla hujamchukua mtoto yeyote ni lazima umjue vizuri na utambue bado anahitaji malezi ya familia hivyo usimchukulie kama mfanyakazi .
Soma pia UMAKINI KATIKA KUISHI NA DADA WA KAZI MAJUMBANI KWETU.