Ujambazi, udokozi hauna direct association na kukosa ajira ya kuendesha bodaboda, ninaamini kazi zipo mbadala zinazoendana na bodaboda kwa maana ya kipato chake.
Ninachokiona vijana wengi wamejificha kwenye kujifanya bodaboda ni ajira yao lakini wao asilimia kubwa sana ndio wahuni, wachora ramani za vibaka we kuja kukuvamia kwako.
Ninafahamu wapo vijana na ninawajua wamefanikiwa maishani kupitia bodaboda maana mie no mdau wa hiyo biashara Ila asilimia kubwa ni vijana wapuuzi sana uliza mwenye bodaboda kati ya 10 basi 7 au 8 watakuambia hawataki kabisa kusikia hiyo biashara sababu vijana hawana malengo hawaleti hesabu.
Nimemiliki pikipiki name sasa Ila nilipata hasara pikipiki tatu mpaka nikabadili namna ya kufanya biashara na pia nikabahatika kuchukua vijana kutoka mkoani kwa maana ya nyumbani hapo inasaidia Ila wakishajua mji wanaanza ulevi wa kunywa vitoko na kuuza spea
Yaani unanunua shock up ya mbele anakulia timing anauza anaweka mbovu usipokuwa makini unanunua Tena hata engine wanabadilisha washenzi sana .
Nawajua pia vijana Ila wachache wanafanya hiyo kazi na wanajenga na wanalisha familia Ila wao huwa wanafanya kazi kwa simu tu hawashindi vijiweni masaa yote na ikifika saa moja jioni wanaenda kulala hawana mambo mengi ya kuhuni na inawalipa sana wanakiri.
Kati ya vijana 10 basi 7 wanakuwa wanaendesha wamelewa wanakunywa vitoko, diamond, Kvant ya kupima za bukubuku.
Nimekuwa nakaa na vijana sana nawajua, wacha polisi wakomae otherwise tutapoteza hili taifa. Bodaboda anakuwa mwizi sababu alikuwa mwizi na ni mwizi tu wanajuana vijiweni.
Bodaboda anayeamua kuiba no sababu pikipiki haipo na amezoea kulewa masaa yote na kuvuta bangi ( wengi wao) Sasa anakuwa amekosa means ya kupata hivyo anarudia kazi yake ya zamani ya kuiba Ila kazi zipo kibao.
Nawajua vijana waliachana na bodaboda na Sasa wameajiriwa kwenye kampuni fulani walianza Kama utingo aisee Sasa hivi wanasukuma Scania za kokoto.
So usiwalaumu polisi wacha wafanye kazi yao, nadhani dawa ni kushirikiana na polisi ili kukomesha uhalifu jambo ambalo nafahamu ni gumu sana maana mhalifu wa kwanza ni polisi na wanawajua hao vibaka Ila wamekuwa wanawatumia kujipatia fedha haramu.
Polisi ni mwizi mwenyewe hao madogo ni kutia kiberiti tu.