Nadhani kama Mbatia ,Mnyika na Lissu wataunda Chama basi hiki ndicho kitakuwa Chama halisi cha Upinzani

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Kiuhalisia ukitoa wana harakati kama kina Mdude ,Mwabugusi na wengine wachache nchi inabaki na watu wachache sana ambao ambao wazalendo wa kweli na mioyo yao kila siku hunena mema kuhusu Tanzania .

Lisu , Mbatia na Mnyika ni moja ya watu makini sana na wazalendo Tatizo hawana nguvu za kichama , siku wakiungana tukapata chama hapa hata mimi ntawaunga mkono .

CCM kwa namna yoyote ile ni ya kutoka madarakani ila huwezi toa CCM na kuweka CHADEMA au ACT za leo hizi labda yatokee mabadiliko makubwa sana ya kiongozi .
 
Huna unachojua wewe!
Mnyika ni Katibu Mkuu wa CHADEMA na ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama na Tundu Lissu ni Makamu Mwenyekiti wa Chama waache nafasi hizo waende wakaanzishe Chama kipya!?
Itakuwa ni akili au matope!
Wafanye maboresho na Mageuzi tu ndani ya Chama chao na wanaweza kufika mbali.
 
Kuongea ukiwa nje ni rahisi sana. Ukiambiwa Leo uwe mwenyekiti wa CHADEMA kwa siku mbili ndio utajua ugumu wa hiyo kazi.
Atakuta Hela zote Mbowe amezikwangua. Atajuta
 
Yaani naona Mbowe anawatia wazimu sana. Imekuwaje mabandiko ya kumshambulia yanakuja dabalidabali??

Lissu na Mnyika ni CHADEMA ila wakitoka na kuunda chama kingine eti ndiyo wataweza kuitoa CCM madarakani.

Kwa nini watoke CHADEMA???
sasa mnyika ana nguvu gani hapo ya maamuzi ?
 
Mbatia yupi, yule aliywaidiwa ubunge na magufuli navgakuupata?
 
Vyama pinzani viko vingi lakini vyote hoi bin taaban!
 
Mtoe Mbatia hapo, acha kuwakosea heshima Mnyika na Lisu tafadhali.
 
Kwanini wewe usianzishe chama chako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…