Nadhani kiongozi wa serikali aliyepiga simu kuzuia geti ni Mwana FA

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
Kwa dhati kabisa naomba Rais Samia muondoe huyu naibu waziri kwenye hii nafasi anaitumia vibaya mno Kwa maslahi, mapenzi na ushabiki wake. Hii wizara wamepita mawaziri wengi ila ila huyu naibu waziri amekuwa kiongozi wa kutengeneza migogoro pale TFF

Huyu naibu waziri ametoa matamko ya kutia mashaka na kishabiki sana

1. Huyu ni shabiki na mwanachama wa Simba,

2. ukaribu wake na Rais wa TFF ambaye wote wanatokea Tanga unatupa mashakaka

3. Matamko yake kusema ati Yanga na Simba ni maasimu wakati sisi Huwa tunasema sisi ni watani wa jadi
Labda kama uhasimu anataka kuuleta yeye na TFF ya Karia

4. Kutangazia bunge kuwa derby ipo June 15
Katikati ya migogoro ya Yanga na bodi ya ligi, haikuwa busara Kwa kiongozi wa serikali kutangazia umma na Dunia kuwa derby ipo wakati akijua YANGA ana madai yake pale TFF na bodi ya Ligi
Huyu ndo kiongozi wa serikali anayeingilia mambo ya football

5. Alitukana viongozi wa CAF matusi baada ya Simba kupigwa final ya CAFCC
Huyu kiongozi aliyetukana viongozi wa CAF na waamuzi, hajui mipaka yake kwamba football inatakiwa ijiendeshe.
Ule ulikuwa upotokaji mkubwa nadhani Ile video na andiko lake likifika FIFA tunafungiwa
Kwa tabia hii unanipa mashaka kuwa ndo alipigwa simu geti lisifunguliwe

6 Kudanganya umma kuwa final ingechezwa Mkapa
Anadhani anavoamrisha akina na Mguto kufunga geti, angeamrisha watu wa CAF wenye weledi kuendesha na matamko yake

Mwana FA ameonekana ni kiongozi asiyetaka suluhu ya huu mgogoro wala kutojali matakwa ya Yanga, yeye anajali maslahi ya Simba na homeboy wake Karia wapige pesa pale TFF

Ki hekima serikali tena wizara ya michezo Kwa uchafu huu wa TFF wangewaita na kuwapa onyo au kutuma vyombo vya serikali kuwakagua

Agenda yake na TFF ni kuhakikisha Simba anakuwa bingwa Kwa vyovyote.
Na Jumapili anaenda kuwapa Simba ushindi wa mezani

Vijana tukipata madaraka tuyatumie vyema sio kulewa madaraka na kukandamiza taasisi zingine Kwa mapenzi na ushabiki wetu
 
Yaani Mwana FA anayeipenda Simba apige simu kwamba timu yake pendwa isifunguliwe mageiti?Yaani aungane na mabaunsa wa Yanga kuihujumu Simba?Timu anayoipenda!!!.It does not add up my friend. Njoo na uzushi mwingine Unamjua aliyepiga simu wacha kujitoa ufahamu.
 
Alipigwa simu ili kuikwepesha Simba kipigo mara ya 5 mfululizo kutoka Kwa Yanga
 
Yaani Mwana FA anayeipenda Simba apige simu kwamba timu yake pendwa isifunguliwe mageiti?Yaani aungane na mabaunsa wa Yanga kuihujumu Simba?Timu anayoipenda!!!.It does not add up my friend. Njoo na uzushi mwingine Unamjua aliyepiga simu wacha kujitoa ufahamu.
Vipi kama barua ya kususia mechi iliandikwa hata kabla hawajaenda uwanjani?
Vipi kama walienda uwanjani ili kujazia vielelezo kukidhi mpango wao wa kutocheza mechi?
Barua yao waliweka wazi kuwa hawatacheza mpaka pale uchunguzi utakapofanyika na wahuni kuchukuliwa hatua,je, uchunguzi umeshatoka na adhabu imesha tolewa?
Nini kinawavutia Simba kucheza na Yanga wakati dai lao halijatekelezwa?
 
Ile game simba key players wake kama 4 walikua injury,so planned ya kuvuruga ule mchezo ilikuwepo
 
Vipi kama barua ya kususia mechi iliandikwa hata kabla hawajaenda uwanjani?
Vipi kama walienda uwanjani ili kujazia vielelezo kukidhi mpango wao wa kutocheza mechi?
Barua yao waliweka wazi kuwa hawatacheza mpaka pale uchunguzi utakapofanyika na wahuni kuchukuliwa hatua,je, uchunguzi umeshatoka na adhabu imesha tolewa?
Nini kinawavutia Simba kucheza na Yanga wakati dai lao halijatekelezwa?
Yaani waliandika barua kabla ya kufanyiwa vurumai?Yaani wana uwezo wa kuona yatakayotokea baadaye?Waliridhika na uamuzi wa Bodi ya Ligi kuahirisha mechi kwa sababu za kiusalama na ahadi kwamba uchunguzi utafanyika na hatua zitachukuliwa.
 
Kanuni gani imeelekeza kuahirisha mechi kisa timu pinzani haijaufanyia mazoezi uwanja wa ugenini?
 
Nani kakuambia mechi imeahirishwa kwa sababu hiyo?Rejea Bodi ya Ligi walitoa sababu ipi ya kuahirisha mechi.
 
Back
Top Bottom