Nadhani Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lipo katika hali mbaya ya kifedha

Mkuu lakini ni vyema tufahamu kwa kina:-
1. Ikiwa pesa za ujenzi zilikuwepo ( mkopo kutoka kwenye mabenki) kwanini majengo hayo hayakamiliki.
2. Gharama zilizopelekea kuhisi wizi/ufisadi na Gharama za kuendelea na ujenzi baada ya kusimama muda mrefu, zipi kubwa?
 
Kujenga nyumba siyo kazi rahisi mkuu, ndo maana kuna taasisi kubwa mfano vyama vya siasa vikubwa na vikongwe lakini hadi leo vinaishi kwenye nyumba za kupanga.
Usihamishe magoli!

Ova
 
Msechu na genge lake wameshiriki kikamilifu kulifikisha shirika katika hali mbaya kiuchumi, yeye alikuwa ananunua ardhi kwa bei mbaya na wazabuni wenye bei mbaya huku ubora wa nyumba ukiwa wa chini!! UFISADI umechangia kuchoka kwa shirika
Huyo Huyo alipigiwa kampeni eti apewe u govoner BOT

Ova
 
Ni shida..
 
Sio sehemu yote ya deni la Taifa ni serikari ndio imekopa, kwenye total humo ndani kuna madeni ya mashirika ya umma ambayo serikari ni mdhamini tu na walipaji ni mashirika yenyewe.

NHC chini ya Nehemia walikopa zaidi ya 1 trillion shillings kwa sababu ya miradi yao ya ovyo deni ambalo mdhamini serikari na kuongeza rent kubwa sana kwa wapangaji mpaka ikawa kero ambayo mawaziri wote wawili Tibaijuka na Lukuvi ilibidi wampige stop.

Pamoja na hayo bado wakajikuta hawana capital za kumalizia miradi yao wanataka serikari iendelee kuwadhamini wakope naona Magu akaona upuuzi unaondelea na kuamua kumtimua.

Wakulaumiwa kwa tatizo la NHC ni aliekuwa CEO wao bogus Mr Msechu na raisi aliyepita JK kwa kuendekeza na kusifia upuuzi wake.

People warned early on strategy ya shirika chini ya Nehemia is not fit for sustainable business ni swala la muda tu kila kitu kitaenda kombo. Kama lawama za Magu ambazo hawezi kuzikwepa mbeleni kwa matumizi ya ovyo kwenye hii midege yake.

It doesn’t take much to predict the future and sustainability of Tanzania government businesses ventures many of their CEO are just not the parts.
 
Mbona shirika hili la NHC lilikuwa linafanya vizuri enzi za Msechu hatukuwahi kusikia ufisadi enzi zake au tatizo ni utumbuaji?
 
Msechu na genge lake wameshiriki kikamilifu kulifikisha shirika katika hali mbaya kiuchumi, yeye alikuwa ananunua ardhi kwa bei mbaya na wazabuni wenye bei mbaya huku ubora wa nyumba ukiwa wa chini!! UFISADI umechangia kuchoka kwa shirika
Hizo ni chuki kwa mchechu, mbona alipokuwa madarakani NHC ilikuwa juu sana?
 
shirika lilijitune kibiashara lakini akina lukuvi ghafla wakarirudisha liliko toka bila kuwa na strategy na kuwa kama la hisani tu na wapangaji wengine wameondoka maksudi maana hawajui kesho.(hakuna stability)

 

ukiona shirika linaanza kuendeshwa kisisa ndo ujue kaburi liko mbele yake.hili shirika lilikuwa linagawa nyumba kwa upendeleo na lilikuwa haliwatendei haki wanyonge hivyo likifa ni sawa tu ijapokuwa litawanyima ajira vijana wetu.tutaunda chombo kingine ambacho kitakuwa kinawatendea haki wanyonge.
 

Kwanini lisife in 10yrs awamu ya nne baadala life within 3yrs awamu ya tano..
 
Siyo rahisi kuunda shirika la nyumba popote pale.
Objectives lazima ziwe clear and yet profitable.
 
Msechu na genge lake wameshiriki kikamilifu kulifikisha shirika katika hali mbaya kiuchumi, yeye alikuwa ananunua ardhi kwa bei mbaya na wazabuni wenye bei mbaya huku ubora wa nyumba ukiwa wa chini!! UFISADI umechangia kuchoka kwa shirika
Nyie ndo haters.
Mchechu alikuwa kiongozi wa 21st Century.
Vikwangua aga alivyobuni inabidi viendelezwe.

Nyie mnaoridhika kuishi maisha yasiyo na maendeleo huko mabonde kuinama nani atawaingilia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…