Nadharia ya demokrasia ndani ya CHADEMA na ukomo wa kipindi cha Uenyekiti

Mtaendelea kukosa usingizi. Maotea mliyoyatuma yako hoi kama ilivyokuwa kwa Kiitila na wenzie.
 
....kama wengi wanataka Mbowe aendelee wacha aendelee, wanasema wengi wape, wachache wasikilize, but msitake kulazimisha mawazo yenu binafsi yawe ndio mawazo ya wengine!
 
Hayo uliyokaririshwa waonaje ukawaimbie huko huko kwenu mnakoogopa hata kumjadili mkiti wenu
Mkuu hayo yalisemwa sana hata wakati wa Awamu ya Nne.

Principle no 1: Kiongozi akibaki madarakani muda mrefu, hakuna ubunifu wowote kiuongozi.
Priple no 2: kioghozi huyo anarudi na watu wale wale
Principle no 3: Its business as usual.
 
Waonekana u mgumu kuelewa. Kukaa kwenye chama chenu hata milele sawa . Nchi ni tofauti na chama chenu.
Kwa hiyi mtaalam.
Sisi CCM tukikubaliana JPM akae madarakani na afanye vitu vyake vya maendeleo chanya kama tunavyoona , si itakuwa demokrasia vile vile?
 
Mleta mada utapata taabu juu ya ukomo wa uongozi katika nafasi ya mwenyekiti uko chadema. Ni hivi, Chadema apo mwanzo katiba yake ili onyesha ukomo ni vipindi viwili vya miaka mitano mitano, Alipo ingia DJ akanyofoa icho kipengele na kwasasa hakuna ukomo. Watetezi wa DJ wanadai ile katiba ya mwanzo haitumiki kwakua kipindi DJ anaingia nafasi ya mwenyekiti iliandikwa katiba Mpya ambayo kipengele cha mihula ya uongozi katika nafasi ya mwenyekiti kiliondolewa.

Yote kwayote ukweli ni kua hakuna kiongozi au mwanachadema anaye weza kuhoji ilo akiwa bado ndani ya Chadema.Ata uyo babamkwe wake kwasasa hawezi tena kumtoa ata akiwa anataka iwe hivyo. Siku ambayo DJ ata toka katika nafasi ile labda chama kisiwe na ruzuku na asiwena ushawishi wa kuteua viti maalum. DJ hawezi kuliachia fupa lenye urojo ndani.
 
CCM yakomalia ukomo wa uwenyekiti CDM Taifa.... !!
 
Mnahangaika kweli na Chadema hamchoki?
 
Hoja yako ni very logical mkuu lakini kwa mwenyekiti mwingine -sio Mbowe.
Shida ya hoja yako ni kuwa Mbowe ndiye aliyeiua CHADEMA 2015 kwa uroho wa mabilioni ya Lowasa.
Kitendo alichokifanya 2015 was suicidal kwa chama, na leo tunaona chama kilivyokosa mwelekeo na hata hakijulikani kinasimamia nini. Siku hizi UFISADI hata kuutamka tu tunajisikia AIBU. Hata zile nyimbo za kuhamasisha UMMA kupinga UFISADI hazipigwi tena kwa sababu maamuzi ya Mbowe yalituondolea kabisa UJASIRI huo.
Ni kweli TANU kiliongozwa na Mwal Nyerere kwa muda mrefu lakini Nyerere hajawahi badili msimamo wa chama kwa dili lolote la pesa na FISADI yeyote. Angebadili kijinga gia angani kwa tamaa ya pesa au wabunge koko naye angestahili kupisha wanasiasa wengine serious na wenye misimamo na misingi wanayoisimamia.
 
Kwani huoni kuwa upinzani unaelekea kifo cha mende kama hadi sasa upinzani hauna uongozi kwenye vijiji, mitaa hadi vitongoji mnategemea Mbowe atafanya miujiza gani ili 2020mchukue nchi?
Nimeshakueleza sitaku kujibizana na wewe kwa sababu hizi:
Akili zako ni kubwa kuliko zangu hivyo level ya reasoning ni tofauti sana
au
Akili zako ni ndogo sana kuliko zangu in such a way that tutapishana sana katika reasoning!

Sababu gani: Unaposema upinzani unakufa kwa vile hawana watu katika mitaa, vijiji, vitongoji etc wakati walisusia uchaguzi, ndipo nakuona akili zetu zimepishana sana.
 
Sasa hili linakuhusu kitu gani? Upuuzi mnaoufanya Lumumba mmeshaushughulikia? Kafagueni kwenu Kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…