Nadharia ya demokrasia ndani ya CHADEMA na ukomo wa kipindi cha Uenyekiti

Nadharia ya demokrasia ndani ya CHADEMA na ukomo wa kipindi cha Uenyekiti

Sasa wewe moumbavu, mbowe na Chadema wanakuhusu nini, nenda jahiji ukomo wa mwenyekiti wa CCM.
Mbowe ndie ameshindwa kusoma alama za nyakati. Anafikiri ataendelea kupendwa tu muda wote. Yeye na wafuasi wake wanapumbazana. Wamesahau kilichowatokea viongozi mbalimbali waliokuwa wanadhani wanapendwa mwishowe wakaondolewa kwa aibu. Wadadisi tunaendelea kutahadharisha.
 
Ni kiherehere changu tu kujiuliza swali la kimsingi kabisa la demokrasia ndani ya CHADEMA. Mimi si mwanachama wa chama hiki cha upinzani lakini ndio chama rasmi kinachoongoza kambi ya upinzani bungeni.

Sasa hivi CHADEMA wamo katika mchakato wa uchaguzi ndani ya chama na kati ya vinyang'anyiro ni uchaguzi wa Mwenyekiti. Kati ya majina yanayofikiriwa ni kumrudisha tena kwa mara nyingine Freeman Mbowe.

Huu ni usultani! Huwezi kuendesha demokrasia kwa kuwa na Mwenyekiti yule yule, timu ile ile, na uongozi ule ule katika upinzani, halafu tukajidai watatetea demokrasia ya nchi. Kama CHADEMA hawawezi ndani ya chama chao kurekebisha katiba kuweka ukomo wa uenyekiti, mtu anajiuliza kwa Taifa je? Si ni yale yale?

Kimsingi kutobadilisha katiba ili kuweka ukomo wa madaraka sababu yake ni kuendeleza ulaji. Wakati CCM wamebadili wenyeviti mara kadhaa ndani ya miongo miwili, upinzani majina ni yale yale; Mbowe, Maalim Seif n.k.

Dhana ya demokrasia haionekani ndani ya vyama vya upinzani. Ni unafiki kufikiri watatetea katiba mpya kitaifa pindi wakipata madaraka.

=====
Maoni ya wachangiaji
(MODS hapa mmeingilia uhuru wangu wa maoni. Ieleweke na wachangiajinkuwa hii quote sijai attach mimi)
Mzee km umeweza kuingia jf. Hujajua bado kuwa siasa nazo nibiashara? Kunasiasa za Ukombozi, Biashara,na zakutafuta KIKI , mbowe ndo nwenye hisa nyingi na chadema nichama cha kibiashara sasa mwenye hisa nyingi ndo mwenye power! Tatizo watu wanashobokea vyama bila kujua nichama cha aina gani, ukienda chadema nenda kwaajiri ya kupata posho na fulsa lkn cyo kuongoza. Chadema nichama cha kibiashara., ukitaka jujua na vingine uliza tutakujibu nauliza makato ya mishahara ya wabunge wa chadema yakila mwezi , lkn pia uliza nani mwenye hisa nyingi kama siyo mh. Mbowee na mzee marehem aliyefariki moshi. Na mzee mteii, ndo wenye hisa nyingi
 
Labda utakua hujui maana ya demokrasia, unafikiri kubadili viongozi tu ndo demokrasia?
 
Nihivi,ccm Haijawahi badili mwenyekiti wachama ,kwani mwenyekiti wa ccm ni cheo cha URAIS ,hivyo kwakua katiba ya nchi inam_bana kukaa kipindi kimoja au viwili kulingana na chaguzi basi ataendelea kua mwenyekiti.....basi nirahisi sana chadema kubadilisha kila awamu mwenyekiti kama na ccm mwenyekiti wao akiwa hana cheo cha urais(kivuli cha uenyekiti ccm taifa)......mana yake chadema wameona mbowe anaweza kupambana na hawa chama dola,nasio cha siasa
 
Ukijaribu kuuliza wasifu wa Mbowe, hasa ashule aliyosomea kidato cha nne na matokeo yake kabla hajaenda kujiunga kidato cha Tano, Jamii Forum aidha wanauondoa uzi au wanakupa ban? Kuna nini Jamii Forum mnazuia taarifa za watu kufahamu historia ya shule ya Chairman Mbowe?
 
Mzee km umeweza kuingia jf. Hujajua bado kuwa siasa nazo nibiashara? Kunasiasa za Ukombozi, Biashara,na zakutafuta KIKI , mbowe ndo nwenye hisa nyingi na chadema nichama cha kibiashara sasa mwenye hisa nyingi ndo mwenye power! Tatizo watu wanashobokea vyama bila kujua nichama cha aina gani, ukienda chadema nenda kwaajiri ya kupata posho na fulsa lkn cyo kuongoza. Chadema nichama cha kibiashara., ukitaka jujua na vingine uliza tutakujibu nauliza makato ya mishahara ya wabunge wa chadema yakila mwezi , lkn pia uliza nani mwenye hisa nyingi kama siyo mh. Mbowee na mzee marehem aliyefariki moshi. Na mzee mteii, ndo wenye hisa nyingi
From that angle of approach demokrasia according to CHADEMA, is ownership of the party by the founding members and sponsors.

Sioni basi wakiachia ownerdhip.
 
Ndio aina ya wanachama "watiifu" ndani ya CHADEMA.
Kwao timu ni ile ile, watu wale wale na masultani wale wale halafu wanategemea mabadiliko!
Hasiyo kuhusu unayatafuta nini. Mbona watu mnaangaika sana. Kama chama kinakufa mbona uchaguzi unawajambisha mpaka mnakuwa wachezaji na marefa? Si muache uchaguzi uru na tume uru muone mtakavyokimbizwa likwata li kruta
 
Wengi wa watetezi wa JPM na CCM ni Wasukuma. Jibu, Paskali and the likes.

P
 
Neil Kinnock aliposhindwa uchaguzi, pamoja na kuwa orator mzuri sana, chama chake Labour kikampumzisha ili iingie damu nyingine.

Sasa nyie ndugu zangu mnategemea Mbowe wa 1980s bado aishinde CCM ya 2020, you are expecting miracles!
Niweke wazi kuwa 2015 nilikuwa mmoja wa wanachadema tuliopinga kwa nguvu zote Lowasa kujiunga na kupewa ugombea urais wa Chadema. Hata tulipozidiwa nguvu niliandika humu JF kuwa madhali Lowasa amechukuliwa kwa kisingizio cha utafiti uliofanywa na kuonyesha kuwa atashinda, basi kama atashindwa Mbowe awajibike kwa kuachia uenyekiti, na hawa wengine wote waliotudanganya na tafiti feki wafuate mkondo. Hakuna aliyesikiliza na mpaka leo wanapeta kana kwamba hakuna kilichotokea.

Ninachotetea ni haki ya Mbowe, sawa na mwanachama mwingine yeyote, kugombea nafasi anayoona anafaa bila kuwekewa vikwazo hivi vya ukomo kwamba kakaa miaka mingi. Kama yapo mambo aliyoharibu (mfano hili la Lowasa) hayo ndiyo yangejadiliwa kuonyesha kutofaa kwake lakini kamwe hili la ukomo lisipewe nafasi.

Wapo wanaokuja na hoja dhaifu kuwa Mbowe aendelee kwakuwa Hanunuliki, hizo ni hoja za kipumbavu. Wanachama waachiwe waangalie na kupima kwa uhuru kama bado wanamhitaji Mbowe awaongoze au kama alipofikia imetosha basi wampumzishe achukue mwingine.

Habari ya ukomo ni uminywaji wa demokrasia.
 
Mkuu ukomo wa vipindi vya uongozi pamoja na kura ndio hewa inayoipa demokrasia uhai mahali popote.
Mbowe wa miaka zaidi ya 20 iliyopita hata awe na haki ya kugombea uongozi, kuna fatigue ya kumuona kila siku, na mbaya zaidi hana jipya.
 
Afrika kusini hawana ukomo, India hawana ukomo, Uingereza hawana ukomo, Ujerumani hawana ukomo, Israel hawana ukomo na kiongozi wao aliye madarakani anaburuzwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa. Nyie mlio na utititri wa wastaafu kwa huo ukomo baadhi yao wakiwa wahalifu ambao hamuwezi hata kuwashitaki mna demokrasia gani ya kuweza kujivunia ukilinganisha na hao niliokutajia?

Hao niliowataja wana-suffocate kwa kukosa hicho unachoita hewa?! Mkataeni Mbowe kwa uchovu wake, si kwa miaka aliyokaa kwenye uenyekiti.
 
Kiongozi akishindwa uchaguzi mmoja, kuna sheria isiyoandikwa kuwa aachie ngazi.
 
Swali langu huwa ni lile lile tu! Hivi kama Mbowe akifa leo chadema inakufa?
Maana kwa mtazamo yenu hicho chama hakina mtu mwingine zaidi ya Mbowe!
Yani hata vikundi vya vikoba haviko na mawazo kama haya yenu! Nyie mnakwama wapi kama taasisi?
Nimeona sredi humu JF, ati Mbowe haoni mtu wa kumuachia chama.
Atamuonaje huyo mtu wakati alikuwa busy kuwaondoa wapinzani gombezi wa nafasi yake?
 
Kiongozi akishindwa uchaguzi mmoja, kuna sheria isiyoandikwa kuwa aachie ngazi.
Hata mimi nimesema baada ya project yake ya Lowasa kushindwa alipaswa kuachia ngazi. Wanachama wangeshinikiza kwa hilo si hii habari ya ukomo. Tatizo huyu Mbowe ana mambo yanayomfanya ahofu kutoka kama haya madeni hewa anayokida chama.
 
Vyama vya siasa nchini viko kwenye mapambano, haviongozi nchi. Mimi nafananisha na majeshi yaliyokuwa yanapigania uhuru dhidi ya mkoloni katika nchi za Africa. Makamanda huwa hawabadilishwi badilishwi tu ili kufurahisha watu. Ni lazima timu ijipange kimkakati ili kufikia malengo. Vinginevyo utaingiza nyoka na kumwaga sumu. Mh Mbowe kaza uzi, panga safu yako vizuri, sasa ndiyo tumeingia kwenye hatua ya mwisho ya mapambano na asubuhi ni karibu. Msifanye makosa hapo, watu walioingia kwa mafuriko ya Lowasa 2015 ni wa kuwaendea kwa uangalifu mkubwa.

Asubuhi inakaribia
 
Cc
Hata mimi nimesema baada ya project yake ya Lowasa kushindwa alipaswa kuachia ngazi. Wanachama wangeshinikiza kwa hilo si hii habari ya ukomo. Tatizo huyu Mbowe ana mambo yanayomfanya ahofu kutoka kama haya madeni hewa anayokida chama.
Ccm pamoja na kuhodhi Mali nyingi za umma,hawajawahi kujitosheleza linapokuja swala hela,Matajiri hulazimishwa kuchangia fedha za kampeni,makampuni,ufisadi kwenye mifuko ya umma na mashirika ya umma,sasa sijui huwa mnaonaaje Mbowe anaposema anakidai chama kisichokuwa na income yoyote
 
Back
Top Bottom