Nadharia ya demokrasia ndani ya CHADEMA na ukomo wa kipindi cha Uenyekiti

Ni kiherehere changu tu kujiuliza swali la kimsingi kabisa la demokrasia ndani ya CHADEMA. Mimi si mwanachama wa chama hiki cha upinzani lakini ndio chama rasmi kinachoongoza kambi ya upinzani bungeni.

Sasa hivi CHADEMA wamo katika mchakato wa uchaguzi ndani ya chama na kati ya vinyang'anyiro ni uchaguzi wa Mwenyekiti. Kati ya majina yanayofikiriwa ni kumrudisha tena kwa mara nyingine Freeman Mbowe.

Huu ni usultani! Huwezi kuendesha demokrasia kwa kuwa na Mwenyekiti yule yule, timu ile ile, na uongozi ule ule katika upinzani, halafu tukajidai watatetea demokrasia ya nchi. Kama CHADEMA hawawezi ndani ya chama chao kurekebisha katiba kuweka ukomo wa uenyekiti, mtu anajiuliza kwa Taifa je? Si ni yale yale?

Kimsingi kutobadilisha katiba ili kuweka ukomo wa madaraka sababu yake ni kuendeleza ulaji. Wakati CCM wamebadili wenyeviti mara kadhaa ndani ya miongo miwili, upinzani majina ni yale yale; Mbowe, Maalim Seif n.k.

Dhana ya demokrasia haionekani ndani ya vyama vya upinzani. Ni unafiki kufikiri watatetea katiba mpya kitaifa pindi wakipata madaraka.

=====
Maoni ya wachangiaji

Anavunja katiba ya chama au ya serikali? Au unataka aachie ili kukufurahisha ww na familia yako?
Mwanaume mzima una wivu wa kike
 
Yote uliyoandika ni sawa kabisa! Awamu ya nne, Kikwete hakuapa, haadharani au kuonyesha dhamira ya kuua upinzani. Kweli muda ule ilibidi Mbowe aondoke. Lakini kwa sasa ndani ya magufuli, hapana! hapana!
Nakusubiri , maana nina uhakika 100% Magufuli atabadili katiba aongoze milele! Nitakusubiri urudi unieleze!
Swali langu huwa ni lile lile tu! Hivi kama Mbowe akifa leo chadema inakufa?
Maana kwa mtazamo yenu hicho chama hakina mtu mwingine zaidi ya Mbowe!
Yani hata vikundi vya vikoba haviko na mawazo kama haya yenu! Nyie mnakwama wapi kama taasisi?
 
Ni kiherehere changu tu kujiuliza swali la kimsingi kabisa la demokrasia ndani ya CHADEMA. Mimi si mwanachama wa chama hiki cha upinzani lakini ndio chama rasmi kinachoongoza kambi ya upinzani bungeni.

Sasa hivi CHADEMA wamo katika mchakato wa uchaguzi ndani ya chama na kati ya vinyang'anyiro ni uchaguzi wa Mwenyekiti. Kati ya majina yanayofikiriwa ni kumrudisha tena kwa mara nyingine Freeman Mbowe.

Huu ni usultani! Huwezi kuendesha demokrasia kwa kuwa na Mwenyekiti yule yule, timu ile ile, na uongozi ule ule katika upinzani, halafu tukajidai watatetea demokrasia ya nchi. Kama CHADEMA hawawezi ndani ya chama chao kurekebisha katiba kuweka ukomo wa uenyekiti, mtu anajiuliza kwa Taifa je? Si ni yale yale?

Kimsingi kutobadilisha katiba ili kuweka ukomo wa madaraka sababu yake ni kuendeleza ulaji. Wakati CCM wamebadili wenyeviti mara kadhaa ndani ya miongo miwili, upinzani majina ni yale yale; Mbowe, Maalim Seif n.k.

Dhana ya demokrasia haionekani ndani ya vyama vya upinzani. Ni unafiki kufikiri watatetea katiba mpya kitaifa pindi wakipata madaraka.

=====
Maoni ya wachangiaji
Unejiingiza Kichwani kichwa kwa mihemuko. Unataka kusema walioipisha Katiba ya CHADEMA hawajui?
 
Anavunja katiba ya chama au ya serikali? Au unataka aachie ili kukufurahisha ww na familia yako?
Mwanaume mzima una wivu wa kike
Mbowe anawategemea sana watu kama nyie maana ndio mtaji wake!

Huwezi kuitenganisha ccm na selikali vile vile chadema Ikishika madaraka huwezi kuitenganisha na selikali. Ndio maana huwa tunalaumu ccm kwa kutoa selikali isiyoleta maendeleo.

Chama kibovu kinazaa selikali mbovu.
Chama chenye usultani litazaa selikali ya kisulatani.
 
Ndio aina ya wanachama "watiifu" ndani ya CHADEMA.
Kwao timu ni ile ile, watu wale wale na masultani wale wale halafu wanategemea mabadiliko!
.....hivi kwenye uongozi huwa unaangalia sura za watu au utendaji kazi wao?!, mnajiona wajuaji kumbe vibuyu tu!, ni common sense tu, kama Mbowe anapigwa vita na ccm maana yake huyo ndie anaefaa kuwa kiongozi wa CDM, yani kwa maana nyingine, nyie mnaojidai hamna vyama na ccm lenu moja, na ujinga wenu ndio unaosababisha CDM waendelee kumchagua Mbowe.
 
Mkuu you missing the learned point.
Soma vizuri mada na uielewe.

Suala ni demokrasia siyo usultani Mbowe.

You have no moral right kudai demokrasia wakati you are not practicing it.
 
Sasa hivi CHADEMA wamo katika mchakato wa uchaguzi ndani ya chama na kati ya vinyang'anyiro ni uchaguzi wa Mwenyekiti. Kati ya majina yanayofikiriwa ni kumrudisha tena kwa mara nyingine Freeman Mbowe.

Huu ni usultani! Huwezi kuendesha demokrasia kwa kuwa na Mwenyekiti yule yule, timu ile ile, na uongozi ule ule katika upinzani, halafu tukajidai watatetea demokrasia ya nchi. Kama CHADEMA hawawezi ndani ya chama chao kurekebisha katiba kuweka ukomo wa uenyekiti, mtu anajiuliza kwa Taifa je? Si ni yale yale?
Usichanganye mambo. Demokrasia si kuwekeana vikwazo (ukomo). Waingereza hawana huo ukomo, sidhani kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia zaidi kuliko Uingereza.

Kwamba Mbowe anagombea kwa mara nyingine, tena akipambana na mmoja wa mawaziri wakuu wastaafu ni kipimo tosha cha demokrasia. Kwa mtazamo wangu, kinachopaswa kuaangaliwa ni kama kutakuwa na mizengwe yoyote kumpendelea mgombea fulani.

Waacheni wanachama wachague mtu wanayeona anafaa kuwaongoza. Hiyo ndiyo nguzo muhimu ya demokrasia.
 
Mkuu you missing the learned point.
Soma vizuri mada na uielewe.

Suala ni demokrasia siyo usultani Mbowe.

You have no moral right kudai demokrasia wakati you are not practicing it.
.....sasa demokrasia maana yake nini, kwani Mbowe huwa anajichagua mwenyewe?!
 
Si mnaimba chadema imekufa,sasa kinachowahangaisha kipindi hiki ni nini? Mafisiem hayajielewi,na bado mtasaga meno awamu hii.Waunga juhudi na wachumia tumbo tunawatembezea kichapo tu
 
Usichanganye mambo. Demokrasia si kuwekeana vikwazo (ukomo). Waingereza hawana huo ukomo, sidhani kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia zaidi kuliko Uingereza.

Kwamba Mbowe anagombea kwa mara nyingine, tena akipambana na mmoja wa mawaziri wakuu wastaafu ni kipimo tosha cha demokrasia. Kwa mtazamo wangu, kinachopaswa kuaangaliwa ni kama kutakuwa na mizengwe yoyote kumpendelea mgombea fulani.

Waacheni wanachama wachague mtu wanayeona anafaa kuwaongoza. Hiyo ndiyo nguzo muhimu ya demokrasia.
Mkuu nimekaa Uingereza tena nimepiga kura enzi za Iron Lady mama Thaatcher.
Unachokisahau ni kwamba kiongozi wa upinzani au chama kilichoshindwa anaachia ngazi kupisha wengine waje na mikakati mipya.

Nilishuhudia mpambano wa Margaret Thatcher(Conservarives) na Neil Kinnock(Labour) na kushiriki uchaguzi.

Neil Kinnock aliposhindwa uchaguzi, pamoja na kuwa orator mzuri sana, chama chake Labour kikampumzisha ili iingie damu nyingine.

Sasa nyie ndugu zangu mnategemea Mbowe wa 1980s bado aishinde CCM ya 2020, you are expecting miracles!
 
Kama atakuwa amepita kihalali kwenye sanduku la kura then haitokuwa tatizo...
Kwa hiyi mtaalam.
Sisi CCM tukikubaliana JPM akae madarakani na afanye vitu vyake vya maendeleo chanya kama tunavyoona , si itakuwa demokrasia vile vile?
 
Kuhusu hili mbowe na timu yake wanabugi sana hata sisi ma-layman wa siasa tunastuka sasa.
Waingereza wanasema you can fool some of the people ALL the time, and you can fool all the people SOME of the times.
BUT you cannot fool ALL the people ALL thr time.
 
Back
Top Bottom