Nadharia ya miaka 1,000 duniani ni sawa na siku moja mbinguni si sahihi kabisa




Mkuu salute sana tuuu....
Biblia imeweka wazi kila kitu ambacho mwanadamu anakihtaj kwa ajli ya usalama wake...kama kuna maswali unajiuliza na umefanya kila jitihada lakn umekosa jibu..basi jua kabisa hilo jambo halina umuhimu wwte kwako na hata ukilijua halitakusaidia ndo mana Mwenyezi Mungu hajalitolea ufafanuzi...mbali na hayo kuna mambo mengi sana ambayo hayajulikani kwa wanadamu walio wengi...lakn sababu siyo kwamba Mungu ameyaficha ila tatizo ni uzembe wetu wa kutosoma Biblia....
Wakristo wengi wamekuwa wakihubir kuwa mwisho wa dunia umekarbia bila kujua dhana hyo inatumika katika mazingira gani..

Matokeo yake wengi wameishia kukata tamaa na kuamua kuishi maisha ya dhambi wakiamini kuwa Mungu ameiacha dunia ijiendeshe yenyewe....Ukweli ni kwamba bado takriban miaka 1000 dunia ifike mwisho wake...ufuatao ni ushahidi wa kibiblia fuatana nami....

Namba saba katika Biblia
Biblia hutumia namba saba kama namba kamilifu kwa jambo fulani...mfano Mungu aliumba dunia kwa siku sita siku ya saba akapumzika Mwanzo 2:2..
Mungu pia anasema tufanye kazi kwa siku sita na siku ya saba ni ya kupumzika..Kutoka 23:12
Mifano mingine ni kama ifuatayo
Kutoka 21:2 Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miakasita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure.
Kutoka 23:10-11
Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kuyavuna maongeo yake; lakini mwaka wa saba utaiacha nchi itulie na kupumzika..
Joshua 2:2-5 ...fanya hivi siku sita. Na makuhani saba watachukua tarumbetasaba
za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba
mtauzunguka mji mara saba.

Hata ukisoma habari za naamani, safari ya saba kujichovya katika maji, ndipo akatakasika ukoma wake.
Eliya pia aliomba mara saba ili mvua inyeshe....1Wafalme 19
Kikawaida Mungu alimaanisha siku yenye mzunguko wa masaa 24 ambayo wanadamu huwa tunaitumia...Mwenyezi Mungu alidokeza pia kuwa kwake siku moja ni sawa na miaka elfu moja ya kibinadamu.. (hapa ndo kwenye kiini cha hoja hii) scenario ya namna hii huwez kuitumia popote ispokuwa kwenye unabii tena unabii mrefu sana...Kwa wataalamu wa Hesabu wanajua kuna wakati unapokokotoa swali la logarithms itakubidi kutumia concept ya exponent kupata jibu lililo sahihi..hvyo bas itatubid tutumie concept ya siku saba kama utimilifu wa jambo na badala ya kutumi siku kama siku tutumie siku=miaka 1000

ushahidi wa kibiblia unaonyesha kuwa tangu dunia kuumbwa ni takriban miaka elfu sita mpak sasa...kama mwaka mmoja ni sawa na miaka 1000 hii ina maana kuwa kwa mtazamo wa Mungu sasa ni siku ya sita na hii siku haijaisha ndo kwanza tumeianza (6017)...ili kufikia miaka 7000 bado miaka takriban 983 karbia 1000 ...so we have almost 1000 years to go and finish the game....
Yesu alibainisha kuwa kuelekea kufikia miaka elfu saba..watumishi wa kweli wa Mungu watapitia wakati mgumu sana ambao hakuna mtumishi yeyote aliyewahi kupitia tangu Dunia iumbwe na hvyo itamlazimu kufupisha siku hzo ili kuokoa wateule wachache watakaokuwa wapo hai (Mathayo 24:22..) hvyo miaka takriban elf iliyobaki inaweza ikapungua, hata hvyo bado ni miaka mamia kufikia huo mwisho....

Kuzaliwa kwa Yesu kulitokea lini
Adamu alipewa ahadi ya kuja kwa Yesu mara ya kwanza kama masihi..hata hvyo alikufa bila ahadi hyo kutimizwa...ahadi ilizidi kutolewa kwa watumishi wengine na waliitarajia kutokea kwa haraka hata hvyo Ibrahimu, Yakobo, Musa, Daudi na hata Danieli wote walikufa bila kuona Ahadi hiyo ikitimizwa...Yesu alitarajiwa kuokoa kizazi chote cha wanadamu tangu Adamu mpak pale mwisho wa dunia utakapofika..Yesu alizaliwa mwaka 4000 tangu dunia kuumbwa hii inaonesha kuwa alizaliwa katkat ya miaka 7000 japo ilizidi miaka 500 hii ilichangiwa na ugumu wa Wayahudi....Pia alizaliwa katikati ya dunia yote (Middle East is the center of the earth)...tokea Yesu azaliwe ni miaka 2017 sasa...ukijumlisha na ile miaka 4000 tangu dunia iumbwe tunapata miaka 6017...ili tufikie siku ya saba au miaka elfu saba tunahtaji miaka mingine karbia elf moja...hvyo bas bado miaka mamia kadhaa kuufikia ule mwisho....

Wanaosema Mwisho wa dunia umefika/umekarbia wapo sahihi?
Naweza nikakubali kuwa mwisho wa dunia umekarbia..hata hivyo jambo hili lipo kiroho zaidi...kwa Mungu ni bado masaa tu kufikia mwisho ila kwetu sisi hayo masaa kadhaa ni miaka mamia kadhaa ambayo kiuhalisia tuliopo hai sa hvi tutakutwa wote tumekufa...
Yesu aliwaambia wanafunzi naja upesi...hata walipokuw awanakufa waliamin kabisa kuwa atarud baada ya miaka michache tu lakn mpak sasa ni miaka 2000 imepita na bado dunia inasonga...
Swala la kifo ndo jambo la kuangalia zaidi kwa sasa kuliko mwisho wenyewe kwa sababu ukifa leo ni millsecond tu itakuchukua kuufikia ule mwisho wenyewe...haijalishi miaka mamia mangap itakuwa imepita tangu ufariki lakni kwako itakuwa ni sekunde tu au millsecond...Yesu aligusia hili akasema, Suala la kifo kwa wengi litafanya tukio la kuja kwa Yesu mara ya pili liwe la kushtukiza kama mwizi japo hata wale wataokutwa wapo hai wengi wao watastukizwa kam mwizi....(Hvyo usibweteke kuwa Yesu bado sana kurudi kwani kifo ambacho hakijulikan kitakuja lin ndo kizingiti kikubwa kwa sasa)

Baada ya siku sita au miaka 6999 or less than nin kitatokea ?
Baada ya siku sita siku ya saba watakatifu watapumzika na Mungu juu mbiguni kwa mda wa siku nzima ile siku ya saba ambayo ni sawa na miaka 1000. Biblia inaiita millenia mpya...

Je ni kweli hatujui siku wala saa ya kurudi mwana wa adamu au Yesu ?
Yesu alisema hakuna mtu ajuaye siku wala saa ya kuja mwana wa Adamu...hata hvyo dalili za kuja kwake ameziweka wazi..ni jambo la kuchunguza tu maana hata yeye mwenyewe alisema "Asomaye na Afahamu (Mathayo 24:15)"

Katika kumi bora ya watu maarufu wa mda wote waliowahi kuishi hapa duniani..wa nne kati yao wametoka ndani ya Biblia..huku Yesu akiwa ndo Mwanadamu maarufu zaidi kupita wote...

 
ngoja nitafute pakuanzia....

kwanza naunga mkono nadharia ya kwamba duniani miaka 1000 ni sawa na siku 1..
kama tunavyojua kuwa muda unatofautiana kati ya nchi na nchi,sayari na sayari nyingine,,,,
hakuna anayeijua physical location ya mbinguni ipo wapi angani,,
kwa mantiki hiyo mbinguni inaweza kuwa billion miles kutoka kwenye galaxy yetu,,,,

mfano mzuri ni proxima centauri hii ni nyota iliyo karibu na dunia,,,
mwanga wa jua kuufikia ni miaka 4.24,wakati dunia ni dakika 8..

na chombo cha nasa walichokituma voyage 1 mwaka 1977 kwenye space hadi kifike proxima centauri kitatumia miaka kama 80000,,,
hapo tuna assume hakuna error yoyote iliyotokea kwani mpaka sasa kimecover 1/600 light year ndani ya miaka 30,,,
lakini mpaka 2025 kitakuwa kime rest in space sababu energy itakuwa imekwisha.......

na kwa nadharia hii naunga mkono hoja mbinguni kuwa siku 1 ni sawa na miaka 1000 duniani..
kwa sababu hatujui location ya mbinguni ipo wapi.........
 
nadharia ya pili ni hii..
huenda mwandishi alikuwa anamaanisha Kwa Mungu hakuna chochote kisichowezekana
vitu tunavyoviona huku duniani ni vigumu kutekelezeka kwa sababu ya muda Mbinguni vinawezekana.....
naamini hii ndio sahihi zaidi
 
Hapana kwa mujibu wa biblia
 
Ahsante mkuu. Ila nadhani na wewe haujanielewa nilichomaanisha.
 
Mkuu umesema muda ni nini?

Kwa mujibu wa nini unaleta tafsiri ya muda..?

Tofautisha kati ya Muda na nyakati.
Tofautosha kati ya siku na muda.siku ina muda lakini muda unaweza usiwe ni siku.
 
ASANTE KWA HOJA YAKO NA MAONI YAKO MAZURI..

NAOMBA NIKCRASH POINT YAKO KWenye VIPANDE ELFU..
1.hata neno moja halitatanguka kwenye biblia ..dunia itapita lakin kwenye bible hata nukta haita pita...

2. ww umechanganya kipo cha muda na wakati...kwa maana ukisema kesho wewe unaelewa kwamba masaa 24 yajayo... lakin kiuhalisia icho ni kipimo cha muda ..hukuna kesho..kesho ni imagination yako... PIA KUMBUKA VIPIMO VYA MUDA NI VYA MWANADAMU KWA MUNGU KUNA UWEPO MWINGINE KABISAA NJE YA LOGIC YA BINADAMU YEYOTE .....

3. mfano mzur kuna mduduanaitwa tsetsefly kama sijakosea yeye anaishi maisha yake yote ndani ya maa 14 yaan anazaliwa anakua anazaa ndani ya huo mda ambao wewe unasema ni siku moja... kwaiyo siku moja kwao ni sawa na siku 24 kwake...
4. MUNGU SIFA YAKE NI KUWA YEYE NDIO MWANZO PIA YEYE NDIO MWSIHO... KILA KITOKEACHO KINATOKEA IN BETWEEN..

..
KWAIYO SWALA LA SIKU MOJA NI SAWA NA MIAKA ELFU NI SAWA.....SIKU MOJA MBAYO WEWE SISI TUNASEMA KUZAMA KWA JUA NA KUCHOMAZA ..NA SIO MAJIRA YA SAA ILIYOKIGANYANI MWAKO WALA ILIYO YA ATOMIC NI KWELI KABISA KWA MAAANA UFAHAMU A MWANADAMU HAUWEZ KUCHAMBUA YALIYO KATIKA HEAVEN KINGDOM..

.....

NIKURAHISISHIE UKIWA DUNIAN ..SIKU MOJA NDIO MAANA YAKE NINI????
AMEN
 
Namuunga mkono mtoa mada. Kwa Mungu hakuna muda ndio mana imeandikwa kwamba yeye anajua ulipotoka na unapokwenda kwasababu kila kitu kinatokea papo kwa hapo in real-time.

Kwahiyo miaka sijui elf hata mimi ninaridhia kuwa ni invalid kwasababu inamaanisha kwamba hata Mungu na mbingu siku moja vitakuwa na mwisho na Mungu alikuwa na mwanzo.

Nahisi hapo zamani waliandika miaka elfu moja kuelezea kwamba ni muda mrefu saanaa (incomprehensible). Time ni sisi tu 0 civilization beings inayotubana na kutufunga.
 
Roho Mtakatifu gani wakati Biblia iliandikwa na watu kwa maslahi yao wenyewe.
Hata kama kuna ambayo Mungu aliwahi kusema yamekuwa saturated sana.
 

Una matatizo, watu kama wewe ni wa kuombea na sioMama kujadiliana nao.
 
Mimi katika andiko langu nimekwambia jinsi gani haiwezekani lakini wewe kwa urahisi tu unaniambia inawezekana...huko pluto na mars tunasema tunapishana miaka kwakua kuna miezi na jua

11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.

1 Wakorintho 2 :11
 
Njoja nijenge hoja
Mwaka 1 duniani ni sawa na miaka mingapi kwenye sayari ya Jupiter au pluto. Kwa maana ya Jua kuzunguka dunia au sayari ya pluto .
Ukishajibu hapo haishindikani mwaka 1 duniani kuwa sawa na miaka 1000 mbinguni!

Hata tunapo hesabu huo muda bado tunatumia Earth years. Shida ni kwamba muda hautakiwi kuwepo kabisa kwenye maongezi ya Mungu kwasababu time ni sisi hapa sentients tunao experience hii kitu.

Na ili muda uwepo lazma kuwe kuna gravity. Inamaanisha mbinguni kuna gravity? Tena itahitaji gravity kubwa haswaa ili one day iwe 1000 earth years.
Hata hivyo mbingu ni hali siyo mahali.
 

11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
1 Wakorintho 2 :11
 
Roho Mtakatifu gani wakati Biblia iliandikwa na watu kwa maslahi yao wenyewe.
Hata kama kuna ambayo Mungu aliwahi kusema yamekuwa saturated sana.

Kwa nini unakosoa vitabu vya watu vya dini? Kama umeichoka na unaona haifai, si unaiacha?

Ila kuna wenzako waliikosoa mwishowe wakakiri, pamoja na kwamba hawaamini dini, dinini ustaarabu ambao umemfanya mwanadamu kuwa mtu bora......

We kama umeichoka usiongee sanasana, achana nayo, au tafuta inayokufaa.
 
11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
1 Wakorintho 2 :11
Kama agenda iliyopo nikutomjua Mungu basi tusingehangaika naye kabisaa. Tusinge sali wala kumuabudu.
 
Dini imesaidia sana kwenye civilization, sijakataa.

Na siwezi kuhama dini au kuanzisha ya kwangu because that's just stupid. Siwezi pia kuacha kukosoa kwa sababu nia yangu ni kumuabudu Mungu na si binadamu mwenzangu.

Hata hivyo nahisi umekosea njia kwasababu hili jukwaa ni la kuuliza na kukosoa kila kitu.
Kama unakereka usipite humu. Na kama unataka kunipinga nipinge na hoja siyo na kuniambia nisiulize wala nisikosoe.
 

Kosoa wanaofundisha Biblia, usikosoe Biblia, ni makosa mdogo. HAKUNA kosa kwenye uandishi, kuna makosa kwenye tafsiri.

Na tulipewa roho mtakatifu ili atusaidie tunapoona hatupati tafsiri nzuri, Mungu ameweka miundo mbinu mizuri sana kwenye kujifunza....

Kama hujaelewa mahali do not try to critisize, uliza, usibishane, mwombe Mungu.

11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
1 Wakorintho 2 :11
 
Sasa ulichoandika si ndio kukosoa kwenyewe?
Au maneno yako pia yapo lost in translation?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…