Nasisitiza kwa Mara nyingine tena, sikubaliani na fundisho la kwenye Bible na Qur'aan kwamba Mungu alimuumba mwanadamu ili amuabudu.
Sababu zangu kuu ni mbili:
1. Hakuna uthibitisho wala dalili yoyote ile kwenye nature inayo suggest kwamba Mungu ametuumba ili tumuabudu.
Ingekuwa huo ndio ukweli basi tungekuta dalili kwenye nature zinazo suggest hiyo dhana.. Kwa mfano tungekuta misikiti na au makanisa tayari yamejengwa bila kumjua alie yajenga ni nani au at least adhana au kengele ya kanisani zingekuwa zinalia kutoka angani kila ukifika muda wa swala/Ibada au makanisa na/au misikiti ingekuwa inachomoza duniani kama jua kila muda wa swala/ibada ukifika.
Au at least mwili wa mwanadamu ungekuwa unapata mabadiliko Fulani kila ukifika muda wa swala/ibada , mabadiliko ambayo ili mwili wako ukae sawa tena ni lazima ukaswali au kusali vinginevyo unapata madhara kama ayapatayo mtu asipo kula chakula au/na kunywa maji for let's say ten days or something.
2. Dhana kwamba " Mungu ametuumba ili tumuabudu haiendani na sifa za Mungu kama ambavyo zimeandikwa kwenye Bible na Qur'aan. Unaposema " Mungu ametuumba ili tumuabudu maana yake ni kwamba " Mungu na yeye ni muhitaji" anahitaji kuabudiwa.
Ndio maana ametuumba ili tumuabudu na ameumba hadi na Jehanamu ili wale watakao shindwa kumuabudu basi siku ya mwisho wanaenda kuchomwa Jehanamu. Yani hii dhana inafanya Mungu aonekane yupo so much desperate na kuabudiwa kiasi cha kuweka hadi sanctions kwa watakao shindwa, jambo ambalo haliwezi kuwa kweli hata kidogo.
Dhana ya kwamba Mungu ametuumba ili tumuabudu inafanya Sisi binadamu ndio tuwe na nguvu zaidi ya Mungu kwa sababu Mungu ndio anataka kuabudiwa na sio Sisi ndio tunataka kumuabudu.
Ndio maana kawatuma mitume na manabii wake kadhaa kwa ajili yetu. Kwa wakristu hadi yeye mwenyewe kaamua kuja duniani kama mwanadamu kwa ajili ya dhambi zetu. Hii inaonyesha Mungu ni muhitaji kiasi gani.
Muulize mchungaji au shekhe, "Unasema Mungu ametuumba ili tumuabudu, je tusipo muabudu atapungukiwa na nini? "
Watakujibu hatopungukiwa na kitu kwa sababu yeye Mungu amekamilika kwa kila kitu hakuna chochote kinachoweza kupungua kwake.
Haya waulize tena, je tukimuabudu Mungu kitu gani kitaongezeka kwake? Watakujibu hakuna kitakacho ongezeka kwake kwa sababu yeye amekamilika tangu mwanzo.
So kwanini mnawaambia watu Mungu ametuumba ili tumuabudu?
Watakwambia una kufuru.
Ukweli ni kwamba Mungu hajatuumba ili tumuabudu ingawa tukimuabudu sio jambo baya pia.
JE KWANINI MUNGU AMETUUMBA DUNIANI?
Jibu sahihi kuliko yote ni hili hapa👇👇👇👇👇👇
Anae jua sababu halisi kwanini binadamu tupo duniani ni yeye yule alie tuumba na kutuweka hapa duniani. Hakuna mwingine yoyote anae jua isipokuwa yeye. Na kwa dalili zote alie tuumba, bado haja disclose kwa mwanadamu yoyote kwanini ametuumba duniani.
Pengine anataka Sisi wanadamu kwa kutumia akili alizo tupa yeye ndio tunaitafute hiyo sababu mpaka tuijue.
Walio tunga Bible na Qur'aan wametumia haki yao Ku suggest ni kwanini wanadamu wapo duniani. Wameona ni kwa sababu alie tuumba anataka tumuabudu.
Lakini mimi sikubaliani nao, Nina wazo tofauti. Ndio maana maana mpaka sasa tayari nimesha suggest nadharia tano na hii ni ya sita kwanini ninadhani Mungu ametuleta duniani.
Na hii ndio. Nadharia yangu namba sita👇👇👇👇👇👇👇
Nadharia hii nimei azima kutoka kwa watunzi wa Bible, kwenye kitabu cha MWANZO 1:28.
Andiko linasema " Mungu akawaambia Adam na Hawa nendeni mkazaliane muijaze dunia"
Ninacho kisema hapa ni kwamba " WANADAMU WAMEUMBWA DUNIANI ILI. WAZALIANE WAIJAZE DUNIA YOTE".
Dunia ikisha jaa, Mungu mwenye dunia yake mwenyewe ndio atajua afanye nini. Anacho taka yeye nyinyi mzaliane muijaze dunia.
Nadharia hii ipo supported na maumbile asilia ya mwanadamu.
Nadharia hii iko supported by both Anatomy and Physiology.
Mwili wa mtu mke na mtu mume vyote kwa pamoja vina support hii nadharia.
Wanaume tuna maumbile ya kiume wanawake wana maumbile ya kike yanayo tutamanisha wanaume naturally.
Wanawake wana mifumo ya uzazi ambayo inafanya kazi subconsciouly.
Nadharia hii iko supported na universe. Menstrual circles of women is governed by the gravity between the moon and the earth. No menstrual circle no pregnant women on earth. Mwezi ukiwa pushed kwa sentimeta chache from its axis kiasi cha kuathiri it's gravity with the earth, hakutokuwa na mwanamke atakae kuwa na uwezo wa Kushika mimba juu ya uso wa dunia.
Na hali ikiendelea hivyo kwa miaka 200 then hakutokuwa na watu duniani kwa sababu watakao kuwepo wote watakuwa wamekufa within 200 years na hawatozaliwa wapya.
Tukipata watoto tunawapenda watoto wetu sana.
Wanawake kwa wanaume wasio pata watoto huhangaika dunia nzima kutafuta tiba wapate watoto.
Hii ni kwa sababu this will Of God on us on earth has been stamped in the universal mind and our mind just receive information from the universal mind.
Hakuna mwanadamu anae hangaika kwa waganga kutafuta dawa ya kumfanya amuabudu Mungu vizuri lakini kuna mamilioni ya watu wanatafuta dawa kupata watoto.
Hakuna mwanadamu anae kuwa desperate eti kwa sababu amekosa kanisa au msikiti mahali anapoishi lakini Wacha akose watoto.
Ukiwaza kwa kina utagundua ule upendo wa wazazi kwa watoto wao huwaga ni upendo wa Mungu mwenyewe. Na Mungu ndio anao walea watoto kuanzia wakiwa tumboni hadi wanazaliwa. Ni kwamba Mungu mwenyewe ndio huingia ndani ya nafsi za wazazi na kuwapenda /kuwalea watoto hao kupitia wazazi wao. ( Hufanya kwa sababu kiuhalisia yeye ndio anao wamiliki hao viumbe wake)
Ndio maana kwenye bible imeandikwa Mungu alisema. " Waheshimu baba yako na mama. Yako upate kuishi miaka mingi na yenye heri duniani" Kwa sababu ni yeye mwenyewe ndio hutulea kupitia wazazi wetu.
Anataka watu waongezeke waijaze dunia ili dunia ikisha jaa afanye hicho anacho taka kufanya ambacho atakifanya dunia ikiwa imejaa.
Je maisha yako yanaendana na kusudi hili la Mungu.
Nadharia namba 7 kukujia hivi punde.