Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuhusu ferry, Zanzibar ferries huwa zinazo route za Pemba Tanga, tena muda ni saa moja tu nilivyosikia (sijawahi kupanda).Habarini ndugu watanzania.
Ninaelekea Pemba kufanya study ya masuala ya mwani, majongoo bahati n.k nikitokea Tanga. Wazoefu na wenyeji wa huko naombeni uzoefu wa kimazingira, tamatuduni, hotel za bei nafuu, price za gari ndogo ya kukodi + driver wakati nikiwa huko na vitu vingine muhimu kuvifahamu kwa mtu ambaye si mwenyeji wa huko.
Lakini pia ningependa kufahamu kama kuna ferry ambazo zinatoka Tanga direct to Pemba.
Ahsanteni.
Wete, Chake-Chake na MicheweniHakuna ferry kwa sasa kuna speedboat Zanzibar 3 nauli ni 35k - 45k.
Hotel ni 25k + 30k na Selfdrive ni ngumu kdg kupata kama utakua huna mtu yoyote ambae unajuana nae uku ila unaweza ukapata
Migahawa ya kula ipo ila sio mingi sana ni ya kutafuta kwa tochi.
Unataka kufikia Pemba Sehem gan mkuu?
jini huyo amekuwa jiwe au?Kutupiwa majini ni kawaida!
arogwe kwa kipi alichonacho? Labda kama atakwenda kuchezea wake za watu.jiandae kurogwa,anyway mwezi huu majini yamefunga
Ahsante mkuuKuhusu ferry, Zanzibar ferries huwa zinazo route za Pemba Tanga, tena muda ni saa moja tu nilivyosikia (sijawahi kupanda).
Gari ya kukodi - bei nafuu ndiyo shida lakini gari zipo. Jaribu kukodi bajaji bei ni nafuu sana kwa sasa bado hazijachangamka.
Hoteli za bei nafuu: hiyo changamoto lakini ukitafuta kwa makini unaweza kupata guest houses za bei afadhali.
Nadhani eneo muafaka la kuishi ni Chake Chake kwani pale ni Center na itakuwa rahisi kwenda Mkoani au Wete kwenye shughuli zako.
Ila mkuu, kule mambo ya kwenda kwenye vyumba vya 'guest' na wageni wa muda mfupi wa jinsia tafauti hilo haiwezekani kabisa, weka hiyo akilini mwako.
Wewe tulia tu na ustaarabu wako, kama ni mkristo basi makanisa yapo utachagua unalopenda (Catholic, Anglican, Quakers, Seventh day), pale eneo la kambi ya jeshi Vitongoji kuna makanisa ya denominations tafauti.
Kwa hivyo kama ni Wete basi unaweza kutafuta guest house huko Wete kwa siku utakazokuwepo kule. Ama kwa Micheweni sikushauri utafute makazi kule ni vyema ukabaki hapo Wete lakini angalia usafiri kama unakuwa rahisi. Micheweni iko karibu zaidi na Wete kuliko Chake.Wete, Chake-Chake na Micheweni
OkWete, Chake-Chake na Micheweni
Ahsante mkuuKwa hivyo kama ni Wete basi unaweza kutafuta guest house huko Wete kwa siku utakazokuwepo kule. Ama kwa Micheweni sikushauri utafute makazi kule ni vyema ukabaki hapo Wete lakini angalia usafiri kama unakuwa rahisi. Micheweni iko karibu zaidi na Wete kuliko Chake.
Hivi Chake kweli kuna wakulima wa mwani? Sehemu gani hiyo? Maana naona watu wa Chake wengi ni wafanya biashara na wanatoka sehemu mbali mbali za mashamba.
Usikubali kulipiwa huduma yoyote au kupunguziwa yakheeeHabarini ndugu watanzania.
Ninaelekea Pemba kufanya study ya masuala ya mwani, majongoo bahati n.k nikitokea Tanga. Wazoefu na wenyeji wa huko naombeni uzoefu wa kimazingira, tamatuduni, hotel za bei nafuu, price za gari ndogo ya kukodi + driver wakati nikiwa huko na vitu vingine muhimu kuvifahamu kwa mtu ambaye si mwenyeji wa huko.
Lakini pia ningependa kufahamu kama kuna ferry ambazo zinatoka Tanga direct to Pemba.
Ahsanteni.
Sawa mkuuUsikubali kulipiwa huduma yoyote au kupunguziwa yakheee
SawaNeng'eneka uneng'enekavyo hakikisha hugusi mke wa Mtu!
naomba fafanua kidogo mkuu, ugumu wa kupata ushirikiano unatokana na nini?Kwa mwezi huu kuwa mgeni mtafiti Pemba... utapata tabu kidogo. Sio muda rafiki sana. Ni vigumu kupata ushirikiano kirahisi kama huna wenyeji.
ngoja nikufafanulie, kwa mwezi huu wa ramadhani huwezi kupata huduma ya breakfast kwenye hoteli au guest house za kawaida. Hata lunch itakuwa shida.naomba fafanua kidogo mkuu, ugumu wa kupata ushirikiano unatokana na nini?
Hoteli zipo chakechake pale. Bei ni kama elfu 50 about 3 years ago. Kwa wale wahuni Pemba hawatapawezaNdugu nipo very serious, lakini mnanijibu utani sana. Nahitaji kuwa na taafifa za kutosha ili niwe na picha ya mazingira ya huko, kuanzia gharama za maisha, hoteli, chakula, tamaduni zao, nini cha kufanya/kutofanya ukiwa huko na kila kitu muhimu.