Naelekea Pemba, naombeni uzoefu wa kimazingira

Naelekea Pemba, naombeni uzoefu wa kimazingira

Pemba wote wanajuana, mgeni unajulikana tu.
Usitongoze tongoze ovyo(muhim sana). Wengi wana mdudu anatoa taarifa kwa ndugu utaijiwa kuadhibiwa au kuozeshwa.
Kuna hadi fumanizi za kupangwa!
Binti, mke,na bibi wanafanana kwa sabab ya maumbo, uvaaji na salaam, hivyo usisimamishe holela jinsia ya kike sehem za wazi hata kama unaulizia huduma za kijamii. Tumia wanaume.
Penda kutembea na mwenyeji.
Vaa kwa namna ambayo dini yako haitatanabaishwa haraka endapo we si muisram.
....................karibu Gando
Sawa mkuu, ahsante sana
 
Pemba;

1. Uislam na tamaduni za kijima zimetawala sana kwani Elimu ya kisekula iko duni sana.

2. Umaskini ni mkubwa sana. Kule watu kutembea pekua ni kawaida(barefoot).

3. Urban culture the way ilivyo bara au unguja kule haipo kabisa.

4. Ubaguzi. Wapemba ni wabaguzi sana kwa wageni haijalishi ni muislam mwenzao. Ubaguzi huu unauona hata kwenye manunuzi. Bidhaa ambayo Mpemba anauziwa buku, mgeni utauziwa ef 5. Ila nimeambiwa kuna supermarket imefunguliwa last month.

5. Heshimu na weka mipaka na wake za watu kule. Wapemba reaction yao ni harsh hata kwa kitu ambacho huku bara huonekana ni kidogo.

6. Usafiri Tanga to Pemba, upo mwingi.

Kwa ujumla, PANAISHIKA.
 
Ahsanteni sana
 
Kwa hakika nimepata info nyingi kutoka kwenye huu uzi, ambazo zitanipa msaada mkubwa ktk safari yangu.
 
Kama unaenda kama mwekezaji ama explorer maana yake hela sio shida kwako maisha yatakuwa simple tu.
 
Ndugu nipo very serious, lakini mnanijibu utani sana. Nahitaji kuwa na taafifa za kutosha ili niwe na picha ya mazingira ya huko, kuanzia gharama za maisha, hoteli, chakula, tamaduni zao, nini cha kufanya/kutofanya ukiwa huko na kila kitu muhimu.
Ww unaona utani ila amini nakwambia mengi waliyokushauri ni ukweli mtupu, issue ya kurogwa, salamu nk

Na mm nakuingezea kule hakuna gest house Bali hoteli, hawali mchana Zanzibar nzima tumefunga, kaa mbali na vibinti/wake za watu.
 
Ndugu nipo very serious, lakini mnanijibu utani sana. Nahitaji kuwa na taafifa za kutosha ili niwe na picha ya mazingira ya huko, kuanzia gharama za maisha, hoteli, chakula, tamaduni zao, nini cha kufanya/kutofanya ukiwa huko na kila kitu muhimu.
Mkuu usiwe na wasiwasi, pemba ni kuzuri n watu wake ni wakarimu sana na wataratibu.
Mimi nimekaa huko , chakechake miaka mingi iliyopita.
Ni mahali pamepoa na watu hawana fujo yoyote.
Siku hizi naambiw kuna hotels nzuri tu Chakechake, lakini kma unaenda na boti basi utafikia Wete.
Wewe fanya kilichokupeleka ila usiingilie mambo yao na unatoka slama usalmin kama mimi nilivyotoka huko.
 
Ndugu nipo very serious, lakini mnanijibu utani sana. Nahitaji kuwa na taafifa za kutosha ili niwe na picha ya mazingira ya huko, kuanzia gharama za maisha, hoteli, chakula, tamaduni zao, nini cha kufanya/kutofanya ukiwa huko na kila kitu muhimu.
Di ndio hayo unayoambiwa hapo au hutaki? Kama wewe sio kijana wa muddy jiandae kupata shida huko hasa hasa kama unaenda wakati huu wa mfungu.

Pemba Iko kushoto sana. Isipojiunga CHAPUTA unaweza jikuta unapoteza ubingwa huko (mademu hakuna)

Kama wewe ni Mzee wa starehe au viwanja hilo sahau.

Yaani Bora ungeenda Unguja mara 100 kule kiwengea Kuna Walima mwani kibao Kijiji kizima wanawake wote Wana shomvi ya mwani.

Kiswahili chao isipokuwa makini utapata tabu sana kuwaelewa
 
Habarini ndugu watanzania.

Ninaelekea Pemba kufanya study ya masuala ya mwani, majongoo bahati n.k nikitokea Tanga. Wazoefu na wenyeji wa huko naombeni uzoefu wa kimazingira, tamatuduni, hotel za bei nafuu, price za gari ndogo ya kukodi + driver wakati nikiwa huko na vitu vingine muhimu kuvifahamu kwa mtu ambaye si mwenyeji wa huko.

Lakini pia ningependa kufahamu kama kuna ferry ambazo zinatoka Tanga direct to Pemba.

Ahsanteni.
Kuna Zanzibar 3 inasafari baina ya Pembeni na Tanga
 
Meli zipo, kuna Sea link, AKRAM kama sikosei, ila huko unapoeenda nyege zako acha nyumbani ukirudi utazikuta ukipuuza utarudi ukiwa chizi au kama wakiume utarudi ukiwa na mimba, hapo ndo ujiulize inawezekanaje. Tofauti na hapo jamaa ni waaminifu mnoooo hata ukisahau hela dukani kwa mtu au mahali ambako kuna watu utarudi na utaikuta
Hii hii pesa tunayoiamgaikia? Mdanganye
 
Kilichosalia sasa naombeni kupata majina ya hotel zilizopo Pemba kwa budget isiyozidi 150,000 kwa siku.
 
Mrejesho baada ya safari yangu ya Pemba:

Ahsanteni wote ambao mliweza kunipa ABC kuhusu Pemba - kisiwa cha marashi ya karafuu.

Niliyobaini

  1. Watu wa Pemba ni wakarimu sana sana sana.
  2. Pemba haina mwingiliano mkubwa wa watu
  3. Mazingira ya Pemba, uoto wa asili uliopo vinavutia sana
  4. Pemba ipo nyuma sana kimaendeleo ukilinganisha na Unguja, sikuweza kuamini kama barabara ya Mkoani - (mahali ambapo kuna bandari inayo tegemewa zaid kwa Pemba) kwenda Chakechake (mji mkubwa kwa Pemba) iwe katika hali ambayo ipo kwa sasa
  5. Pemba ina uhaba wa nyumba za kulala wageni (Lodge) hata hizo chache zilizopo ni bei ya juu sana
  6. Pemba ina hoteli chache sana na hizo zilizopo ni bei sana
  7. Gharama za chakula zipo juu sana (labda kwa sababu nimeenda kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani)
  8. Pemba inakubali kilimo cha mazao mbalimbali nimeona kilimo cha Karafuu, mihogo, mchele, ndizi nk hivyo mbali na shughuli zinazofanywa na wengi wao kama uvuvi, kilimo cha mwani nk bado wanayo fursa ya kufanya kilimo cha mazao hayo kujiongezea kipato
  9. Usafiri ni changamoto kubwa Pemba - usafiri mkuu ni chai maharage
  10. Nimeona jitihada za sasa za serikali kuwezesha sekta ya uchumi wa blue (wao wanasema uchumi wa buluu), kama vile vijana kupata mikopo ya boat, engine za boat, n.k
Katika yote nimependa sana jinsi walivyo wakarimu. Ila, mwenyeji wangu alinisisitiza kuna fumanizi nyingi za kutengenezwa hivyo niwe makini hata kama ni kwa nia njema nisisimame na mwanamke mahali pasipo salama, naweza fungishwa ndoa kinguvu au kulipishwa faini. Hayo ni machacke kati ya mengi niliyo yaona Pemba.
 
Back
Top Bottom