Naendelea kuunga mkono Urusi; Hoja zangu hazijajibiwa

Naendelea kuunga mkono Urusi; Hoja zangu hazijajibiwa

SABABU YA PILI; ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kutaka kujenga ngome ya kijeshi Ukraine, na katika kutimiza hilo Marekani kwakutumia washirika wake wa Nato wakamshawishi avunje Mkataba wa Minsk wa 2015 pamoja na mambo mengine, ulisema Ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Urusi (Ukraine) uliokuwa Umoja wa Kisoviet ya zamani Hautaruhusiwa kujiunga na Umoj wa Ulaya. Katika kibri cha Zelensk akaomba kujiunga Umoja wa Ulaya. Moscow akajibu kwa moto.
Mkuu Yericko Nyerere, Colonel Douglas Macgregor, afisa mstaafu wa jeshi la Marekani, pia anakusapoti hiyo sababubu yako ya pili.

Colonel Douglas Macgregor anasema kuwa Marekani ina nafasi ya kuepusha vita na Putin (Russia). Jambo la kwanza wanalopaswa kufanya Wamarekani ni kukiri na kukubaliana na nukta ya msingi ya Putin (Russia), ambayo serekali ya Russia imeiweka wazi kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Nukta yenyewe ni kuwa Russia hawataki majeshi ya Marekani, mizinga ya Marekani, na majeshi ya NATO kwenye mpaka wake na Ukraine (Mashariki ya Ukraine kwenye majimbo yaliyotangazwa huru na Putin).

Colonel Douglas akaendelea kusema: Kiukweli kabisa hata sisi Wamarekani hatukuyataka majeshi ya Russia na mizinga yake ndani ya Cuba (mwaka 1962), Putin naye hataki mambo hayo mashariki mwa Ukraine. Lazima tukubali madai hayo. Tuache kujifanyisha kuwa madai hayo hayana maana (ni ya kipuuzi).


===


COL. DOUGLAS MACGREGOR: Let me just reiterate something. I, like you and millions of Americans, would prefer that the troops headed to Eastern Europe right now were headed to the Mexican border. But I’m also very concerned that we find a way to avoid a conflict with Russia. The first thing we have to do is acknowledge that Putin’s basic point, not just his point, the Russian government’s point, which they’ve made for 25 years, is valid. They don’t want U.S. forces and missiles and NATO troops immediately across the border in eastern Ukraine. Absolutely. We didn’t want them in Cuba, he doesn’t want them in eastern Ukraine. We should acknowledge that. Stop pretending it’s a nonissue. It is a major issue for them. Let’s acknowledge it and then let’s get down to business and tell them fine, our concern at this point is we don’t want you to proceed west towards the polish border over the Dnieper River in Ukraine.
 
Kwako wewe Usalama wa raia wa Ukraine hauna maana; yaani unafurahia kuwaona wauwawa bila kosa vile?

Hicho kivuli cha Urusi kudai usalama wake ni bogus kabisa na ni wapumbavu tu wanaoweza kukiamni. Urusi inapakana moja kwa moja Marekani kwa karibu sana wakitenganishwa na eneo dogo sana la Berring Sea; mtu anaweza kueogelea kutoka Alaska kwenda Urusi na kurudi, lakini bado hawajahi kuweka jeshi kubwa pale au kusema waipige Alaska ili kulinda usalama wao.

Kwa nyie msiolewa, ukweli ni kuwa Putin anataka nchi zote zilizokuwa USSR zamani zote ziwe chini yake na zifuate amri yake tu; ni sawa na kusema Uingereza ilazimishe nchi zote zilizokuwa makoloni yake yafuate matakwa ya uingereza tu, jambo ambalo haliwezekani kabisa katika dunia ya leo. Nchi zile zilizobaki chini ya matakwa wa Putin ni zile ambazo zina marais wa maisha, kwa mfano Belarus, Azerbaijan na nyinginezo ambazo rais hachaguliwi na wananchi. Halafu Putini ana ubaguzi sana kwani anabagua wote wasiokuwa warusi kama vile hawana maana; utaona amekuwa analazimisha maeneo ya Ukraine ambayo yana watu wengi wenye asili ya urusi yajitenge na amekuwa anawapa silaha. Na anavyouwa watu wengine wa urusi ni kwamba anona hawastahili kuhisi anataka awamalize wote.
When Kichuguu speaks you have to sit down and take some notes.
 
Huelewi chochote kuhusu usalama wa Taifa.. Kama ingekuwa usalama wa Taifa ni usalama wa raia pekee jiulize kwa nini mataifa yanaingia vitani, kwani we huoni vita husababisha majanga kwa raia ( mauaji, umasikini, vikwazo vya kiuchumi, wakimbizi) ? Pia kwa nini nchi tofauti mfano Canada na USA ziwe nchi mbili tofauti kama usalama wa Taifa ni usalama wa raia pekee?

Kama usalama wa Taifa ni usalama wa raia pekee, kwa nini India ilijigawa na kuunda nchi mbili za India na Pakistan.

Kama usalama wa Taifa ni usalama wa raia pekee, kwa nini Tanganyika iliungana na visiwa vya Zanzibar? Kwa nini haikuungana Tanganyika na Zambia?

Kama usalama wa Taifa ni usalama wa raia pekee, kwanini USA na NATO walisupport kumpindua Gaddafi Libya?

Kama usalama wa Taifa ni usalama wa raia pekee, kwa nini USA waliweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya kampuni ya Huawei ya China?

Kama usalama wa Taifa ni usalama wa raia pekee, kwa nini North Korea na South Korea hazipatani abadani wakati ni ndugu wa damu?

Bila shaka huelewi chochote?
...
..
.
Anaemwambia Kichuguu hajui chochote kuhusu usalama wa raia ndiyo huyu anaetoa hizi hoja hapa 😀😀
 
Yeriko acha ni seme tu ww sio mtaalamu wa siasa kimataifa ukiacha na tule tuvitabu twako uliyotuandika kwa kuangalizia kwenye movie.

Yani ww mrusi anau watu bila hatia unasema unamuunga mkono.
Yeriko ww ni mtu mmoja katili sana ila haujapata nafasi.
kwa hayo mabandiko yako ipo siku yatakuja kukughalimu. Kwa sababu dunia imeisha kurecod.
Kwanza saizi nataka kukichoma moto kitabu ambacho uliniuzia. Kwa siwezi kutunza Takataka ambayo imeandikwa na mtu ambaye hajali maisha ya watu.
Ilikuwaje hadi ukashawishika kununua hicho ki pamphlet cha blah bla zake huyu.
 
Soma Alichokiandika....
Je inakaribia hata robo ya Ukweli?
Bado unarudia kile kile ninachokukatalia,wewe weka ukweli wako ukiniambia nirudie kusoma alichoandika mimi nitakwambia yupo sahihi.Wewe unaempinga ndiyo uthibitishe na siyo kuja na vijineno viwili na unataka tukuamini.
 
Bado unarudia kile kile ninachokukatalia,wewe weka ukweli wako ukiniambia nirudie kusoma alichoandika mimi nitakwambia yupo sahihi.Wewe unaempinga ndiyo uthibitishe na siyo kuja na vijineno viwili na unataka tukuamini.
Mtu anaandika kuwa Putin anataka kuwamaliza wote wasio wa Russia.
Hivi hili nalo linahitaji ushahidi, kuwa ni Uongo?
 
Kwako wewe Usalama wa raia wa Ukraine hauna maana; yaani unafurahia kuwaona wauwawa bila kosa vile?

Hicho kivuli cha Urusi kudai usalama wake ni bogus kabisa na ni wapumbavu tu wanaoweza kukiamni. Urusi inapakana moja kwa moja na Marekani kwa karibu sana wakitenganishwa na eneo dogo sana la Berring Sea; mtu anaweza kuogelea kutoka Alaska kwenda Urusi na kurudi, lakini bado hawajahi kuweka jeshi kubwa pale au kusema waipige Alaska ili kulinda usalama wao.

Kwa nyie msiolewa, ukweli ni kuwa Putin anataka nchi zote zilizokuwa USSR zamani zote ziwe chini yake na zifuate amri yake tu; ni sawa na kusema Uingereza ilazimishe nchi zote zilizokuwa makoloni yake yafuate matakwa ya uingereza tu, jambo ambalo haliwezekani kabisa katika dunia ya leo. Nchi zile zilizobaki chini ya matakwa wa Putin ni zile ambazo zina marais wa maisha, kwa mfano Belarus, Azerbaijan na nyinginezo ambazo rais hachaguliwi na wananchi. Halafu Putin ana ubaguzi sana kwani anabagua wote wasiokuwa warusi kama vile hawana maana; utaona amekuwa analazimisha maeneo ya Ukraine ambayo yana watu wengi wenye asili ya urusi yajitenge na amekuwa anawapa silaha. Na anavyouwa watu wengine wa Ukrainei ni kwamba anona hawastahili kuishi anataka awamalize wote.
Vipya Libya mkuu.. USA alivyo sababisha ubaribu mkubwa, kupoteza uhai na hadi libya unayo iona leo.. rudi pale Iraq.. na maeneo mengine.. mwisho wa siku haya mataifa yanalinda interest zao..
 
Nakili wazi bado sijapata majibu ya hoja zangu tatu za kwanini naunga mkono Urusi kuchukua hatua za Kijeshi Ukraine. Hoja zangu hazijajibiwa, wanaojaribu kujibu wanajibu kwa hisiasa zao bila kugusa hoja za msingi nilizozijenga wakati naweka msimamo wangu kwamba naunga mkono Urusi katika mgogoro huu. Leo ni siku ya 15 bado sijajibiwa na kushawishika kutengua msimamo wangu. Wakati naweka msimamo nilijenga sababu kuu Tatu na kuziorodhesha kama ifuatavyo;

SABABU YA KWANZA: ya kuunga mkono Urusi ni kwamba ni hatua muhimu ya kukomesha mauaji ya miaka karibu kumi sasa yanayofanywa na Ukraine dhidi ya Wananchi wa Majimbo ya Luhansk na Donetsk. Kwa msiojua Mtangulizi wa Rais Zelensk wa Ukraine, bwana Petro Poroshenko tangu ashike madaraka 2014 aliendesha mauaji ya wapinzani wengi katika majimbo ya DPR na LPR yaliyotaka kujitenga hadi alipoondoka tu vita havikumalizika.

Alipoingia Zelensk nae akafuata nyayo za mtangulizi wakw, akaigeuza Ukraine kuwa jehanamu kwa aliowaita waasi, aliendesha mauaji makubwa sana hasahasa 2021 dhidi ya raia kule katika miji ya Donbass katika kile alichokiita kudhibiti waasi wanaotaka kujitenga. Dunia hii ilikaa kimya, Urusi ikawa ndio pango la kupokea wakimbizi zaidi la laki tatu, Kiongozi Jimbo la Donetsk Bwana Denis Pushilin amenusurika mauaji zaidi ya marakumi hadi alipoomba ulinzi wa kimataifa kutoka Moscow, na mwisho akaongoza mapambano na kufanikiwa kujitangazia Uhuru.

Vile vile kiongozi wa jimbo la Luhansk bwana Leonid Pasechnik nae ilimlazimu kutafuta hifadhi ya kisiasa Moscow kwa lengo la kunusuru maisha yake dhidi ya Rais wa Ukraine bwana Zelensk aliyeapa kufuta uasi katika majimbo hayo, Aliongoza mapambano kwa ushirika wa Kiongozi wa jimbo la Donetsk bwana Pushilin na hatimaye wiki jana wamefanikiwa kumshinda Zelensk na Kujitangazia Uhuru. Urusi imeyatambua majimbo hayo kama nchi huru, Belarus na nchi nyingine tano tayari zimetambua. Ukraine imepinga uhuru huo ikaapa kuendesha vita nzito zaidi dhidi ya waliojitenga, Hatua hiyo ikawalazimu viongozi wa mapinduzi waombe msaada wa kijeshi kutoka Urusi. Na wameupata. Oparesheni ya Urusi ndio mwarobaini wa kukomesha mauaji ya miaka zaidi ya kumi sasa, kinyume na hapo miji itaendelea kuvuja damu kila kukicha.
Hoja hii ya kwanza inaungwa mkono na documentary hii ilitoka miezi sita nyuma kabla ya hii vita kuanza link Ukraine on Fire


SABABU YA PILI; ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kutaka kujenga ngome ya kijeshi Ukraine, na katika kutimiza hilo Marekani kwakutumia washirika wake wa Nato wakamshawishi avunje Mkataba wa Minsk wa 2015 pamoja na mambo mengine, ulisema Ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Urusi (Ukraine) uliokuwa Umoja wa Kisoviet ya zamani Hautaruhusiwa kujiunga na Umoj wa Ulaya. Katika kibri cha Zelensk akaomba kujiunga Umoja wa Ulaya. Moscow akajibu kwa moto.

SABABU YA TATU; ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kupitia shirika lake la kijasusi la CIA kuvuruga dili la Urusi la kujenga bomba la awamu ya pili la gesi maarufu kama NORD STREAM II, ambalo lingelisha gesi Ulaya yote kwa 90% tofauti na sasa mbapo Ulaya inategemea gesi ya Urusi kwa 40% tu, Marekani ameitumia Ukraine kukwamisha mradi huu na baadhi ya nchi za Nato. Kitendo hiki ilikuwa ni uchokozi wa kiuchumi na kijasusi, Jibu la Urusi limeanzia kwa Ukraine kwanza.

Hoja ya kwanza na ya tatu hazijaguswa na yeyote na nikama vile hawaoni kama ni sababu ama laaa, Lakini wako watu wachache wamejaribu kujibu kwakudonoa hoja moja tua hasa ile ya pili ndio imerudiwarudiwa kujibiwa lakini kwa majibu mepesa yanayotafsiri kwamba wengi hawaelewi dhana ya dunia na nguvu zake ama kijasusi huitwa Ushawishi wa Nchi, Na wako wengine waliweka msimamo tu wakupinga vita bila kueleza sababu, hawa dhana yao inalalia kwenye hoja ya pili pia bila kuwa na vuungo vya hoja.

Katika kuifafanua hoja ya pili na kuikazia hoja yangu ya kwanini naunga mkono Urusi. Naomba niseme kwamba, Dunia inawatu wanaotwa Wafanyamaamuzi, na kuna anaoitwa Watekelezaji wa maamuzi. Yaani kuna Super power countries, Karne ya 19 mkubwa duniani (Super power) alikuwa ni Urusi (Soviet Union), huyu aliamua mwelekeo wa dunia hadi alipoanguka 1989. Pamoja na kwamba Marekani alikuwepo na nguvu, lakini dunia ilikuwa na balance ya nguvu za kimagharibi na Mashariki.

Sijui kama watu wanakumbuka tukio la Cuban missile crisis USSR la October - November 1962, Soviet katika kilele cha nguvu zake na ubabe duniani waliweka makombora (missile) Cuba, kama eneo muhimu la kueneza Ujamaa Amerika ya Kusini na Kaskazini pia, Marekani walipofahamu tu jambo hili, ukaibuka mvutano mkubwa duniani uliohatarisha vita kuu ya pili duniani, Marekani walikizunguka Kisiwa cha Cuba kwa Meli na ndege kwa mwezi mzika, na mwisho makombora hayo yaliondolewa na Russia baada ya majadiliano ya mezani kama wakubwa sio vinginevyo. Marekani walionao ni hatari kwa usalama wao Soviet kuweka kituo chao cha Kijeshi Cuba, Tambua Cuba ilikuwa nchi huru kama Ukraine, yaani Cuba ileile ya mjamaa halisi Fedel Castro ambae alikuwa ni adui mkubwa wa Marekani hadi kufa kwake. Sasa anayeamini kuna uhuru wa nchi mbele ya Super power countries huyo bado ni mtoto duniani, akae kitako tuendelee kumfundisha kwamba uhuru unaojadiliwa na kusimuliwa ni ule wa kisiasa wa ndani tu wa vyama vya siasa na wa kuzungumza, nje ya hapo dunia ya tatu haiko huru na haitakuwa huru. Uhuru ni dhana pana sana. Haihusiani na Maslahi ya nchi kwa Marekani, Urusi na Uchina japo uchina bado hajajikomboa kufika viwango vya hawa wawili.

Sasa karne ya 21 Maslahi ya Urusi yanaguswa, Russia nae ana haki hiyo dhidi ya Ukraine. Uhuru wa nchi zote za mlengo wa kushoto unategemea msimamo wa Moscow, Hilo upende au usipende ndivyo dunia ilivyo. Vile vile Uhuru wa Nchi zenye mlengo wa Kulia unategemea msimamo wa Washington. Sera ya mambo ya nje ya Marekani ni muhimu na hutazamwa ndio eneo la usalama wa Marekani, Vivyo hivyo Sera ya Mambo ya nchi ya Urusi hii mpya chini ya Waziri shupavu Sergio Lavrov inalindwa kwa wino mwekundu kabisa kwakuwa ndio roho ya Kremlin.

Pengini watu hawajafahamu msingi wa India ambayo ni nchi muhimu sana kwa Urusi katika kuishinda Marekani kwenye vita vya ushawishi duniani kitendo cha kutochagua upande, na kwake ina maana kubwa sana katika geopolitics autonomy. India ni mteja mkubwa wa silaha za Urusi na ndege binsfsi. Hayuko tayari kupoteza fursa hiyo.

Nchi muhimu kwa USA za Israel, Saudia Arabia, UAE licha ya kuombwa kukemea operesheni ya kijeshi hadharani zimeamua kutochagua upande ni jambo tofauti kabisa na matarajio ya Marekani, sawa kabisa na nchi yangu ya Tanzania isiyofungamana na upande wowote.

Wako waliokosa hoja za kuipinga Urusi, badala yake wanabeza kwakusema kwanini hadi leo siku ya 15 bado tu Urusi haijateka mji mkuu Kyiv? Kwamba hii inaonyesha Urusi ali underrate vita hii, na kwamba Urusi ameshindwa vita. Binafsi naomba niwajibu hawa ndugu, Kama tutakubaliana kwa imani yangu ya Mizimu toka Mbutu Block E, Kigamboni niwakumbushe tu kwamba, Russia alilivamia Afghastan mwaka 1979 na kuondoka 1989, yaani aliikalia Afghanistan kimabavu kwa miaka 10 na alifanya hivyo baada ya Marekani Mjomba wake NATO kujaribu kuingilia vita kwakufadhili makundi ya ya Taliban ambayo makundi hayohayo baadae Marekani huyohuyo akatutangazia kuwa ni makundi ya Kigaidi.

Watu hawa wanaoipinga Urusi wanaenda mbali wanasema Marekani alivamia Iraq kwa siku chache tu akitokea Marekani, iweje Urusi iliyoko jirani na Ukraine inadhindwa kumaliza vita hadi leo? Majibu yangu kwao ni kwamba, Vita vya Marekani na Iraq vilipiganwa kutokea nchi vibaraka za Kuweit (669.9 km hadi mji mkuu Baghdad), Afghanistan (2,156 km hadi mji mkuu Baghdad) na Pakstan ( 2551 km hadi Baghdad). Havikupiganwa tokea moja kwa moja Marekani.

Vita vya Urusi na Ukraine vinapiganwa tokea Cremia (2,098.7 km hadi mji mkuu Kyiv), Donetsk (722.7 km hadi mji mkuu Kyiv) Luhansk (831.3 km hadi mji mkuu Kyiv) na Belarus (496.4 km hadi mji mkuu Kyiv). Izingatiwe na ieleweke kwamba, Marekani katika vita vya Uvamizi wake Iraq alikuwa na Ushirika wa Uingereza iliyovamia kutokea jiji la Basra, Ujerumani, Ufaransa, Australia, na ndugu wengine wa NATO. Lakini iliwachukua siku 23 hadi kuuteka mji mkuu Baghdad.

Je Urusi yuko na nani vitani, halafu hajapeleka jeshi lake halisi la Red Amy, anatumia majeshi ya nchi mpya zilizojitenga kama Cremia, Donetsk, Luhansk, Chechnia na wale Mercenary wa kirusi waitwao Wagner Group. Kuna majenerali wachache toka Vikosi maalumu Urusi wanaoongoza oparesheni lakini jeshi rasmi la Urusi liko standby kusubiri USA au NATO atie pua, Kilichomuondoa duniani Hitler watakiona live. Vita hivi vitaisha Urusi na Marekani wakikaa chini na kukubaliana yaani mazungumzo ya amani na si vinginevyo

Bado unasubiri nini?

Soma vitabu (Soft copy) vya Yericko Nyerere kwa 5,000/= tu kwa wiki kupitia App bora kabisa ya Vitabu Tanzania. Pakua sasa jisajili lipia wiki, mwezi au mwaka ujisomee vitabu vyote kupitia Play store Link 👉👉👉Yericko Nyerere App - Apps on Google Play

View attachment 2152327
haya mambo tuliyajadiri enzi hizo na ndugu yangu MALCOM LUMUMBA 😀
 
Wao kama Ukraine ni nchi yenye katiba yake na taratibu zake; Urusi wao pia wana katiba yao na taratibu zao. Inakuwaje Urusi iipangie Ukraine namna ya kujiendesha?
Katika ufafanuzi nimeeleza uhuru wa nchi unaoufikiri upo ni wa bendera tu mbele ya mataifa makubwa... Jiulize kwanini Taiwani inazuiwa na China kuwa mshirika wa USA? Kwanini Cuba ilizuiwa na USA kuwa mshirika wa Urusi? Ukiyajua hayo hautahoji hilo tena
 
Vipya Libya mkuu.. USA alivyo sababisha ubaribu mkubwa, kupoteza uhai na hadi libya unayo iona leo.. rudi pale Iraq.. na maeneo mengine.. mwisho wa siku haya mataifa yanalinda interest zao..
Siyo kweli. Marekani hakusababisha uharibifu huo; uharibifu ulisababishwa na walibya wenyewe walipoiga kufanya mapinduzi kama ya Tunisia. Marekani lisaidia upande mmoja wa mgogoro lakini siyo kuwa ilitangaza vita na Libya na kuiweka masharti ya kufanya. Hali ilikuwa vivyo hivyo kwa Misri na Syria, vurugu zilianzishwa na raia wenyewe.
 
Ngumbaru kabisa wewe nilikuwa nahisi unazo za kichwani kumbe ni shabiki tu.
Ndio maana likitabu lako haliuziki miaka nenda rudi utasoma na wanao
Nimekuja fasta nione kama UNAMJIBU jamaa kumbe nimeambulia matusi tu; hebu fafanua, elimu bora tutaipata kwa kua na mawazo kinzani. Toa hayo madini bhana
 
Yeriko acha ni seme tu ww sio mtaalamu wa siasa kimataifa ukiacha na tule tuvitabu twako uliyotuandika kwa kuangalizia kwenye movie.

Yani ww mrusi anau watu bila hatia unasema unamuunga mkono.
Yeriko ww ni mtu mmoja katili sana ila haujapata nafasi.
kwa hayo mabandiko yako ipo siku yatakuja kukughalimu. Kwa sababu dunia imeisha kurecod.
Kwanza saizi nataka kukichoma moto kitabu ambacho uliniuzia. Kwa siwezi kutunza Takataka ambayo imeandikwa na mtu ambaye hajali maisha ya watu.
Daa, simfahamu Yerico, sijawahi kusoma kitabu chake hata kimoja but michango yenu sometimes ndio mnamfanya aonekane Yerico ana akili; hivi ni kweli unashangaa Urusi kuua watu Ukraine halafu haushangai vita zingine zinazo endelea mashariki ya kati? Libya vipi? Iraq je??? Anyway but pia unaunga mkono mauaji aliokua akiyafanya rais wa sasa wa Ukraine ila hupendezwi na mauaji ya sasa ya Warusi huko Ukraine? Kumbuka vyote jamaa kaviandika humu; i thought, kama kweli hupendi mauaji then ungemlaani hata huyu rais wa sasa wa Ukraine kuua raia waliokua hawamuungi mkono, ungeandika pia kutopendezwa kwako na mauaji yanayo endelea sehemu zingine kama Syria, Iraq, Afghanistan, Libra to date hakujatulia etc. Mwishoni ningefurahi kama ningesikia UKIPINGA utengenezaji wa silaha za kisasa unaoendelea duniani kote, hapa ungelaani USA, Urusi, Korea ya kaskazini, China nk. I think umejificha kwenye mauaji yanaeyo endelea lakini chuki yako halisi ipo kwa Urusi, sio mauaji
 
Katika ufafanuzi nimeeleza uhuru wa nchi unaoufikiri upo ni wa bendera tu mbele ya mataifa makubwa... Jiulize kwanini Taiwani inazuiwa na China kuwa mshirika wa USA? Kwanini Cuba ilizuiwa na USA kuwa mshirika wa Urusi? Ukiyajua hayo hautahoji hilo tena
Kuna makosa natika perspectives zako, yaani unatoa tafsiri zisizo za kweli. Miaka ya nyuma kidogo wakati wa Kikwete, Marekani ilitaka kufungua ofisi yake ya Africa Command hapa Tanzania kwa vile sasa hivi iko ujerumani ambako ni mbali sana na Africa. Tanzania ilikataa, na wala hawakutumia nguvu kutulazimisha tukubali ingawa wangeweza kufanya hivyo kwa mabavu kama haya ya urusi.

Cuba haijawahi kuzuiliwa kuwa mshirka wa Urusi, in fact maisha ya cuba yamekuwa yanaitegemea urusi miaka yote. Walizuiwa kutumika kama kituo cha kijeshi cha urusi, lakini siyo kuwa na urafiki na urusi.

China na Taiwani kuna mgororo wa kihistoria baina ya Chiang Kai Shek na Mao ambao bila kuuelewa umekimbilia kwenye false conclusions
 
Siyo kweli. Marekani hakusababisha uharibifu huo; uharibifu ulisababishwa na walibya wenyewe walipoiga kufanya mapinduzi kama ya Tunisia. Marekani lisaidi upande mmoja wa mgogor lakini siyo kuwa ilitangaza vita na Libya na kuiweka masharti ya kufanya. Hali ilikuwa vivyo hivyo kwa Misri na Syria, vurugu zilainzishwa na rai wenyewe.
Mkuu rudia vizuri ya Libya.. but mwisho wa siku mataifa makubwa yote yanalinda interest zao. na yapo tayari hata kuua.. na kuangamiza..
 
Back
Top Bottom