Naendelea kuunga mkono Urusi; Hoja zangu hazijajibiwa

Naendelea kuunga mkono Urusi; Hoja zangu hazijajibiwa

Nakupongeza sana Mkuu Yerico,
Umeandika ukweli mtu,Hali halisi na mambo mazito sana.
Umeandika hoja zilizojaa uhalisia na hoja zilizoshiba.

Ila kitu kimoja ,watu wote wanaokupinga hayo uliyoyaandika Yako juu ya uwezo wao kuyaelewa..
 
Mtu anaandika kuwa Putin anataka kuwamaliza wote wasio wa Russia.
Hivi hili nalo linahitaji ushahidi, kuwa ni Uongo?
Tuishie hapa naona hatuwezi kuelewana kabisa.Nilitegemea utuwekee ukweli uliojitosheleza badala yake unakuja na vijimaswali juu ya maswali,sasa unataka nikujibu nini wakati wewe ndiyo unapaswa utetee hoja yako.
 
Kwako wewe Usalama wa raia wa Ukraine hauna maana; yaani unafurahia kuwaona wauwawa bila kosa vile?

Hicho kivuli cha Urusi kudai usalama wake ni bogus kabisa na ni wapumbavu tu wanaoweza kukiamni. Urusi inapakana moja kwa moja na Marekani kwa karibu sana wakitenganishwa na eneo dogo sana la Berring Sea; mtu anaweza kuogelea kutoka Alaska kwenda Urusi na kurudi, lakini bado hawajahi kuweka jeshi kubwa pale au kusema waipige Alaska ili kulinda usalama wao.

Kwa nyie msiolewa, ukweli ni kuwa Putin anataka nchi zote zilizokuwa USSR zamani zote ziwe chini yake na zifuate amri yake tu; ni sawa na kusema Uingereza ilazimishe nchi zote zilizokuwa makoloni yake yafuate matakwa ya uingereza tu, jambo ambalo haliwezekani kabisa katika dunia ya leo. Nchi zile zilizobaki chini ya matakwa wa Putin ni zile ambazo zina marais wa maisha, kwa mfano Belarus, Azerbaijan na nyinginezo ambazo rais hachaguliwi na wananchi. Halafu Putin ana ubaguzi sana kwani anabagua wote wasiokuwa warusi kama vile hawana maana; utaona amekuwa analazimisha maeneo ya Ukraine ambayo yana watu wengi wenye asili ya urusi yajitenge na amekuwa anawapa silaha. Na anavyouwa watu wengine wa Ukrainei ni kwamba anona hawastahili kuishi anataka awamalize wote.
VLADMIR PUTIN NI SHETANI MWENYE FORM YA BINADAM.
 
Nakili wazi bado sijapata majibu ya hoja zangu tatu za kwanini naunga mkono Urusi kuchukua hatua za Kijeshi Ukraine. Hoja zangu hazijajibiwa, wanaojaribu kujibu wanajibu kwa hisiasa zao bila kugusa hoja za msingi nilizozijenga wakati naweka msimamo wangu kwamba naunga mkono Urusi katika mgogoro huu. Leo ni siku ya 15 bado sijajibiwa na kushawishika kutengua msimamo wangu. Wakati naweka msimamo nilijenga sababu kuu Tatu na kuziorodhesha kama ifuatavyo;

SABABU YA KWANZA: ya kuunga mkono Urusi ni kwamba ni hatua muhimu ya kukomesha mauaji ya miaka karibu kumi sasa yanayofanywa na Ukraine dhidi ya Wananchi wa Majimbo ya Luhansk na Donetsk. Kwa msiojua Mtangulizi wa Rais Zelensk wa Ukraine, bwana Petro Poroshenko tangu ashike madaraka 2014 aliendesha mauaji ya wapinzani wengi katika majimbo ya DPR na LPR yaliyotaka kujitenga hadi alipoondoka tu vita havikumalizika.

Alipoingia Zelensk nae akafuata nyayo za mtangulizi wakw, akaigeuza Ukraine kuwa jehanamu kwa aliowaita waasi, aliendesha mauaji makubwa sana hasahasa 2021 dhidi ya raia kule katika miji ya Donbass katika kile alichokiita kudhibiti waasi wanaotaka kujitenga. Dunia hii ilikaa kimya, Urusi ikawa ndio pango la kupokea wakimbizi zaidi la laki tatu, Kiongozi Jimbo la Donetsk Bwana Denis Pushilin amenusurika mauaji zaidi ya marakumi hadi alipoomba ulinzi wa kimataifa kutoka Moscow, na mwisho akaongoza mapambano na kufanikiwa kujitangazia Uhuru.

Vile vile kiongozi wa jimbo la Luhansk bwana Leonid Pasechnik nae ilimlazimu kutafuta hifadhi ya kisiasa Moscow kwa lengo la kunusuru maisha yake dhidi ya Rais wa Ukraine bwana Zelensk aliyeapa kufuta uasi katika majimbo hayo, Aliongoza mapambano kwa ushirika wa Kiongozi wa jimbo la Donetsk bwana Pushilin na hatimaye wiki jana wamefanikiwa kumshinda Zelensk na Kujitangazia Uhuru. Urusi imeyatambua majimbo hayo kama nchi huru, Belarus na nchi nyingine tano tayari zimetambua. Ukraine imepinga uhuru huo ikaapa kuendesha vita nzito zaidi dhidi ya waliojitenga, Hatua hiyo ikawalazimu viongozi wa mapinduzi waombe msaada wa kijeshi kutoka Urusi. Na wameupata. Oparesheni ya Urusi ndio mwarobaini wa kukomesha mauaji ya miaka zaidi ya kumi sasa, kinyume na hapo miji itaendelea kuvuja damu kila kukicha.
Hoja hii ya kwanza inaungwa mkono na documentary hii ilitoka miezi sita nyuma kabla ya hii vita kuanza link Ukraine on Fire


SABABU YA PILI; ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kutaka kujenga ngome ya kijeshi Ukraine, na katika kutimiza hilo Marekani kwakutumia washirika wake wa Nato wakamshawishi avunje Mkataba wa Minsk wa 2015 pamoja na mambo mengine, ulisema Ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Urusi (Ukraine) uliokuwa Umoja wa Kisoviet ya zamani Hautaruhusiwa kujiunga na Umoj wa Ulaya. Katika kibri cha Zelensk akaomba kujiunga Umoja wa Ulaya. Moscow akajibu kwa moto.

SABABU YA TATU; ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kupitia shirika lake la kijasusi la CIA kuvuruga dili la Urusi la kujenga bomba la awamu ya pili la gesi maarufu kama NORD STREAM II, ambalo lingelisha gesi Ulaya yote kwa 90% tofauti na sasa mbapo Ulaya inategemea gesi ya Urusi kwa 40% tu, Marekani ameitumia Ukraine kukwamisha mradi huu na baadhi ya nchi za Nato. Kitendo hiki ilikuwa ni uchokozi wa kiuchumi na kijasusi, Jibu la Urusi limeanzia kwa Ukraine kwanza.

Hoja ya kwanza na ya tatu hazijaguswa na yeyote na nikama vile hawaoni kama ni sababu ama laaa, Lakini wako watu wachache wamejaribu kujibu kwakudonoa hoja moja tua hasa ile ya pili ndio imerudiwarudiwa kujibiwa lakini kwa majibu mepesa yanayotafsiri kwamba wengi hawaelewi dhana ya dunia na nguvu zake ama kijasusi huitwa Ushawishi wa Nchi, Na wako wengine waliweka msimamo tu wakupinga vita bila kueleza sababu, hawa dhana yao inalalia kwenye hoja ya pili pia bila kuwa na vuungo vya hoja.

Katika kuifafanua hoja ya pili na kuikazia hoja yangu ya kwanini naunga mkono Urusi. Naomba niseme kwamba, Dunia inawatu wanaotwa Wafanyamaamuzi, na kuna anaoitwa Watekelezaji wa maamuzi. Yaani kuna Super power countries, Karne ya 19 mkubwa duniani (Super power) alikuwa ni Urusi (Soviet Union), huyu aliamua mwelekeo wa dunia hadi alipoanguka 1989. Pamoja na kwamba Marekani alikuwepo na nguvu, lakini dunia ilikuwa na balance ya nguvu za kimagharibi na Mashariki.

Sijui kama watu wanakumbuka tukio la Cuban missile crisis USSR la October - November 1962, Soviet katika kilele cha nguvu zake na ubabe duniani waliweka makombora (missile) Cuba, kama eneo muhimu la kueneza Ujamaa Amerika ya Kusini na Kaskazini pia, Marekani walipofahamu tu jambo hili, ukaibuka mvutano mkubwa duniani uliohatarisha vita kuu ya pili duniani, Marekani walikizunguka Kisiwa cha Cuba kwa Meli na ndege kwa mwezi mzika, na mwisho makombora hayo yaliondolewa na Russia baada ya majadiliano ya mezani kama wakubwa sio vinginevyo. Marekani walionao ni hatari kwa usalama wao Soviet kuweka kituo chao cha Kijeshi Cuba, Tambua Cuba ilikuwa nchi huru kama Ukraine, yaani Cuba ileile ya mjamaa halisi Fedel Castro ambae alikuwa ni adui mkubwa wa Marekani hadi kufa kwake. Sasa anayeamini kuna uhuru wa nchi mbele ya Super power countries huyo bado ni mtoto duniani, akae kitako tuendelee kumfundisha kwamba uhuru unaojadiliwa na kusimuliwa ni ule wa kisiasa wa ndani tu wa vyama vya siasa na wa kuzungumza, nje ya hapo dunia ya tatu haiko huru na haitakuwa huru. Uhuru ni dhana pana sana. Haihusiani na Maslahi ya nchi kwa Marekani, Urusi na Uchina japo uchina bado hajajikomboa kufika viwango vya hawa wawili.

Sasa karne ya 21 Maslahi ya Urusi yanaguswa, Russia nae ana haki hiyo dhidi ya Ukraine. Uhuru wa nchi zote za mlengo wa kushoto unategemea msimamo wa Moscow, Hilo upende au usipende ndivyo dunia ilivyo. Vile vile Uhuru wa Nchi zenye mlengo wa Kulia unategemea msimamo wa Washington. Sera ya mambo ya nje ya Marekani ni muhimu na hutazamwa ndio eneo la usalama wa Marekani, Vivyo hivyo Sera ya Mambo ya nchi ya Urusi hii mpya chini ya Waziri shupavu Sergio Lavrov inalindwa kwa wino mwekundu kabisa kwakuwa ndio roho ya Kremlin.

Pengini watu hawajafahamu msingi wa India ambayo ni nchi muhimu sana kwa Urusi katika kuishinda Marekani kwenye vita vya ushawishi duniani kitendo cha kutochagua upande, na kwake ina maana kubwa sana katika geopolitics autonomy. India ni mteja mkubwa wa silaha za Urusi na ndege binsfsi. Hayuko tayari kupoteza fursa hiyo.

Nchi muhimu kwa USA za Israel, Saudia Arabia, UAE licha ya kuombwa kukemea operesheni ya kijeshi hadharani zimeamua kutochagua upande ni jambo tofauti kabisa na matarajio ya Marekani, sawa kabisa na nchi yangu ya Tanzania isiyofungamana na upande wowote.

Wako waliokosa hoja za kuipinga Urusi, badala yake wanabeza kwakusema kwanini hadi leo siku ya 15 bado tu Urusi haijateka mji mkuu Kyiv? Kwamba hii inaonyesha Urusi ali underrate vita hii, na kwamba Urusi ameshindwa vita. Binafsi naomba niwajibu hawa ndugu, Kama tutakubaliana kwa imani yangu ya Mizimu toka Mbutu Block E, Kigamboni niwakumbushe tu kwamba, Russia alilivamia Afghastan mwaka 1979 na kuondoka 1989, yaani aliikalia Afghanistan kimabavu kwa miaka 10 na alifanya hivyo baada ya Marekani Mjomba wake NATO kujaribu kuingilia vita kwakufadhili makundi ya ya Taliban ambayo makundi hayohayo baadae Marekani huyohuyo akatutangazia kuwa ni makundi ya Kigaidi.

Watu hawa wanaoipinga Urusi wanaenda mbali wanasema Marekani alivamia Iraq kwa siku chache tu akitokea Marekani, iweje Urusi iliyoko jirani na Ukraine inadhindwa kumaliza vita hadi leo? Majibu yangu kwao ni kwamba, Vita vya Marekani na Iraq vilipiganwa kutokea nchi vibaraka za Kuweit (669.9 km hadi mji mkuu Baghdad), Afghanistan (2,156 km hadi mji mkuu Baghdad) na Pakstan ( 2551 km hadi Baghdad). Havikupiganwa tokea moja kwa moja Marekani.

Vita vya Urusi na Ukraine vinapiganwa tokea Cremia (2,098.7 km hadi mji mkuu Kyiv), Donetsk (722.7 km hadi mji mkuu Kyiv) Luhansk (831.3 km hadi mji mkuu Kyiv) na Belarus (496.4 km hadi mji mkuu Kyiv). Izingatiwe na ieleweke kwamba, Marekani katika vita vya Uvamizi wake Iraq alikuwa na Ushirika wa Uingereza iliyovamia kutokea jiji la Basra, Ujerumani, Ufaransa, Australia, na ndugu wengine wa NATO. Lakini iliwachukua siku 23 hadi kuuteka mji mkuu Baghdad.

Je Urusi yuko na nani vitani, halafu hajapeleka jeshi lake halisi la Red Amy, anatumia majeshi ya nchi mpya zilizojitenga kama Cremia, Donetsk, Luhansk, Chechnia na wale Mercenary wa kirusi waitwao Wagner Group. Kuna majenerali wachache toka Vikosi maalumu Urusi wanaoongoza oparesheni lakini jeshi rasmi la Urusi liko standby kusubiri USA au NATO atie pua, Kilichomuondoa duniani Hitler watakiona live. Vita hivi vitaisha Urusi na Marekani wakikaa chini na kukubaliana yaani mazungumzo ya amani na si vinginevyo

Bado unasubiri nini?

Soma vitabu (Soft copy) vya Yericko Nyerere kwa 5,000/= tu kwa wiki kupitia App bora kabisa ya Vitabu Tanzania. Pakua sasa jisajili lipia wiki, mwezi au mwaka ujisomee vitabu vyote kupitia Play store Link 👉👉👉Yericko Nyerere App - Apps on Google Play

View attachment 2152327
Sababu ya KWANZA imekaa kimpropaganda sana,yaani DOMBASS region iko under Russian influence toka mwaka 2014,that means Russian inteligency wana operate kule since 2014,leo uje utuambie kuna genocide ilifanyika huko Donetsky na Luhansky halafu hakuna hata picha au video inayoonyesha hayo mauaji ya halaiki yakifanyika eti sababu tu Putin amesema bila hata ushahidi hata mmoja basi anafaa kuaminiwa.
Kingine yale majimbo kujitenga ni kama treasonous ACT na lazima taifa lolote lile litumie nguvu yoyote kuhakikisha wanayarudisha majimbo hayo,so nguvu waliotumia Ukraine sina shida nayo sababu hata Urusi mwaka 2008 aliivamia Georgia na kufanya massacre sababu tu walionyesha interest za kutaka kuegemea west ile haikuwa genocide sio?vipi chenchen war haikuwa genocide pia?,Yaani mnataka kutuaminisha kwamba Ukraine hakutakiwa kuonyesha effort yoyote kuyarudisha majimbo yake yanayotaka kujitenga?,
Yaaani sababu wanazungumza kirusi basi hawakutaka kuguswa?,Leo west Ukrainians wanakuwa slaughtered na Russian cruise missiles sbabu tu hawataki kuegemea upande wa urusi,kwa iyo unataka kutuaminisha hiki anachofanya Urusi ni sawa ila Ukraine kupigana na waasi kule DOMBASS kuirejesha miji iliojiyenga kinyemela basi amefanya Genocide?..
Tusimezeshane propaganda aisee
 
Mtu anaandika kuwa Putin anataka kuwamaliza wote wasio wa Russia.
Hivi hili nalo linahitaji ushahidi, kuwa ni Uongo?
Hujiulizi kwa nini miji yote inayoongea kurusi Putin alifanya jitihata ikajitenga kwanza ndio wakaanza kuivamia Ukraine?,Kwa nini walipoanza vita waliingiza majeshi kwanza ile miji inayoongea kirusi kuilinda kwanza kabla ya kuanza kurusha Cruise missiles Kyiv na Kharkiv??
 
Hujiulizi kwa nini miji yote inayoongea kurusi Putin alifanya jitihata ikajitenga kwanza ndio wakaanza kuivamia Ukraine?,Kwa nini walipoanza vita waliingiza majeshi kwanza ile miji inayoongea kirusi kuilinda kwanza kabla ya kuanza kurusha Cruise missiles Kyiv na Kharkiv??
Aseee hapo si ndio kulikuwa na mapambano miaka yote 8?
Ulitaka waanzie wapi mjomba?
Anataka kuwamaliza wote na Anaruhusu humanitarian corridor?
 
Taifa linaundwa na raia, hakuna taifa bila raia. Iwapo unatofutisha usalama wa Taisa na Usalama wa raia basi unaishi nchi ya kufikirika kabisa. Kwa nini asiogope usalama wa taifa kutokea Alsaka au kwenye bahari ya pacific ambako marekani amejaza manuwari za kivita na Aircraft carriers kibao.
Mbona USA mwenyewe aliogopa kambi ya jeshi la Russia pale Cuba na alimwomba Russia itoe ngome yao na Russia ilikubali kutoa bila mtimanyongo, sasa kwanini iwe nongwa kwa Russia inapoamua kufanya hivyo sawa na USA ilivyofanyaga kwa Cuba?

Je USA ilikuwa na uhalali gani wa kuua Raia wa Libya, Yemen, Afghanistan, Iraq, Syria na Vietnam ikiwa inapenda amani?
 
Nawaoneaga huruma sana watu wanaosoma vitabu vya yeriko nyerere ni wanapoteza mda wao, kwenye vitabu vyake anaelezea mambo ya ujasusi laki in reality ana support udikteta mim kusoma vilivyoandikwa na author sababu hawaamin walichoandika
Rasilimali, mazao ya shambani yako wewe, kwanini upangiwe bei na mnunuaji tena kwa masharti magumu sana kama ilivyo kwa Barrick company?

Huo si udikteta?
 
Wao kama Ukraine ni nchi yenye katiba yake na taratibu zake; Urusi wao pia wana katiba yao na taratibu zao. Inakuwaje Urusi iipangie Ukraine namna ya kujiendesha?
Mbona USA inazipangia nchi zingine zisitengeneze mabomu ya nyuklia kama Iraq na North Korea nakati yenyewe inatengeneza mabomu hayo hayo, inamaana Iraq na Korea Kaskazini si nchi huru kama USA?
 
Mleta uzi alichofanya ni kuamua kua tofauti na mitazamo ya walio wengi, anajua kabisa hoja anazoleta zina maelezo zaidi ya hayo aliyoyatoa ila amestick na maelezo haya.

Kazi ni kwetu kuchambua
 
Naomba kueleweshwa, hivi CIA walivurugaje dili la warusi kujenga bomba la pili la gesi Ulaya
USA ana wivu wa kitoto sana, aliona Russia itaenda kuuza gesi na mafuta Ulaya zaidi ya 90% tofauti na sasa inavyouza kwa 40%, akaona isiwe tabu ni heri tu ivuruge huo mradi maana Russia itaenda kuinuka zaidi kiuchumi duniani.
 
Aseee hapo si ndio kulikuwa na mapambano miaka yote 8?
Ulitaka waanzie wapi mjomba?
Anataka kuwamaliza wote na Anaruhusu humanitarian corridor?
Hujajibu swali,unahisi ni kwa nini Putin alifanya hujuma kwanza miji inayoongea kirusi ijitenge kwanza ndio aanze michakato wa kuivamia Ukraine?..
Humanitarian corridor ni makubaliano ya pande zote mbili,hata hivyo Urusi amekuwa akikiuka makubaliano ya humanitarian Corridor haya kabla muda haijaisha,Kule Mariupol mji wite umakuwa magofu,waliweka ceasefire angalau watu wapate maji,Russia few hours wakaanza bombardment.
 
Mbona USA inazipangia nchi zingine zisitengeneze mabomu ya nyuklia kama Iraq na North Korea nakati yenyewe inatengeneza mabomu hayo hayo, inamaana Iraq na Korea Kaskazini si nchi huru kama USA?
Huo ndio ubishi unaotokana na maneno ya mtaani bila kuelewa facts.

Sikiliza: Swala la utenegenzaji wa mabomu ya Nuclear ni la Umoja wa Mataifa- Nuclear Non Proliferation. Marekani inachofanya kujaribu kulisimamia agizo hilo la umoja wa mataifa. Katika kufanya hivyoa huwa inashirikiana na nchi nyingine, siyo kuwa inatoa amri ya peke yake tu. Kwa mfano hilo la Iran limekuwa linasimamiwa pamoja na Urusi, China na nchi nyingine za Ulaya pamoja na Umoja wa mataifa wenyewe; halafu lile na North Korea pia inashirikiana na urusi na China pamoja na umoja wa mataifa.

Jifunze kuwa informed ili uwezea kuwa unatoa hoja za uhakika.
 
Huo ndio ubishi unaotokana na maneno ya mtaani bila kuelewa facts.

Sikiliza: Swala la utenegenzaji wa mabomu ya Nuclear ni la Umoja wa Mataifa- Nuclear Non Proliferation. Marekani inachofanya kujaribu kulisimamia agizo hilo la umoja wa mataifa. Katika kufanya hivyoa huwa inashirikiana na nchi nyingine, siyo kuwa inatoa amri ya peke yake tu. Kwa mfano hilo la Iran limekuwa linasimamiwa pamoja na Urusi, China na nchi nyingine za Ulaya pamoja na Umoja wa mataifa wenyewe; halafu lile na North Korea pia inashirikiana na urusi na China pamoja na umoja wa mataifa.

Jifunze kuwa informed ili uwezea kuwa unatoa hoja za uhakika.
Hujui chochote kuhusu UN kaka, unafahamu sera ya VETO POWER katika UN?

Nchi yako TZ ina nafasi gani kimaamuzi ndani ya mipango ya UN zaidi tu ya kuwa mtazamaji ikiwa kuna usawa kuhusu maswala ya mabomu ya nyuklia?

Ondoa mihemuko utumie upeo halisi ili utambue USA na EU ni mashetani wanaokuchekea kwa nnje lakini kiuhalisia hawana hata chembe ya democracy unayoiwaza kiundani zaidi ya Neo-Colonialism ili Mwafrika unyonywe vizuri rasilimali zako na uendelee kuwa mtumwa milele yote.
 
Hujui chochote kuhusu UN kaka, unafahamu sera ya VETO POWER katika UN?

Nchi yako TZ ina nafasi gani kimaamuzi ndani ya mipango ya UN zaidi tu ya kuwa mtazamaji ikiwa kuna usawa kuhusu maswala ya mabomu ya nyuklia?

Ondoa mihemuko utumie upeo halisi ili utambue USA na EU ni mashetani wanaokuchekea kwa nnje lakini kiuhalisia hawana hata chembe ya democracy unayoiwaza kiundani zaidi ya Neo-Colonialism ili Mwafrika unyonywe vizuri rasilimali zako na uendelee kuwa mtumwa milele yote.
Nimekuwapo hapa JF kwa muda mrefu sana, takriban miaka 16 sasa hivi. Watu wasiojua wanaloongea huanza post zao kwa kubisha na kutukana kisha kuuliza maswali badala ya kujibu hota. Haya sasa nikukubalie kuwa mimi sijui chochote na pia sijua veto power maana yake; nimekubali.j Je hayo mawili ya mimi kutojua chochote na kutojua veto power yanakupa faraja gani katika kuelewa ukweli kuwa swala na Nuclear non-proliferation ni la umoja wa mataifa.

Mambo mengine yote uliyandika ni pumba tu zisizojibu chochote. yaani maneno ya vichochoroni tu.
 
Nimekuwapo hapa JF kwa muda mrefu sana, takriban miaka 16 sasa hivi. Watu wasiojua wanaloongea huanza post zao kwa kubisha na kutukana kisha kuuliza maswali badala ya kujibu hota. Haya sasa nikukubalie kuwa mimi sijui chochote na pia sijua veto power maana yake; nimekubali.j Je hayo mawili ya mimi kutojua chochote na kutojua veto power yanakupa faraja gani katika kuelewa ukweli kuwa swala na Nuclear non-proliferation ni la umoja wa mataifa.

Mambo mengine yote uliyandika ni pumba tu zisizojibu chochote. yaani maneno ya vichochoroni tu.
Ushakiri hujui chochote, kaa kimya.
 
Kuna makosa natika perspectives zako, yaani unatoa tafsiri zisizo za kweli. Miaka ya nyuma kidogo wakati wa Kikwete, Marekani ilitaka kufungua ofisi yake ya Africa Command hapa Tanzania kwa vile sasa hivi iko ujerumani ambako ni mbali sana na Africa. Tanzania ilikataa, na wala hawakutumia nguvu kutulazimisha tukubali ingawa wangeweza kufanya hivyo kwa mabavu kama haya ya urusi.

Cuba haijawahi kuzuiliwa kuwa mshirka wa Urusi, in fact maisha ya cuba yamekuwa yanaitegemea urusi miaka yote. Walizuiwa kutumika kama kituo cha kijeshi cha urusi, lakini siyo kuwa na urafiki na urusi.

China na Taiwani kuna mgororo wa kihistoria baina ya Chiang Kai Shek na Mao ambao bila kuuelewa umekimbilia kwenye false conclusions
Aisee soma tena ulichoandika. Unapinga kisha unakubali kitu kilekile....🤣🤣🤣
 
Ukraine watasoma na kukujibu. Sisi Watanzania tuko bize kutafuta chakula na karo za watoto. Wee endelea na kuandika kurasa za magazeti.
Na yeye ndiyo anaingiza kipato hivyo kupitia kalamu yake! Unaweza kuta anaingiza mara kumi yako! Aliye busy kusaka shilingi wala asinge comment kama ulivyo fanya wewe! Pole.
 
Back
Top Bottom