Naendelea kuunga mkono Urusi; Hoja zangu hazijajibiwa

Mkuu Yericko Nyerere, Colonel Douglas Macgregor, afisa mstaafu wa jeshi la Marekani, pia anakusapoti hiyo sababubu yako ya pili.

Colonel Douglas Macgregor anasema kuwa Marekani ina nafasi ya kuepusha vita na Putin (Russia). Jambo la kwanza wanalopaswa kufanya Wamarekani ni kukiri na kukubaliana na nukta ya msingi ya Putin (Russia), ambayo serekali ya Russia imeiweka wazi kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Nukta yenyewe ni kuwa Russia hawataki majeshi ya Marekani, mizinga ya Marekani, na majeshi ya NATO kwenye mpaka wake na Ukraine (Mashariki ya Ukraine kwenye majimbo yaliyotangazwa huru na Putin).

Colonel Douglas akaendelea kusema: Kiukweli kabisa hata sisi Wamarekani hatukuyataka majeshi ya Russia na mizinga yake ndani ya Cuba (mwaka 1962), Putin naye hataki mambo hayo mashariki mwa Ukraine. Lazima tukubali madai hayo. Tuache kujifanyisha kuwa madai hayo hayana maana (ni ya kipuuzi).


===


COL. DOUGLAS MACGREGOR: Let me just reiterate something. I, like you and millions of Americans, would prefer that the troops headed to Eastern Europe right now were headed to the Mexican border. But I’m also very concerned that we find a way to avoid a conflict with Russia. The first thing we have to do is acknowledge that Putin’s basic point, not just his point, the Russian government’s point, which they’ve made for 25 years, is valid. They don’t want U.S. forces and missiles and NATO troops immediately across the border in eastern Ukraine. Absolutely. We didn’t want them in Cuba, he doesn’t want them in eastern Ukraine. We should acknowledge that. Stop pretending it’s a nonissue. It is a major issue for them. Let’s acknowledge it and then let’s get down to business and tell them fine, our concern at this point is we don’t want you to proceed west towards the polish border over the Dnieper River in Ukraine.
 
When Kichuguu speaks you have to sit down and take some notes.
 
Anaemwambia Kichuguu hajui chochote kuhusu usalama wa raia ndiyo huyu anaetoa hizi hoja hapa 😀😀
 
Ilikuwaje hadi ukashawishika kununua hicho ki pamphlet cha blah bla zake huyu.
 
Soma Alichokiandika....
Je inakaribia hata robo ya Ukweli?
Bado unarudia kile kile ninachokukatalia,wewe weka ukweli wako ukiniambia nirudie kusoma alichoandika mimi nitakwambia yupo sahihi.Wewe unaempinga ndiyo uthibitishe na siyo kuja na vijineno viwili na unataka tukuamini.
 
Bado unarudia kile kile ninachokukatalia,wewe weka ukweli wako ukiniambia nirudie kusoma alichoandika mimi nitakwambia yupo sahihi.Wewe unaempinga ndiyo uthibitishe na siyo kuja na vijineno viwili na unataka tukuamini.
Mtu anaandika kuwa Putin anataka kuwamaliza wote wasio wa Russia.
Hivi hili nalo linahitaji ushahidi, kuwa ni Uongo?
 
Vipya Libya mkuu.. USA alivyo sababisha ubaribu mkubwa, kupoteza uhai na hadi libya unayo iona leo.. rudi pale Iraq.. na maeneo mengine.. mwisho wa siku haya mataifa yanalinda interest zao..
 
haya mambo tuliyajadiri enzi hizo na ndugu yangu MALCOM LUMUMBA 😀
 
Wao kama Ukraine ni nchi yenye katiba yake na taratibu zake; Urusi wao pia wana katiba yao na taratibu zao. Inakuwaje Urusi iipangie Ukraine namna ya kujiendesha?
Katika ufafanuzi nimeeleza uhuru wa nchi unaoufikiri upo ni wa bendera tu mbele ya mataifa makubwa... Jiulize kwanini Taiwani inazuiwa na China kuwa mshirika wa USA? Kwanini Cuba ilizuiwa na USA kuwa mshirika wa Urusi? Ukiyajua hayo hautahoji hilo tena
 
Vipya Libya mkuu.. USA alivyo sababisha ubaribu mkubwa, kupoteza uhai na hadi libya unayo iona leo.. rudi pale Iraq.. na maeneo mengine.. mwisho wa siku haya mataifa yanalinda interest zao..
Siyo kweli. Marekani hakusababisha uharibifu huo; uharibifu ulisababishwa na walibya wenyewe walipoiga kufanya mapinduzi kama ya Tunisia. Marekani lisaidia upande mmoja wa mgogoro lakini siyo kuwa ilitangaza vita na Libya na kuiweka masharti ya kufanya. Hali ilikuwa vivyo hivyo kwa Misri na Syria, vurugu zilianzishwa na raia wenyewe.
 
Ngumbaru kabisa wewe nilikuwa nahisi unazo za kichwani kumbe ni shabiki tu.
Ndio maana likitabu lako haliuziki miaka nenda rudi utasoma na wanao
Nimekuja fasta nione kama UNAMJIBU jamaa kumbe nimeambulia matusi tu; hebu fafanua, elimu bora tutaipata kwa kua na mawazo kinzani. Toa hayo madini bhana
 
Daa, simfahamu Yerico, sijawahi kusoma kitabu chake hata kimoja but michango yenu sometimes ndio mnamfanya aonekane Yerico ana akili; hivi ni kweli unashangaa Urusi kuua watu Ukraine halafu haushangai vita zingine zinazo endelea mashariki ya kati? Libya vipi? Iraq je??? Anyway but pia unaunga mkono mauaji aliokua akiyafanya rais wa sasa wa Ukraine ila hupendezwi na mauaji ya sasa ya Warusi huko Ukraine? Kumbuka vyote jamaa kaviandika humu; i thought, kama kweli hupendi mauaji then ungemlaani hata huyu rais wa sasa wa Ukraine kuua raia waliokua hawamuungi mkono, ungeandika pia kutopendezwa kwako na mauaji yanayo endelea sehemu zingine kama Syria, Iraq, Afghanistan, Libra to date hakujatulia etc. Mwishoni ningefurahi kama ningesikia UKIPINGA utengenezaji wa silaha za kisasa unaoendelea duniani kote, hapa ungelaani USA, Urusi, Korea ya kaskazini, China nk. I think umejificha kwenye mauaji yanaeyo endelea lakini chuki yako halisi ipo kwa Urusi, sio mauaji
 
Kuna makosa natika perspectives zako, yaani unatoa tafsiri zisizo za kweli. Miaka ya nyuma kidogo wakati wa Kikwete, Marekani ilitaka kufungua ofisi yake ya Africa Command hapa Tanzania kwa vile sasa hivi iko ujerumani ambako ni mbali sana na Africa. Tanzania ilikataa, na wala hawakutumia nguvu kutulazimisha tukubali ingawa wangeweza kufanya hivyo kwa mabavu kama haya ya urusi.

Cuba haijawahi kuzuiliwa kuwa mshirka wa Urusi, in fact maisha ya cuba yamekuwa yanaitegemea urusi miaka yote. Walizuiwa kutumika kama kituo cha kijeshi cha urusi, lakini siyo kuwa na urafiki na urusi.

China na Taiwani kuna mgororo wa kihistoria baina ya Chiang Kai Shek na Mao ambao bila kuuelewa umekimbilia kwenye false conclusions
 
Mkuu rudia vizuri ya Libya.. but mwisho wa siku mataifa makubwa yote yanalinda interest zao. na yapo tayari hata kuua.. na kuangamiza..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…