Naendelea kuunga mkono Urusi; Hoja zangu hazijajibiwa

Nakupongeza sana Mkuu Yerico,
Umeandika ukweli mtu,Hali halisi na mambo mazito sana.
Umeandika hoja zilizojaa uhalisia na hoja zilizoshiba.

Ila kitu kimoja ,watu wote wanaokupinga hayo uliyoyaandika Yako juu ya uwezo wao kuyaelewa..
 
Mtu anaandika kuwa Putin anataka kuwamaliza wote wasio wa Russia.
Hivi hili nalo linahitaji ushahidi, kuwa ni Uongo?
Tuishie hapa naona hatuwezi kuelewana kabisa.Nilitegemea utuwekee ukweli uliojitosheleza badala yake unakuja na vijimaswali juu ya maswali,sasa unataka nikujibu nini wakati wewe ndiyo unapaswa utetee hoja yako.
 
VLADMIR PUTIN NI SHETANI MWENYE FORM YA BINADAM.
 
Sababu ya KWANZA imekaa kimpropaganda sana,yaani DOMBASS region iko under Russian influence toka mwaka 2014,that means Russian inteligency wana operate kule since 2014,leo uje utuambie kuna genocide ilifanyika huko Donetsky na Luhansky halafu hakuna hata picha au video inayoonyesha hayo mauaji ya halaiki yakifanyika eti sababu tu Putin amesema bila hata ushahidi hata mmoja basi anafaa kuaminiwa.
Kingine yale majimbo kujitenga ni kama treasonous ACT na lazima taifa lolote lile litumie nguvu yoyote kuhakikisha wanayarudisha majimbo hayo,so nguvu waliotumia Ukraine sina shida nayo sababu hata Urusi mwaka 2008 aliivamia Georgia na kufanya massacre sababu tu walionyesha interest za kutaka kuegemea west ile haikuwa genocide sio?vipi chenchen war haikuwa genocide pia?,Yaani mnataka kutuaminisha kwamba Ukraine hakutakiwa kuonyesha effort yoyote kuyarudisha majimbo yake yanayotaka kujitenga?,
Yaaani sababu wanazungumza kirusi basi hawakutaka kuguswa?,Leo west Ukrainians wanakuwa slaughtered na Russian cruise missiles sbabu tu hawataki kuegemea upande wa urusi,kwa iyo unataka kutuaminisha hiki anachofanya Urusi ni sawa ila Ukraine kupigana na waasi kule DOMBASS kuirejesha miji iliojiyenga kinyemela basi amefanya Genocide?..
Tusimezeshane propaganda aisee
 
Mtu anaandika kuwa Putin anataka kuwamaliza wote wasio wa Russia.
Hivi hili nalo linahitaji ushahidi, kuwa ni Uongo?
Hujiulizi kwa nini miji yote inayoongea kurusi Putin alifanya jitihata ikajitenga kwanza ndio wakaanza kuivamia Ukraine?,Kwa nini walipoanza vita waliingiza majeshi kwanza ile miji inayoongea kirusi kuilinda kwanza kabla ya kuanza kurusha Cruise missiles Kyiv na Kharkiv??
 
Aseee hapo si ndio kulikuwa na mapambano miaka yote 8?
Ulitaka waanzie wapi mjomba?
Anataka kuwamaliza wote na Anaruhusu humanitarian corridor?
 
Mbona USA mwenyewe aliogopa kambi ya jeshi la Russia pale Cuba na alimwomba Russia itoe ngome yao na Russia ilikubali kutoa bila mtimanyongo, sasa kwanini iwe nongwa kwa Russia inapoamua kufanya hivyo sawa na USA ilivyofanyaga kwa Cuba?

Je USA ilikuwa na uhalali gani wa kuua Raia wa Libya, Yemen, Afghanistan, Iraq, Syria na Vietnam ikiwa inapenda amani?
 
Nawaoneaga huruma sana watu wanaosoma vitabu vya yeriko nyerere ni wanapoteza mda wao, kwenye vitabu vyake anaelezea mambo ya ujasusi laki in reality ana support udikteta mim kusoma vilivyoandikwa na author sababu hawaamin walichoandika
Rasilimali, mazao ya shambani yako wewe, kwanini upangiwe bei na mnunuaji tena kwa masharti magumu sana kama ilivyo kwa Barrick company?

Huo si udikteta?
 
Wao kama Ukraine ni nchi yenye katiba yake na taratibu zake; Urusi wao pia wana katiba yao na taratibu zao. Inakuwaje Urusi iipangie Ukraine namna ya kujiendesha?
Mbona USA inazipangia nchi zingine zisitengeneze mabomu ya nyuklia kama Iraq na North Korea nakati yenyewe inatengeneza mabomu hayo hayo, inamaana Iraq na Korea Kaskazini si nchi huru kama USA?
 
Mleta uzi alichofanya ni kuamua kua tofauti na mitazamo ya walio wengi, anajua kabisa hoja anazoleta zina maelezo zaidi ya hayo aliyoyatoa ila amestick na maelezo haya.

Kazi ni kwetu kuchambua
 
Naomba kueleweshwa, hivi CIA walivurugaje dili la warusi kujenga bomba la pili la gesi Ulaya
USA ana wivu wa kitoto sana, aliona Russia itaenda kuuza gesi na mafuta Ulaya zaidi ya 90% tofauti na sasa inavyouza kwa 40%, akaona isiwe tabu ni heri tu ivuruge huo mradi maana Russia itaenda kuinuka zaidi kiuchumi duniani.
 
Aseee hapo si ndio kulikuwa na mapambano miaka yote 8?
Ulitaka waanzie wapi mjomba?
Anataka kuwamaliza wote na Anaruhusu humanitarian corridor?
Hujajibu swali,unahisi ni kwa nini Putin alifanya hujuma kwanza miji inayoongea kirusi ijitenge kwanza ndio aanze michakato wa kuivamia Ukraine?..
Humanitarian corridor ni makubaliano ya pande zote mbili,hata hivyo Urusi amekuwa akikiuka makubaliano ya humanitarian Corridor haya kabla muda haijaisha,Kule Mariupol mji wite umakuwa magofu,waliweka ceasefire angalau watu wapate maji,Russia few hours wakaanza bombardment.
 
Mbona USA inazipangia nchi zingine zisitengeneze mabomu ya nyuklia kama Iraq na North Korea nakati yenyewe inatengeneza mabomu hayo hayo, inamaana Iraq na Korea Kaskazini si nchi huru kama USA?
Huo ndio ubishi unaotokana na maneno ya mtaani bila kuelewa facts.

Sikiliza: Swala la utenegenzaji wa mabomu ya Nuclear ni la Umoja wa Mataifa- Nuclear Non Proliferation. Marekani inachofanya kujaribu kulisimamia agizo hilo la umoja wa mataifa. Katika kufanya hivyoa huwa inashirikiana na nchi nyingine, siyo kuwa inatoa amri ya peke yake tu. Kwa mfano hilo la Iran limekuwa linasimamiwa pamoja na Urusi, China na nchi nyingine za Ulaya pamoja na Umoja wa mataifa wenyewe; halafu lile na North Korea pia inashirikiana na urusi na China pamoja na umoja wa mataifa.

Jifunze kuwa informed ili uwezea kuwa unatoa hoja za uhakika.
 
Hujui chochote kuhusu UN kaka, unafahamu sera ya VETO POWER katika UN?

Nchi yako TZ ina nafasi gani kimaamuzi ndani ya mipango ya UN zaidi tu ya kuwa mtazamaji ikiwa kuna usawa kuhusu maswala ya mabomu ya nyuklia?

Ondoa mihemuko utumie upeo halisi ili utambue USA na EU ni mashetani wanaokuchekea kwa nnje lakini kiuhalisia hawana hata chembe ya democracy unayoiwaza kiundani zaidi ya Neo-Colonialism ili Mwafrika unyonywe vizuri rasilimali zako na uendelee kuwa mtumwa milele yote.
 
Nimekuwapo hapa JF kwa muda mrefu sana, takriban miaka 16 sasa hivi. Watu wasiojua wanaloongea huanza post zao kwa kubisha na kutukana kisha kuuliza maswali badala ya kujibu hota. Haya sasa nikukubalie kuwa mimi sijui chochote na pia sijua veto power maana yake; nimekubali.j Je hayo mawili ya mimi kutojua chochote na kutojua veto power yanakupa faraja gani katika kuelewa ukweli kuwa swala na Nuclear non-proliferation ni la umoja wa mataifa.

Mambo mengine yote uliyandika ni pumba tu zisizojibu chochote. yaani maneno ya vichochoroni tu.
 
Ushakiri hujui chochote, kaa kimya.
 
Aisee soma tena ulichoandika. Unapinga kisha unakubali kitu kilekile....🤣🤣🤣
 
Ukraine watasoma na kukujibu. Sisi Watanzania tuko bize kutafuta chakula na karo za watoto. Wee endelea na kuandika kurasa za magazeti.
Na yeye ndiyo anaingiza kipato hivyo kupitia kalamu yake! Unaweza kuta anaingiza mara kumi yako! Aliye busy kusaka shilingi wala asinge comment kama ulivyo fanya wewe! Pole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…