Nafanya kazi lakini nahisi kama nimeshafukuzwa

Nafanya kazi lakini nahisi kama nimeshafukuzwa

MBUZI MWENYE BUSARA

Senior Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
143
Reaction score
160
Habari Wana jukwaa?

Kampuni ninayofanyia kazi nina miaka mitano kasoro Sasa. Wakati naanza kazi kulikuwa hakuna hesabu. Iliyowahi kufungwa maana kazi yangu ni ya kihasibu. Nimepambana kwasasa kuna hesabu zilizokaguliwa za miaka sita.

Mwanzoni tulikubaliana salari kiasi kwa maelewano kwamba nitaongezewa. Lakini baada ya pale kazi zimekuwa nyingi lakini Boss akagoma kabisa kuongeza.
Nilipoona kazi zinanizidi na mshahara ni mdogo nikamwambia aniongezee mtu mmoja. Akamamleta mtu akampa mshahara Mara mbili ya mshahara wangu lakini jamaa hakuwa na muda maana anachelewa kufika kazini au akaamua haji ndani ya wiki anaweza kuja Mara tatu au mbili hivyo kazi ikawa bado inaniangalia Mimi tu na jamaa kila akija ni mgeni hajui kinachoendelea. Sikutaka hata kumsemea kwa Boss niliendelea kukomaa na hali yangu.

Mwajiri akaamua kumwajiri mzee mmoja rafiki yake akamlipa Mara tatu ya mshahara wangu na nyumba akampa lakini Mimi Wala hataki kuniongezea hivyo nikawa namuelekeza huyu mzee ambaye kimsingi alipewa kuwa Boss wangu.

Ikapita muda akamwajiri mtu mwingine raia wa India akamlipa Mara 6 ya mshahara wangu, nyumba na gari.

Juzi tu akamwajiri mtu mwingine naye ni mzee akamlipa Mara mbili ya mshahara wangu!

Sasa tupo watano wao ni over 40 Mimi ni under 40 wote wananizidi mshahara lakini kila kitu wananitegemea Mimi niwaelekeze.

Wao wenyewe wananiambia nikosana nini na mwajiri mbona ananifanyia hivyo!

Kiukweli Mimi nimevunjika moyo kabisa na sielewi kinachoendelea na kwanini mwajiri ananifanyia hivyo!

Naona ule msemo usemao akufukuzae hakuambii toka.

Kweli natamani niondoke lakini nategemewa na familia ya mke na watoto kadhaa naona kuacha kazi kabla sijapata kazi naona nitaionea familia yangu.

Ebu wadau mniambie kwanza kisaikolojia huyu mwajiri ananipa ujumbe gani Mimi? Na bado kila kitu ananiambia nifanye yaani haoneshi kama hanitaki.

Pia nipeni ushauri niweze kufanya maamuzi sahihi! Please!!
 
Ni kweli kupata kazi ni kazi pale uachapo kazi.

-Vumilia mpaka utakapopata mbadala wake ili usibaki bilabila mjini.

-Kama una akiba ya kutosha(sidhani kama unayo)"rara mbere" ukajitafutie riziki sehemu salama na stress-free zone.

-yeye boss wako si Maanani wa kukupangia uwe kapuku mwenye sonona.
 
Ni kweli kupata kazi ni kazi pale uachapo kazi.
-Vumilia mpaka utakapopata mbadala wake ili usibaki bilabila mjini.
-Kama una akiba ya kutosha(sidhani kama unayo)"rara mbere" ukajitafutie riziki sehemu salama na stress-free zone.
-yeye boss wako si Maanani wa kukupangia uwe kapuku mwenye sonona.
Shukrani mkuu!
 
Vipi hizo kazi nyingine unazitafuta mkuu??
Tafuta ukipata, tingisha kiberiti kidogo ukiona anarespond tulia si ajabu akakulipa mara 7 zaidi ya hapo. Ila kama anakupotezea ni bora usepe tu.
 
Hakutaki hapo kazini..
Pole sana
 
Habari Wana jukwaa?

Kampuni ninayofanyia kazi nina miaka mitano kasoro Sasa. Wakati naanza kazi kulikuwa hakuna hesabu. Iliyowahi kufungwa maana kazi yangu ni ya kihasibu. Nimepambana kwasasa kuna hesabu zilizokaguliwa za miaka sita...
Kweli ajira utumwa, usiache, ila tafuta kazi kwa bidii I Sana Sana Sana!
 
Hakutaki hapo kazini..
Pole sana

Mkuu Mimi pia nawaza kama Wewe. Lakini naona kama treatment zake kwangu haioneshi maana juzi kati nilipata wazo fulani la kuandaa sehemu ya kuiweka familia yangu incase of loss of employment nikamuomba kamkopo akanipa japo kidogo lakini pia hakuniambia nianze marejesho lini!
 
Iyo sehemu sio salama kwa ustawi wanmaisha yako kazi Kama unaifanya ikiwa huna amani iyo sio kazi ni utumwa

Muhimu kwanza ujiulize unatka kuendelea kuajiriwa au kujiajiri ukipata jibu fanya maamuz riziki ni popote pale huwezi pia kubeba maji masafi ukiwa tayari unandoo ya maji machafu mkononi
 
Back
Top Bottom