Nafanya kazi lakini nahisi kama nimeshafukuzwa

Mkuu nakupata, Asante!
 
Kama hujawahi kuomba likizo Omba sasa kama ni ya mwezi au nusu mwezi. Kwenye likizo hiyo jaribu kufanya mambo yako kama kuomba kazi kwa nguvu na kuanzisha biashara ndogo ndogo. Iwe likizo kweli uwe mbali na ofisi. Itakusaidia akili yako kujua kuwa kunamaisha nje ya kampuni iyo. Yakibuma rudi kazini. Uwe unaomba likizo mkuu. Likizo ni muhimu kwa afya ya akili!
 
Shukrani mkuu.
 
Huu uzi ni utumbo wa bata.
 
A good dancer should know when to leave a stage, ukielewa tafakuri ya huo ujumbe itakua ndio mwisho wa mateso yako kazini. Kila la heri mkuu
 
Kama una familia anza kutafuta kazi sehemu nyingine hvyo vitu vya kawaida kwenye kazi yaani kwenye kampuni ukikosea tu kuingia ndo umekula kwako mambo ya chukua laki 2 halafu tutakuongezea nyingine baadae ukikubali tu imekula kwako.
 
Kweli shida zinatofautiana, pambana tu ndugu kuna watu wanatafuta iyo kazi unayonyanyasika usiku na mchana ilimrad wapate icho kidogo unachopata wewe.

Ushauri omba kazi sehem nyngne ndo uondoke hapo maana kwa experience yako ya miaka yote hiyo hutopata tabu sana kupata sehem nyngne
 
Amen mkuu.
 
As long umesema kwamba hao 40+ wote wanakutegemea wewe simple chukua likizo ya mwezi mzima automatic gape lako litaonekana

Then changamoto zitakazoonekana kwasababu ya wewe kutokuwepo ofsn ndio gape la ww kuomba salary increase

Akigoma hapo sasa maamuzi juu yako ubakie uendelee kuteseka ama usepe ukaanze upya
 
Ongeza elimu yako ili na wewe uwe masoko,unapakwenda kwakuwa Elimu yako ni ndogo.inaonyesha unatumia uzoefu ulionao kufanya hiyo kazi. Kwahiyo pamoja wigo wa ujuzi uliyo nao kwa kuongeza Elimu.Tafuta mda wa ziada nenda chuo ,kulalamika hakutakusaidia.
 
Duh! Pole sana mkuu. Hii hali inanitokea hata mimi.
 

Elimu yangu ni level ya degree ndio ni ndogo lakini kati ya hawa wengine wanne moja tu ana CPA waliobaki tupo level moja. Of course sina mpango wa kuendelea kusoma hadi uchumi ukae sawa.
 
Anza kutafuta kazi sehemu zingine, ukifanikisha hama.
 
Yalinikutaga kama yako sema tu mimi alikuwa ni mtu mmoja tu nilichofanya mimi ni kudeal na zile zangu tu kazi zao ctaki kabisa miezi sita akawatimua kabla hawajaondoka nikajifanyia kosa akaniachisha nikaenda ubalozini ni kamshtaki mpaka leo hanisahau yule fala nlijiongezea mshahara mara tatu akabaki mdomo wazi wenzangu nao wakajiunga na mimi tulimkomba zakitosha

NADHANI MPAKA HAPO USHAJUA NI KIPI UNAPASWA KUFANYA JIANGALIE WEWE
 
Daah wewe ni mimi kabisa. Yaani nimepiga kazi for almost six years sikuenda leave kutokana na unyeti wa kazi yenyewe. Ikifika annual leave yangu wanainunua fasta.
Sasa nikaja kupata maradhi nikalazwa hospitali kwa siku kumi sikua na mawasiliano nao kipindi niko hospitalini kutokana na matibabu nilikua natibiwa wao wakamleta mtu mwingine kutoka tawi jingine ni nimepona narudi kazini naambiwa ni handover kazi nizokua nazifanya. Sielewi ila kifupi hawa watu ni zaidi ya nyoka .
Naangalia taratibu wanipe barua yangu nifanye mambo mengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…