Nafanyaje kuwa pilot wa ndege?

Na wanao watapiga hesabu hizo hizo za kuwekeza. The circle goes on ...
 
Hapo utakuta ametafuta kimvuli ili apumzike na jua kali baada ya kuendesha Guta lake toka Mabibo mpaka Kariakoo,
Katika mapumziko yake hayo ndio akaamua achangie JF kidogo kabla ya kuwahisha mzigo kwa tajiri.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Daah sema mkuu una kumbukumbu sana aisee.
Sio mara ya kwanza kuona una refer uzi wa mtu ambaye kaja na mada nyingine πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Nakwendaga nayo papaa...
 
Mkuu ujawahi kujibu swali langu..
We ni pilot au aircraft eng..?
Mkuu sio pilot wala Aircraft Eng...nimefanya kazi kama saidia fundi kwenye meli kubwa kwa muda mrefu ila nilisoma Mechanics kwa level ya kawaida hapo Stellenbosch University...mimi pia nilikua natamani kusoma Urubani mwaka 1999 nililipa Ada ilikua rand 10,000 chuo kimoja hapo Pretoria baadae nikapata kazi nikaona bora nifanye kazi tu kuliko kusoma nianze kutafuta kazi tena...hiyo hela ilikua nyingi sana kipindi hicho hawakurudisha hiyo Ada...
 
Ni Pesa ndefu Peasant's Son's & Daughters hawawezi kulipia HIO elimu ya urubani
Ndio hivyo kama mimi namshauri ikishindikana walau asome huku huku tu bongo aendeshe hutu tundege walau awe amekamilisha ndoto yake kwa sehemu fulani ,hata kama akisema japo kuwa sikuendesha ndege kubwa lakini walau niliitwa pilot
 
Sawa mkuu hapo nimekuelewa sana...
Bado upo kitengoni lakini... Yaani matengenezo au kazi nyingine kabisa
 
Nipo kwenye kazi nyingine kabisa ila inahusiana na Engine za magari na magari ya kutoka SA na Parts zake..
Safi sana mkuu...
Mi kina broo wangu yupo dom hapa ni aircraft eng huwa naingia pale likitokea deal la kupiga rangi hvi vindege vidogo vidogo...

Hivo kuna hint huwa napata pata ambazo kwa huku jf naona mkuu upo deep sana ndo mana nikauliza vile πŸ™πŸ™πŸ™
 
Mimi naenda SA nilikua na dream hiyo na Ada nilitoka nayo Tanzania nilifatilia sana nilipofika pale nikakutana na kazi na wengi wanaofanya kazi hawana hata Elimu kubwa nikaona nijichanganye na kazi sasa hivi nipo na magari haswa ya Kutoka SA au Mashine Tools...
 
Safi mkuu.. maokoto kwanza .
Ila now si upo tz hapa au
...!?
 
Wanaotaka ushauri wachukue kwako.Mimi nina taaluma nao kiasi fulani na ndio maana nimekujua hii ni fani yako.
Ukweli ni kuwa kozi za urubani ni ghali sana na asikudanganye mtu akakutajia kiwango fulani kwamba ndio utafuzu mpaka CPL.
kama unataka upate unafuu na umalize haraka nenda Marekani,sio Afrika kusini.
 
Ada yake mtu anaetaka kusoma urubani akunjue Misimbazi mingapi? Swali la MTEGO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…