Nafanyaje kuwa pilot wa ndege?

Nafanyaje kuwa pilot wa ndege?

Ada yake mtu anaetaka kusoma urubani akunjue Misimbazi mingapi? Swali la MTEGO
Mkuu sasa hivi sijafatilia unajua miaka ya nyuma Ada ya SA ilikua inahusisha Nchi za SADC sasa hivi wametoa tulikua tunalipa kidogo sana ukitaka kusoma chochote toka SA wameamua kufanya biashara kwenye Elimu sijawafatilia zaidi zaidi naulizwa accommodation tu kwa vijana walio tayari kujiunga..
 
Wakuu nahisi nina kitu.

Tafadhali nisibezwe maana hii imekuwa ndoto yangu kitambo sasa.

Sasa nataka mnipe ABC's za namna navoweza kuifikia ndoto yangu hii.

Naanzia wapi? natakiwa kuwa na nini? au kuwaje namimi nianze kujipanga.

Zingatia: Ni ndege hizi za mchawi mweupe kama hizi alizoleta magu na sio zile zenu za kuruka usiku tu.
Kijana Pilot ni dereva kama dereva wa Mwendokasi
 
Waambie pia hio ni kwa saa moja. Practical. Sasa utahitaji masaa mangapi hadi ufuzu hizo ndege ndogo halafu ukitoka hapo ukasomee mashine kubwa utajua simulator training itacost how much pale airbus France au huki USA boeng.
Upo vizri sana...
Haya mambo sio rahisi hivo.
Mi sijaona pilot anasema kasoma NIT hapo mybe wapo ila sijaona
 
Mkuu sio pilot wala Aircraft Eng...nimefanya kazi kama saidia fundi kwenye meli kubwa kwa muda mrefu ila nilisoma Mechanics kwa level ya kawaida hapo Stellenbosch University...mimi pia nilikua natamani kusoma Urubani mwaka 1999 nililipa Ada ilikua rand 10,000 chuo kimoja hapo Pretoria baadae nikapata kazi nikaona bora nifanye kazi tu kuliko kusoma nianze kutafuta kazi tena...hiyo hela ilikua nyingi sana kipindi hicho hawakurudisha hiyo Ada...
Popote ulipo jua kuwa yako mengi unakuwa unashare hapa haujui ni kiasi gani unanimotivate lakini itoshe kusema wewe ni mpambanaji ninayekukubali sana .
Bravo Kaka.
 
Dereva ni dereva
Mbona Wana majina tofauti Rubani ni yeyote anayeendesha chombo Cha moto hewani kusiko na Ardhi akitumia utaalamu na dira sio kukodoa macho tu

Dreva ni muendesha chombo Cha moto ardhini bila kutumia utaalamu wa Hali ya juu Wala dira anaendesha Kwa kukodoa mimacho tu kama mjusi aliyefiwa na mkwewe kuangalia mbele kwenye barabara bila dira yeyote
 
Daah aisee madereva tuna tabu hapa...
 
Mkuu ma rubani wengi wenye CPL ni watoto wa watu wenye uwezo. Sasa hivi wanaongezeka watoto wa kihindi.
ATCL wana uhaba wa marubani jilipue.
For sure nilipanga mtoto wangu asomee urubani lakini hapo sitaweza,,ngoja nijichange halafu nijilipue nimtafutie chuo ughaibuni akapambane mwenyewe maana hata akisoma hapa bongo ni shida tu!
 
For sure nilipanga mtoto wangu asomee urubani lakini hapo sitaweza,,ngoja nijichange halafu nijilipue nimtafutie chuo ughaibuni akapambane mwenyewe maana hata akisoma hapa bongo ni shida tu!
Mtoto kutoka kimaisha ni gharama sio lelemama

Na kugeuza status ya kizazi kutoka umaskini kwenda juu lazima aweko wa kujilipua

Kuna wazazi wameuza Hadi nyumba jijini Dar watoto watoke kimaisha wakarudi vijijini kuishi maisha ya kawaida

Julipue tu upate kizazi kilichofanikiwa

Otherwise vicious circle ya umaskini haiji kwisha kwenye familia au ukoo

Hongera kupanga kujilipua nakuunga mkono
 
Back
Top Bottom