Nafasi iliyopatikana kwenye uchaguzi wa 2020 ikitumika vizuri ni faida kubwa kwa CCM

Nafasi iliyopatikana kwenye uchaguzi wa 2020 ikitumika vizuri ni faida kubwa kwa CCM

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Uchaguzi wa mwaka 2015 ulikuwa mgumu mno kuwahi kutokea tangu vyama vingi vya siasa vianzishwe. CCM ilipita kwenye tundu la sindano kushinda ule uchaguzi. Chama kilikuwa hoi mno. Kabla hata ya Lowassa kuhama tayari upinzani ulikuwa una nguvu mno kutokana na kuwepo vichwa hatari mno kisiasa vikiongozwa na Dr Slaa. Ni tofauti kabisa na upinzani huu uliopo unaopambana na bodaboda & viccoba. Inashangaza kumshambulia mtu ambaye hawezi kukijibu chochote na wala hana tatizo na wewe. Lema ni laana ya taifa. Upinzani uliokuwepo hadi 2015 ulikuwa unajenga hoja nzito huku ukishawishi wananchi kwa namna nzuri. Lowasa kujiunga nao ndo ikawa msumari wa mwisho kwenye jeneza ila kwa umahiri wa viongozi wa CCM tulishinda ule uchaguzi.

Uchaguzi wa 2020 ulikuwa wa kibabe na iko wazi kwamba demokrasia ilikanyagwa hadharani. Uchaguzi haukuwa huru wala wa haki. Mengi yameshazungumzwa kuhusu ule uchaguzi hivyo sitaelezea sana. Leo nataka niwakumbushe wanaCCM kuwa pamoja na uchaguzi ule kutupendelea lakini kwa hii miaka mitano tumepata nafasi ya pekee kujisahihisha ili 2025 kwenye uchaguzi utakaokuwa huru na wa haki tusipate shida kushinda uchaguzi hasa kwa nafasi za wabunge na madiwani. Haiwezekani kwa sasa halmashauri karibu zote ziwe chini ya CCM halafu ifike 2025 kukawa hakuna lolote lililofanyika la kujinadi kwenye uchaguzi.

Mbunge pambana sana jimboni kwako kuchochea maendeleo ili 2025 hawa wapinzani wasikuangushe. Kwenye kampeni wananchi watataka kuona mbunge au diwani umefanya nini kwenye miaka mitano na sio maneno matupu. Wapinzani wao watamwaga tu maneno kwasababu hawakuwa wakiongoza halmashauri. Mama Samia tayari kashashinda hata kabla ya uchaguzi kwa sababu hadi wapinzani wanamkubali na tuzo wamempa. Kwa vyovyote vile Mama hataingilia uchaguzi kwahiyo wagombea wote bila kujali vyama watashinda kwa haki. Mbunge au diwani wa CCM asiyesoma alama za nyakati ajue kabisa atapoteza jimbo. Binafsi tayari nimeshashauriwa kutia nia kwenye jimbo mojawapo hapa nchini.
 
Rais yeyote atakayekuja,heshima yake italetwa na katiba mpya na si vinginevyo.ata mama Ssh akitaka ajijengee jina na heshima alete katiba mpya.bila katiba mpya ni KAZI bureee.
 
Kulikuwa na ugumu Gani??jeshi,polisi mahakama,tume zilikua ccm
 
Back
Top Bottom