Nafasi ipi ni ngumu kuicheza katika soka?

Nafasi ipi ni ngumu kuicheza katika soka?

Golikipa yeye binafsi akiamua anaweza akaigombanisha timu, viongozi, wachezaji na wanaobeti. Kitu kama hicho hawezi kufanya mchezaji yeyote yeye binafsi.
 
Hakuna nafasi nyepesi, nafasi zote ngumu, wewe usiyekuwa position yako ndio unaona mateso, ila mwenyewe anainjoi kabisa na ukimtoa hapo ukampeleka kwingine ni adhabu kubwa mnoo kwake...
 
6 na 8

6 anatoa hatima ya timu ifungwee au isifungwe (kiungo mkabaji)

8 anatoa hatima ya timu ifunge goal ngapi au itoe droo (kiungo mchezeshaji)

lakini kiujumla wachezaji wote wanatengemea ndiomaana ikaitwa TEAM
Team; kikundi cha watu wanao fanya kazi pamoja kufanikisha dhamira yao
 
Wengi wanasema no 6.sina hakika sana kama mmecheza mpira mnajua mifumo mbali mbali.nimecheza karibu nambaa zote tu 11.
Zote sawa tu inategemea na mfumo mnaotumia, maelewano yaani kujuliana kitimu n.k

Middle hiyo 6 au 8 ukiijulia unainjoi sana ni namba nyepesi tu.
 
Me nafikiri ni nafasi ya kiungo mkabaji. Imagine unatakiwa ukabe, ufanye interception, ufanye blocking, tackling na bado uanzishe mashambulizi kwenda langoni kwa mpinzani wako. Ukizubaa ndio timu inaelemewa.

Kwa upande wako ni nafasi/namba gani ni ngumu kuicheza kwenye football?
Kwa kutumia principle ya LOGIC nafasi ngumu ni KIPA... watu hawataki kusikia timu imefungwa hata kama wote 10 waliopo uwanjani wamefanya makosa....

😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Me nafikiri ni nafasi ya kiungo mkabaji. Imagine unatakiwa ukabe, ufanye interception, ufanye blocking, tackling na bado uanzishe mashambulizi kwenda langoni kwa mpinzani wako. Ukizubaa ndio timu inaelemewa.
Nafkiri kukaba siku hz Ni System (Pressing System n Zone playing ) na No.6 anatumika kama Quarter back wa pili zaidi..
mfano 4-3-3 Yani immediately mpira ukipotea nje watakuwa 7 ndani watatu.
Kazi ipo kwa AMF na CM kuhakikihsa Wanapenya na kuposes kuelekea kwa adui akili nyingi Sana inahitajika kuliko nguvu.
 
Namba 6 ni namba ngumu kama timu inatumia kiungo mkabaji mmoja, kwa sababu inatakiwa ushuke kwa namba 5 na 4 wakat wa kukaba kisha uchukue mipira wakat wa kutengeneza mashambulizi kisha umuangalie namba nane kumi au mawinga, Yani unakuwa kama punda timu ikiyumba tuu duarani lawama kwako

Namba sita inakuwa na unafuu kama timu ikitumia viungo wakabaj wawili ambao mnagawana dimba la chini kushoto na kulia au juu na chini mnakuwa mnaswitch

Ila all in all namba sita ni ngumu kwa sababu haikupi mda wa kupumzika kidogo tofaut na namba zingine namba sita mda wote unakuwa unajog na kusprint
 
Wengi wanasema no 6.sina hakika sana kama mmecheza mpira mnajua mifumo mbali mbali.nimecheza karibu nambaa zote tu 11.
Zote sawa tu inategemea na mfumo mnaotumia, maelewano yaani kujuliana kitimu n.k

Middle hiyo 6 au 8 ukiijulia unainjoi sana ni namba nyepesi tu.

Yani point kubwa ni kwamba inategemea na mfumo wa mwalimu, Ila sita ni position ya muhimu sana ambao wanakuwaga hawaonekani sana ukubwa wa kazi zao ila ndio muhimili wa timu
 
Kazi ngumu kabisa kwenye mpira wa miguu ni kutupia mpira wavuni(kufunga) na huwezi kushinda mechi bila kushinda ndio maana wafungaji wanalipwa pesa nyingi, wanapata umaarufu pamoja na kuchukua tuzo
 
Kazi ngumu kabisa kwenye mpira wa miguu ni kutupia mpira wavuni(kufunga) na huwezi kushinda mechi bila kushinda ndio maana wafungaji wanalipwa pesa nyingi, wanapata umaarufu pamoja na kuchukua tuzo
Hata beki Canavalo alichukua tuzo,viungo akina Zidane,Modric Pavel Nedved wakabeba
 
Kiungo.

Ukiangalia hata takwimu.

Viungo wanaanzaga kuonekana bora baada ya umri kusogea(late 20 au early 30).

Ni nafasi ambayo inataka mtu awe mzoefu kwanza.

Nafasi kama Winger, FBs, Striker, mara nyingi unakuta hata madogo wa 19, 20 wanakiwasha.

Ambapo kwa upande kwa Viungo ni nadra kukuta anaanza kukiwasha akiwa na umri mdogo.

Baada ya kiungo zinazofuatia ni GKs na CBs.

Sent using Jamii Forums mobile app
Fabregas,wilshere,mcOcran,gerald
 
Back
Top Bottom