Lukonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 1,469
- 2,086
Wanaitaji:
• Kinyozi 1
• Msusi 1
• Msafishaji na kuremba kucha 1
Aina ya kazi, kuwezesha:
• Urembo(wanawake)
• Utanashati(wanaume)
Sehemu ya kazi:
• Kivule - Ilala(DSM)
Mwajiri:
• Mtu binafsi
Ujuzi:
• Mwenye ujuzi wa kutosha kulingana na kazi husika, mfano: kunyoa(kinyozi) mitindo mbalimbali. Kutumia dawa na vipodozi mbalimbali kwa kadri ya mahitaji ya mteja pia kutoa ushauri kulingana na hitaji sahihi la mteja.
• Pia aweze kuwa na matumizi sahihi na utunzaji wa vifaa vya kazi.
Maelezo mahsusi:
• Waafanyakazi tajwa hapo juu, wenye utaalam, ujuzi na uzoefu wa kufanya kazi katika Barbershop na sehemu ya ususi.
• Wawe ni wasafi, wakweli, waaminifu, wenye kuipenda kazi yao, wawe na lugha nzuri kwa wateja, uelewa mzuri wa kazi, wapenda kujifunza zaidi na wenye uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja.
• Pia, waweze kujisimamia kwa kazi za siku kwa siku kwa ujumla na kufuata taratibu za kazi zilizopo.
Malipo:
• Aina na kiasi cha malipo ni makubaliano kulinganana hadhi na eneo la kazi.
Mahitaji:
• Barua ya maombi
• Kitambulisho cha NIDA
• Barua ya utambulisho toka serikali ya mtaa anapoishi.
• Cheti chochote kuthibitisha mafunzo aliyowahi kupata kulingana na kazi husika(faida ya nyongeza).
Tarehe ya mwisho kupokea maombi: 08/09/2024
Mawasiliano:
• Simu: 0757316497
• Whatsapp: 0757316497