Nafasi ya kazi ya Saluni

Nafasi ya kazi ya Saluni

1: Fani hizi inatolewa mafunzo na VETA kwa sasa, ukisoma sentensi husika imesema kuwa ni sifa ya faida/ziada/added advantage.

2: Ukiwekeza hela yako kufanya kitu kizuri/pesa hutumika. Ukiajiri kwa kukutana barabarani, ukilizwa ndo utakumbuka busara uliiacha wapi wakati wa kupata watenda kazi.

3: Kazi hii ikifanywa vyema/mazingira rafiki inawaingizia kipato vijana kuliko watu wengi tunaoenda ofisini/white collar jobs hivyo ni kuiheshimisha tu.
Safi sana mkuu haya ni mabadiliko chanya kwenye sekta ya ajira binafsi kama hizi ZINGATIA tu na kwenye malipo angalao yawe manono pia😂
 
Weka mshahara nijue nisije kukuletea barua alafu mwisho wa mwezi nikulambe na makofi
Kwa kauli hii wewe si mhitaji wa kweli. Pia siwezi kuweka pesa sehemu nianze kumtenda anaetakiwa kuwezesha pesa kupatikana kwani haya maudhi yatarudi kwa wanaohudumiwa. Huwezi kutimiza 10 GOLDEN rules kwa mteja huku una njaa au maudhi.
 
+255789123575

Kuna huyo mwanangu anaitwa Amasha fundi sana sana yupo ukonga ebu mcheki mpe offer kama unataka uwe na saloon yenye vinyozi walionyooka maana hizi saluni za kisasa mara nyingi vinyozi huwa ni chenga.

Ukijikuta boss lazima utafutwe na mfanyakazi sawa.
Nitampigia muda si mrefu.
 
1.jpg

Wanaitaji:
• Kinyozi 1
• Msusi 1
• Msafishaji na kuremba kucha 1

Aina ya kazi, kuwezesha:
• Urembo(wanawake)
• Utanashati(wanaume)

Sehemu ya kazi:
• Kivule - Ilala(DSM)

Mwajiri:
• Mtu binafsi

Ujuzi:
• Mwenye ujuzi wa kutosha kulingana na kazi husika, mfano: kunyoa(kinyozi) mitindo mbalimbali. Kutumia dawa na vipodozi mbalimbali kwa kadri ya mahitaji ya mteja pia kutoa ushauri kulingana na hitaji sahihi la mteja.

• Pia aweze kuwa na matumizi sahihi na utunzaji wa vifaa vya kazi.

Maelezo mahsusi:
• Waafanyakazi tajwa hapo juu, wenye utaalam, ujuzi na uzoefu wa kufanya kazi katika Barbershop na sehemu ya ususi.

• Wawe ni wasafi, wakweli, waaminifu, wenye kuipenda kazi yao, wawe na lugha nzuri kwa wateja, uelewa mzuri wa kazi, wapenda kujifunza zaidi na wenye uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja.

• Pia, waweze kujisimamia kwa kazi za siku kwa siku kwa ujumla na kufuata taratibu za kazi zilizopo.

Malipo:
• Aina na kiasi cha malipo ni makubaliano kulinganana hadhi na eneo la kazi.

Mahitaji:
• Barua ya maombi
• Kitambulisho cha NIDA
• Barua ya utambulisho toka serikali ya mtaa anapoishi.
• Cheti chochote kuthibitisha mafunzo aliyowahi kupata kulingana na kazi husika(faida ya nyongeza).

Tarehe ya mwisho kupokea maombi: 08/09/2024

Mawasiliano:
• Simu: 0757316497
• Whatsapp: 0757316497
Weka malipo wazi

Makubaliano ndio aina gani ya malipo
 
Weka malipo wazi

Makubaliano ndio aina gani ya malipo

Kama ulishakuwa karibu na hii kazi utaelewa. Kuna wanaopenda:
1: Mshahara

AU
2: Kumlipa mwenye mtaji kwa idadi ya viti na yeye kutafuta yake.

Yote hayo hutegemea mzunguko wa watu, hadhi ya saluni pia nani alipe nini.
 
+255789123575

Kuna huyo mwanangu anaitwa Amasha fundi sana sana yupo ukonga ebu mcheki mpe offer kama unataka uwe na saloon yenye vinyozi walionyooka maana hizi saluni za kisasa mara nyingi vinyozi huwa ni chenga.

Ukijikuta boss lazima utafutwe na mfanyakazi sawa.
Nimewasiliana nae, yuko sehemu anaendelea kusukuma gurudumu. Tumeongea mengi na ni kijana mkweli na mwaminifu kulingana na mrejeshi wake. Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom