Nafasi ya mume. . .

Nafasi ya mume. . .

Sasa kama wenyewe mnasaidiana majukumu je? Si tutajuaje banaa! Manake inawezekana yeye ana mgeni na wewe umeona udeki, mwanao akakulilia ukaamua umbebe! Sana nikifika hapo kama sijiskii kudeki ntakuambia nipe mtoto nimsalimie. Nifanye lililonileta (kama ni mzinga wa hela ama kusalimia) kisha nikaonyeshe ufundi wa kulea mume kwangu! Ukija ukute shemejio anapepelewa na kipepea mpenzi,lol
lol wafanye kilicho waleta hapo sio kuchokonoa waliyoyakuta.
kila nyumba ina utaratibu wake jaman.
kina mume kupiga deki ni part n parcel ya utaratibu wao hapo nyumban je?
kweli imefika wakat waache midomo domo wa2lie makwao wao kila siku kwa kaka yao 2 loh.
 
Aksante Lizzy kwa mada Maridhawa. Aksanteni wachangiaji wote kwa michango mizuri sana.

Kongosho na AishaDii, mmezungumzia haki za mwanamke kama kichocheo kimojawapo cha kuvunjika kwa ndoa nyingi. To tell you the truth mimi sizifahamu vizuri.si kwamba hazinihusu la hasha ila nadhani nimekuwa mzembe katika hilo. Ninaomba mnisaidie kuainisha zile zinazohatarisha ndoa.
 
....kaka, a real husband na a real man ni watu wawili tofauti bana, au nini mtazamo wako juu ya vyeo hivi viwili?

Kweli kabisa kaka,

Siyo kila mwanamume ambaye anaonekana wa shoka, anaweza kuwa mume mzuri. Wakati suala la kujua kama mtu ni mume na dume la uhakika kabisa yanaonekana ndani ya nyumba zaidi, na yanamhusu mke, ila suala la kujua kama mtu ni mwanamume wa maana au la linaonekana hata nje ya nyumba....Katika hili suala tuonaongelea mume wa ukweli.

Hata sharobalo (ambaye watu wengi wanamwona kama mtu wa hovyo), anaweza kuwa na hizo sifa zote kwa mke wake!!

Heri ya mwaka mpya babu.

Ahsante!!
Kweli unatakiwa uwe mtetezi wa mkeo. Sio unaacha familia nzima iunde aliance dhidi yake.

Yaani mwanamume usipokuwa imara na bahati mbaya ukawa unatoka kwenye familia kubwa na ambayo ina mavuvuzela wa kutosha, unaweza kumfanya mke hata asijue mume wake ni yupi....Yaani husband anabaki kuyumba tu kama debe tupu. That's not health kwa ndoa.

Binafsi, when it comes to my wife, nawaomba ndugu wote wanipe break kidogo....She is mine and only mine, and she belongs to a no go zone!!

Hahahahah Mbu sasa we unataka kuchokonoa mambo tu. Ni one of the same, sema tatizo ni kwamba tafsiri inaweza ikatofautiana toka mtu na mtu, tamaduni na tamaduni. Muolewaji anaweza akamwona mumewe ni "real husband. . . real man" wakati watu wa nje wanamwona sivyo.

There you are!!

Aksante Lizzy kwa mada Maridhawa. Aksanteni wachangiaji wote kwa michango mizuri sana.

Kongosho na AishaDii, mmezungumzia haki za mwanamke kama kichocheo kimojawapo cha kuvunjika kwa ndoa nyingi. To tell you the truth mimi sizifahamu vizuri.si kwamba hazinihusu la hasha ila nadhani nimekuwa mzembe katika hilo. Ninaomba mnisaidie kuainisha zile zinazohatarisha ndoa.

MJ1,

Mie sina hakika. ila naamini kwamba baadhi ya wanaume wameshindwa kudeal na changamoto zinazoletwa na hii lifestyle impya. Badala yake wanatafuta visingizio. Ndiyo maana utasikia kuwa wanawake wengi ambao ni wasomi wa siku hizi hawaoleki. Ila naamini kuwa, wanaume wengi wanashindwa kudeal na mabadiliko yanayosababishwa na hali ya mwanamke kuwa empowered kielimu, kiuchumi na kimtazamo. Ninao washikaji wengi ambao hadi sasa wanasema kuwa wanawaogopa wasomi kama ukoma....

I personally wish my wife was a professor ili nione hicho wanachokiogopa!!

Heri ya mwaka mpya kwa wadau wote wa MMU,

Babu DC
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Babu DC mimi nadhani wachangiaji wengi, including you mmeliweka sawa hili la nafasi ya Mwanaume, nina amini kabisa mwanaume na mwanamke wakijiheshimu, wakiwa na upendo wenye mipaka kwa ndugu zao yaani ule upendo wa baba/mama/dada/kaka zangu, ninawapenda sana lakini mume/mke wangu pia ni sehemu ya maisha yangu. Kama kuna tatizo nitazungumza nae mimi na tutalitatua kwa staili yetu sisi.
Sidhani kama mawifi/wakwe au mashemeji hawatakuelewa.

Ingawa ninaelewa pia kuwa wako wanawake wenye chokochoko kwa mawifi na wakwe zao! Na hata hawa ni mume pekee anayeweza kuwadhibiti iwapo atauweka msimamo thabit kwa mkewe pia.

Lizzy aksante kwa hii mada
 
Lizzy nakushukuru kwa uzi huu mzuri na wenye mafundisho muhimu sana hasa wale ambao hatujaingia humo ndoani,
Kwani binafsi nimejifunza mengi kupitia wachangiaji na nazidi kufatilia coz naamini mwisho wa siku nikiingia humo nitakuwa na uelewa fulan kupambana na situation km hizi,

Nawatakien heri ya mwaka mpya wadau wote wa MMU.
 
Safi sana binti,

Ukiitumia vizuri MMU na ukawa na mtazamo chanya, basi utakuwa very informed kabla ya kuanza maisha matamu (ambayo pia ni machungu sana) ya ndoa!

Jitahidi kutumia muda wako kudigest posts za watu kwani kuna vitu ambavyo mwanzoni unaweza kuviona vinakera ila ukifuatilia kwa karibu unakuta vimebeba ujumbe mzito. My simplest but yet the best example ni post ya The Boss, my Platnum thread for 2011,

https://www.jamiiforums.com/habari-...kishaamua-kuwa-na-nyumba-ndogo-the-guide.html

Babu DC
 
Babu DC mimi nadhani wachangiaji wengi, including you mmeliweka sawa hili la nafasi ya Mwanaume, nina amini kabisa mwanaume na mwanamke wakijiheshimu, wakiwa na upendo wenye mipaka kwa ndugu zao yaani ule upendo wa baba/mama/dada/kaka zangu, ninawapenda sana lakini mume/mke wangu pia ni sehemu ya maisha yangu. Kama kuna tatizo nitazungumza nae mimi na tutalitatua kwa staili yetu sisi.
Sidhani kama mawifi/wakwe au mashemeji hawatakuelewa.

Ingawa ninaelewa pia kuwa wako wanawake wenye chokochoko kwa mawifi na wakwe zao! Na hata hawa ni mume pekee anayeweza kuwadhibiti iwapo atauweka msimamo thabit kwa mkewe pia.

Lizzy aksante kwa hii mada

MJ1,

Linapokuja suala la ndoa, mume anatakiwa kuwa msemaji mkuu katika mambo yote ya muhimu yanayohusu kuset policy za familia...Naamini utakubaliana na mimi kwenye hili!!

Huwezi ukamwachia kila mtu akawa PRO halafu ndoa isiyumbe.

Hata kwa watoto na ndugu wanaoishi kwako, kama kuna suala ambalo linawahusu wao wenyewe (may be ugomvi) lazima walipoti kwa babu (au mama kama hakuna objection). Kwa hiyo suala linalomhusu mke, inabidi ndugu wakueleze wewe na ndiyo umalizane na mke wako. Hata hivyo, ni muhimu sana mume kuweka msimamo wake wazi mbele ya ndugu zake (vinginevyo watamyumbisha kama TV adverts). Awaeleze tu kuwa hana muda na udaku udaku..Unless wanaweza kuback allegations zozote wanazotaka kuleta. If not, wakae tu kimya!!
 
Hapa nakubaliana na wewe kabisa. Kwa suala la kumprotect wife dhidi ya chokochoko za mawifi (kamma zipo)mume anawajibika lakini pia mke anatakiwa aifahamu role yake katika hili si anakuwa yeye ndo mchokozi kila mara kwa vile tu mumewe anamtetea! Ama sivyo sentence za 'hata mkichonga vipi, kakenu/mwanao ashanipenda' zitatawala na ugomvi hautokaa uishe!
 
MJ1 ndio maana ni vizuri kaka yao aongee nao ili kama mke ndio tatizo wamweleze. Nae akipima na kuona kweli kwamba mkewe anaweza akawa ndie kisabibishi kikuu basi anaweza akaongea nae mwenyewe badala ya kuacha aendelee kukorofishana na mawifi zake.

@babu DC
Ahsante babu.
Nimefurahi sana kuona ulivyoelezea namna wanaume wanavyosingizia na kulaumu "haki sawa" badala ya kutokujiamini kwao na woga wa changamoto. Haki sawa zinaweza zikawepo na bado nyumbani kila mtu akawa kwenye nafasi yake, sema basi tu watu wanatafuta short cut ya matatizo yao binafsi.

@Canta
Karibu mwaya, hata zile zinazotisha usiziogope we jifunze taratibu yakikufika ya kukufika uwe na solution za kila aina.
 
mpaka dada waje kuleta maneno kuna jambo moja hapo

shule ndogo na kukosa kazi ya kufanya.......

ukitaka kumlinda mkeo,somesha dada zako
hakikisha wanapata kazi za maana.......

na somesha mkeo pia ikibidi........

nakubaliana na wewe, shule muhimu jamani.
 
Kwa upande mwingine
ni bora wifi mshari ambaye hajasoma kuliko aliyesoma

mtu ambaye hajasoma ugomvi wake ni wa kumwagiana maji machafu au kutunga uongo usio na kichwa wala miguu

lakini msomi, anaweza kukuangamiza kama hauko makini

halafu hata mashemeji nao
wabo baadhi wana roho hata za mawifi afadhali
tena wanamme wakiwa wabaya ni hatari sana
wanaweza fanya vitu vya ajabu zaidi

hii nakubaliana nayo kwa uzoefu.
 
Hapa nakubaliana na wewe kabisa. Kwa suala la kumprotect wife dhidi ya chokochoko za mawifi (kamma zipo)mume anawajibika lakini pia mke anatakiwa aifahamu role yake katika hili si anakuwa yeye ndo mchokozi kila mara kwa vile tu mumewe anamtetea! Ama sivyo sentence za 'hata mkichonga vipi, kakenu/mwanao ashanipenda' zitatawala na ugomvi hautokaa uishe!

Kweli dada,

Ni jukumu la mwanamume pia kujua aina ya mke aliyemuoa na kutafuta mbinu muafaka za kudeal naye pale inapotokea matatizo ya namna hii. Kama mwanamke ni dizaini ya kasuku na mwenye uswahili mwingi pia ajue. Ila hata angekuwa hivyo, na maadam kampenda na kukubali kuishi naye, basi mume anawajibika kumlinda dhidi ya chochoko zozote za ndugu. La sivyo amwache atafute mwingine!
 
...hakuna fitna kubwa inayosababisha manung'uniko haya kama fitna ya mali...
 
Kweli kabisa kaka,

Siyo kila mwanamume ambaye anaonekana wa shoka, anaweza kuwa mume mzuri. Wakati suala la kujua kama mtu ni mume na dume la uhakika kabisa yanaonekana ndani ya nyumba zaidi, na yanamhusu mke, ila suala la kujua kama mtu ni mwanamume wa maana au la linaonekana hata nje ya nyumba....Katika hili suala tuonaongelea mume wa ukweli.

Hata sharobalo (ambaye watu wengi wanamwona kama mtu wa hovyo), anaweza kuwa na hizo sifa zote kwa mke wake!!

Yaani mwanamume usipokuwa imara na bahati mbaya ukawa unatoka kwenye familia kubwa na ambayo ina mavuvuzela wa kutosha, unaweza kumfanya mke hata asijue mume wake ni yupi....Yaani husband anabaki kuyumba tu kama debe tupu. That's not health kwa ndoa.

Binafsi, when it comes to my wife, nawaomba ndugu wote wanipe break kidogo....She is mine and only mine, and she belongs to a no go zone!!

There you are!!

MJ1,

Mie sina hakika. ila naamini kwamba baadhi ya wanaume wameshindwa kudeal na changamoto zinazoletwa na hii lifestyle impya. Badala yake wanatafuta visingizio. Ndiyo maana utasikia kuwa wanawake wengi ambao ni wasomi wa siku hizi hawaoleki. Ila naamini kuwa, wanaume wengi wanashindwa kudeal na mabadiliko yanayosababishwa na hali ya mwanamke kuwa empowered kielimu, kiuchumi na kimtazamo. Ninao washikaji wengi ambao hadi sasa wanasema kuwa wanawaogopa wasomi kama ukoma....

I personally wish my wife was a professor ili nione hicho wanachokiogopa!!

Heri ya mwaka mpya kwa wadau wote wa MMU,

Babu DC

.....Mkuu DC unamwaga vitu vilivyojaa hekima na busara ya hali ya juu na ni ukweli mtupu. Hongera zako bana!!! Wanaume wanaogopa wanawake wasomi, lakini hawajui mke msoni ni asset kubwa sana kwa familia ukilinganisha na yule ambaye aliishia madarasa ya chini ama kwa kuukimbia umande au kutohimili mikiki mikiki ya shule.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Ila na nyie kina mama ni mafundi wa kuchimba umbeya na vijimaneno ambavyo havina kichwa wala miguu. Wakati mwingine unaletewa maneno ya umbea na mke ambayo hata vyanzo vyake havieleweki na unapodadisi kujua wapi yametoka ili ushughulike na vyanzo unakosa ushirikiano akidai kuwa hataki kuharibu uhusiano na vyanzo hivyo. Ila anataka uchukue hatua haraka sana iwezekanavyo.
 
.....Mkuu DC unamwaga vitu vilivyojaa hekima na busara ya hali ya juu na ni ukweli mtupu. Hongera zako bana!!! Wanaume wanaogopa wanawake wasomi, lakini hawajui mke msoni ni asset kubwa sana kwa familia ukilinganisha na yule ambaye aliishia madarasa ya chini ama kwa kuukimbia umande au kutohimili mikiki mikiki ya shule.

....huyu mzee hajawahi kuusikia ule msemo, "...be careful what you wish for!"...
Mke msomi anaweza kuwa chachu au chungu kwenye ndoa yako kwa sababu zilizo nje ya uwezo wako,
mfano akiwa ni mtumishi wa umma, mbunge, nk, nk....yeye siku zote yu kwenye semina, vikao, safarini tuu...

Ridhika na maajaaliwa yako bana.

...hakuna fitna kubwa inayosababisha manung'uniko haya kama fitna ya mali...

True!!
Sasa watu wafanyeje kama ndugu na mke wanagombea mali zake ilhali bado yuko hai?
 
....huyu mzee hajawahi kuusikia ule msemo, "...be careful what you wish for!"...
Mke msomi anaweza kuwa chachu au chungu kwenye ndoa yako kwa sababu zilizo nje ya uwezo wako,
mfano akiwa ni mtumishi wa umma, mbunge, nk, nk....yeye siku zote yu kwenye semina, vikao, safarini tuu...

Ridhika na maajaaliwa yako bana.

kuna wanawake ambao waume zao ni wasomi, watumishi wa serikali, bankers, wabunge etc. wake zao wanajisikiaje kwani baba kila siku kiguu na njia.

Ila napenda sana familia ambazo ke na me ni high profile, baba akisafiri akirudi mama anasafiri the next da au wanapishana kama si airport basi mawinguni. Inatia raha sana pale wanapostaafu huku ndoa ikiwa imesimama imara. Umbali hustawisha penzi, mnapokutana inakuwa kama honeymoon vile.
 
Kama wote wanakuwa waaminifu ina raha yake. Tatizo linakuwepo kwenye malezi ya watoto.

Mie napenda walau mmoja awepo nyumbani ili watoto wawe na mzazi wa kuwaangalia na kufuatilia maendeleo ya shule ya watoto.

Kwa vyovyote vile, kila aina ya maisha ina changamoto zake!!
 
Back
Top Bottom