SoC01 Nafasi ya Mwanamke katika jamii na familia

SoC01 Nafasi ya Mwanamke katika jamii na familia

Stories of Change - 2021 Competition

Vicenza

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2019
Posts
1,020
Reaction score
1,515
Habari za saa wana JamiiForums,

Kwanza kabisa niingie moja kwa moja kwenye maada husika inayomuhusu mama/mwanamke wa kiafrika anayepitia changamoto mbalimbali,Ni kujaribu kujua jamii ya afrika ni kwa nini hatuwezi kuwaamini kinamama katika kufanya jambo la maendeleo katika familia na hata ngazi ya jamii husika inayomzunguka.

Kabla hutujaendelea ni vizuri kujua mwanamke ni nani katika familia na jamii kwa ujumla. Mwanamke katika familia kwenye hii karne ya ishirini na moja ni nguzo,msingi,fundi,na mlezi katika familia (wanaume mtusamehe hii ni zamu ya kina mama).Nitaeleza kwa mifano ni kwa nini mwanamke ni nguzo na msingi wa familia.

Mwanamke amekuwa nguzo ndani ya familia pale ambapo mwanaume anakuwa hajui wajibu ndani ya familia,ni katika nyakati tofauti mwanamke anapambana kuhudumia familia kutafuta chochote kitu ili tu watoto wapate ata mlo mmoja kwa siku,ni wazi kuwa wanaume wamekuwa wakitoroka majukumu yao ndani ya familia,hii inapelekea mama kupambania watoto kwa nguvu zake zote ili tu watoto wapate mlo waione kesho yake.Mwanamke amekuwa akipambana na changamoto nyingi sana kuipambania familia hasa watoto pale tu baba akiwa amekata tamaa kuwajibika.

Mwanamke ni msingi ndani ya familia katika nyanja tofauti pale tu mwanaume anapotoa maamuzi na amri lakini mwanamke anakuwa msingi wa maamuzi na utekelezaji.Mwanamke amekuwa akileta chanya ndani ya familia na kuifanya familia kuimarika.Mwanamke amekuwa akifanikisha majukumu kwa asilia kubwa,wengi tunajua wanawake wengi wamekuwa wanapenda kuwa na maendeleo ndani ya familia,na pengine kuwa na wivu wa kutaka kuinuka kimaendeleo,wanawake wamekuwa mstari wa mbele kuwashawishi wanaume zao nini kifanyike ili maendeleo yaonekane ndani ya familia,wanaume wamekuwa kama wapitisha sheria ndani ya familia lakini ni kwa ushawashi wa mwanamke, ila wengi hawajui ilo.Kwa mfano mwanamke anaweza akaona nyumba ya jirani ina mabati mazuri au kwa jirani kuna nyumba nzuri ya kisasa mtaa mzima,hapa wanawake wengi wanakuwa wanapenda sana maendeleo manyumbani kwao,ita mlazimu ajipange kima wazo na kwa weledi wa hali ya juu ili akaongee na mume wake kuhusu jambo hilo, ni kwa jinsi gani atamshawishi mwanaume ili wakubaliane kujenga nyumba ya kisasa ili na wao pia waonekane wamepiga hatua kwenye maendeleo na jamii.wengi watajua ni wazo la mwanaume kujenga nyumba ya kisasa lakini si kweli hii imetokana na msukumo na mawazo ya mwanamke kumshauri mwanaume katika kupiga hatua na kujikwamua katika kupiga vita umasikini.

Tuangaze nafasi mbalimbali ya mwanamke katika jamii.

Wanawake katika kilimo

Mwanamke katika jamii amekuwa akijipambanua kujiimarisha katika michango mbalimbali hasa kushiriki katika shughuli mbalimbali za jamii,wanawake wengi wamekuwa wahanga kuleta chanya katika jamii,hasa kuibua changamoto zinazo wakabili katika jamii inayo wazunguka,changamoto hizo ni kama vile miundombinu,hapa wahanga wakubwa wamekuwa wanawake hasa katika kupeleka mazao katika miji,tunatujua kwa asilimia kubwa wanawake wamekuwa wanachangia kwa asilimia kubwa sana katika kilimo,lakini changamoto wanazopitia ni nyingi sana hasa wanapo safirisha mazao yao,wanawake wamekuwa kipaza sauti kwa serikali katika kuleta chanya katika miuondombinu ya jamii,
46915050774_c9837229ae_b.jpg

picha na mtandao

Wanawake na teknologia

Hapa kidogo wanawake wengi wamekuwa wako nyuma katika teknologia hasa tehama kwa ujumla,hii inapelekea wanawake kuwa nyuma katika mabadiliko ya tehama na kuwalazimu kutumia mifumo duni katika kazi zao.wanawake wengi wamekuwa wahanga katika kutumia tehama.Hapa nina zungumzia mifumo ambayo itakayo weza kuwasadia katika biashara zao kama vile simu za janja zenye uwezo wa kurahisisha kazi zao kwa mda mfupi,wanawake wengi walioko vijijini wanakabiliwa na matatizo na mabadiliko ya tehama na kuwa nyuma ya mda.wengi wamekuwa wakipitwa na fursa nyingi katika mitandao na kupelekea kuwa nyuma kimaendeleo.

Wanawake katika ufundi

Katika sekta ya ufundi wanawake wamekuwa wako mbele kujutuma kujenga taifa,baadhi ya wanawake ikiwamo kwa makundi wamekuwa wakijikita kwenye masuala ya ufundi katika nyanja tofauti ikiwamo kujitegeme na kunzisha vikundi mbalimbali vya ufundi kama vile utengeneazaji wa magari,na masuala ya ujenzi,kwa namna mbalimbali wanawake wamekuwa wakijitegemea na kupambana na umasikini,na kuacha kuwa tegemezi kwa wanaume.kwa namna hiyo baadhi ya wanawake wamekuwa wakiepuka mateso kwa wanaume kwa kuwa tegemezi.Tanzania ni moja ya nchi ambayo imewezesha wanawake wengi katika ufundi wa masuala mbalimbali,kwa kuanzisha vyuo vya ufundi kuwalenga wanawake na wanaume kupambana na kuwa wabunifu na kupiga hatua katika maendeleo


25d5804bc7ce9ad365969c6cbff928be.jpg

picha na mtandao

Ni wazi kuwa wanawake wanapambana katika kazi na majukumu yao ya kila siku,kwa sasa hakuna tena kazi za wanaume na wanawake,kwa sasa kila kazi zina fanyika na jinsia zote,hii imetokana na wanawake kubaguliwa katika kazi na kupelekea kuamka na kuanza kujituma bila kuangalia jamii itasema nini.kwenye picha hapo juu tunamuona mwanamke akiwa yupo katika fani yake ya ufundi magari,pengine wanaume wange sema hastahili kufanya kazi kama hiyo la hasha,wanawake wanapenda sana kufanya kazi zozote ambazo kwa miaka ya nyuma zililkuwa zikifanywa na wanaume,kwa ongezeko kubwa wanawake wamekuwa wakijituma kuboresha maisha yao katika kufanya kazi kwa weledi bila kukata tamaa.Ni zamu ya wanawake kuamka na kufanya kazi zote halali bila kubaguana .

Wanawake katika siasa

Ni miaka mingi sana watanzania wanaamini kuongozwa na mwanamke ni ngumu,kwa miaka michache tumeona wanawake wanaongezeka katika masuala ya uongozi bila kukata tamaa kama watashinda au watashindwa kuwania nafasi za uongozi,kwa ongezeko la juu wanawake wamekuwa wakijitaidi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi na kufanya wananchi wengi waamini pia wanawake wanaweza kuongoza na kuleta maendeleo katika nchi,tumezoe kuona nafasi nyingi za uongozi ziki shikiliwa na wanaume ila kwa asilimia ndogo wanawake wakishika nafasi hizo,hii inaonyesha bado kuna kasumba mwanamke hawezi kuongoza wananchi ila sio kweli, wanawake wanaweza kuongoza tena kwa weledi wa hali ya juu kuazia ngazi ya kitongoji adi nafasi za juu zaidi,wanawake wamejitaidi kugombania nafasi za uongozi kutokana na changamoto wanazopitia katika jamii inayowazunguka,kwa kiasi wanawake katika serikali wamejitaidi kuwania nafasi za uongozi kama vile hayati mama Ana mngwira,ambaye aliamsha wanawake wengi kuwa viongozi,hii ili wafanya wanawake kuwa na muelekeo wa kuwania nafasi za uongozi,katika mipango na mikakati katika awamu ya raisi mama Samia imelenga wanawake katika uongozi,hii itafanya wananchi kuondoa kasumba ya kuwa wanawake hawawezi kuongoza nchi,
1.jpg
picha na mtandao​

Wanawake katika biashara

Wanawake wengi wamejitaidi kuchapa kazi katika biashara hasa vijijini na hata mijini,wanawake wamekuwa wakijituma kuchapa kazi kuliko kina baba,hapa wengi watabisha ila ukweli wanawake wanaujua,katika jamii mbalimbali wanawake wamekuwa wakipambana katika kazi,kwa mifano mingi hai wanawake wamekuwa wengi katika masoko makubwa kuliko wanaume,hii ina maana kuwa wanawake hawataki utani katika biashara,utakuta wanawake wengi wanapata changamoto za unyanyasaji kwa wanaume zao pindi watokapo sokoni wakiwa na fedha za biashara,hii uwalazimu kutoa pesa izo na kuwafanya warudi nyuma,kwa hali hiyo wanawake wamekuwa hawakati tamaa hata kidogo,wakijua kwamba wana watoto wakulea,biashara nyingi zimekuwa ziki fanyika na wanawake na kuleta ufanisi mkubwa katika maendeleo,hasa mama ntilie,na biashara nyingi za chakula zimekuwa zikifanywa na wanawake.biashara nyingi zimekuwa msaada kwa wanawake kujikwamua katika umasikini na kupiga hatua katika maendeleo.Ni wazi kuwa wanawake wengi wamesomesha watoto wao kupitia biashara mbalimbali,hii ni kutokana na kuwa wanawake wameimarika kwenye sekta ya biashara,serikali kwa kushirikiana na raisi wa nchi ijenge sera nzuri kuwaimarisha wanawake katika biashara na kuweka mazingira wezeshi ya biashara kwa Wanaume na wanawake Kwa usawa bila kubagua jinsia.Hii itawafanya kuacha kuwa tegemezi.
76ba12e2f92a00de52bc6152926f65b63d0de30d.jpg
picha na mtandao​

Hitimisho na mapendekezo

Ni wakati sasa wanawake kuanza kujitegemea na kuanza kufanya kazi kwa bidii ndani ya familia. Hapa ni kuangazia wajibu wa mwanamke katika familia na hata jamii husika. Kila fursa inayotokea mwanamke asibaki nyuma na kuanza kumtegemea mwanaume atafanya, baadhi ya wanawake wamekuwa wakitegea kuwa ni lazima mwanaume awajibike kwa kila nafasi lakini si wanaume wote watakuwa na mtazamo wa kuwajibika vyema, hii inawafanya wanawake wazembee katika fursa wakijua ni lazima mwanaume awajibike kwa kila kitu, kwa muda mwingi wanawake wanakuwa hawataki kujituma na mwishowe hushindwa kuendesha biashara pindi tu mwanaume amefariki.

Wanawake wote waanze kusema wanaweza, hii italeta chanya na mtazamo mzuri katika jamii na kuleta ushawishi mkubwa wa jamii kuanza kuamini kuwa pia hata wanawake wanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika jamii,kwa namna hii wanawake wengi watajua wajibu wao katika jamii na kuanza kuzijua fursa nyingi ndani na nje ya nchi,hususani kuchangamkia fursa zinazotokea katika jamii kama vile siasa,biashara,kilimo na hata masuala ya tehama.

Serikali ichangie kuhamasisha kuwafadhili wanawake wabunifu katika kazi zao. Hapa najua wanawake wanaweza kubuni na kufanya mapinduzi katika tekinologia,wengi tumezoe kuwaona wanaume wakifanya ubunifu na kuleta madiliko ndani na nje ya nchi,ila pia wanawake wanaweza tena sana kuleta mabadiliko,ni wakati sasa jamii kuanza kuwa na mtazamo chanya kuwa wanawake wanaweza.

Taasisi za kifedha ziboreshe mazingira mazuri ya mikopo kwa wanawake,apa naamini wanawake watakuwa wengi kupata mikopo,kwa asilia kubwa wanawake wanatumia mikopo vizuri kuliko wanaume au kina baba,(wanaume tulieni kwanza).kwa miaka ya karibu wanawake wanajituma sana katika biashara zao,wengi wana penda sana kupiga hatua za juu sana, kupiga vita umasikini,wanawake wame kuwa na mipango mirefu katika kupangilia mikopo watakayo ipata,hii hufanya wanawake kuamka na kunza kuchakarika katika biashara zao na kuweza kupiga hatua za maendeleo.

Miundombinu iboreshwe kurahisisha usafirishaji wa mazao na hata jamii,serikali iangaze vizuri maeno ambayo yenye changamoto ya miundombinu kuwasaidia wakulima na hata jamii kusafiri kwa unafuu zaidi na kupata mawasiliano.

# Haki sawa katika fursa za wanawake kwa wanaume izingatiwe.
 
Upvote 3
karibuni wote kwa mdahalo.
 
nikategemea wanawake watakuwa wa kwanza kuja kusoma na kupiga kura..(msiniangushe hii mada ni yenu kwa asilimia kubwa)😀
 
Si um edema kwenye tehama wako nyuma! Ndio uvumilie inawezekana hata kuusoma bado hawajausoma.
Wanawake ni mama zetu
Nalog off
naenda kuwa tafuta waijue tehama ni nn, usikute hata kitufe cha kupiga kura hawakioni.
 
naenda kuwa tafuta waijue tehama ni nn, usikute hata kitufe cha kupiga kura hawakioni.
Uzi mrefu Sana dah [emoji3166]
Unahitajika muda wa ziada kuisoma kwa Makin na kuelewa kaa kwa kutulia tuna majukumu mengi ya familia ,tutasoma tu.
 
Back
Top Bottom