Nafasi ya tatu kwenye mashindano mengi ni ya kisiasa tu Haina maana yoyote.Fifa waondoe hii

Nafasi ya tatu kwenye mashindano mengi ni ya kisiasa tu Haina maana yoyote.Fifa waondoe hii

Habarini wadau wa soka.

FIFA wangeanza kwa kuondoa hii nafasi ya tatu kwenye mashindano haya ya kombe la dunia then wengine wangefuata.

Sioni maana ya hii nafasi zaidi ya kupoteza muda na kujichosha tu.Labda iwe kwa ajili ya kupata pesa tu.
Dhumuni la timu ni kucheza fainali na sio kucheza kutafuta nafasi ya tatu.Hata morari ya mechi yenyewe inakuwa hakuna.

Nguvu ya wachezaji huwa inakwisha kabisa pale wanapotolewa kwenye nusu fainali.Huwa wanalia wengine,biashara ndio huwa imeishia pale.Nafasi ya tatu ni kupoteza muda na nguvu bure.
Mi ningeshauri FIFA watoe tu zawadi kwa timu zilozotolewa kwenye nusu fainali.Na sio kutafuta mshindi wa tatu.Kifupi hizo ndio the best timu kwenye mashindano yoyote.Nguvu yao yote kwenye nusu fainali ni kutaka kuingia fainali.Inapotokea bahati mbaya basi huwa wachezaji wanakosa morari kabisa.

FIFA itoe zawadi Kama the best timu zilizoingia nusu fainali na kuzipongeza.

Tukiachana na Hilo kwenye mechi ya fainal Kama ufaransa wakimdhibiti Messi basi watakuwa mabingwa.Messi ndio huwa na makabrasha mengi kule mbele yanayoleta matatizo.Nawatakia ubingwa waafrika wenzetu ufaransa..
Kila la heri kina mbappe.
Wivu huo hamia Morocco
 
Kazi kweli kweli mtu yupo kiburugwa anampangia mtu aliyekuwa Qatar cha kufanya wakati nchi yake ina matatizo kibao leo tumeangalia mpira kama tupo vitani machuma kila sehemu.
 
Sioni maana ya hii nafasi zaidi ya kupoteza muda na kujichosha tu.Labda iwe kwa ajili ya kupata pesa tu.
Lengo la hayo mashindano ni kupata pesa pia...hivyo ikiwepo sio tatizo.

Nawatakia ubingwa waafrika wenzetu ufaransa..
Kila la heri kina mbappe.
Wale ni Wafaransa tu, sio waafrika wenzako..... waafrika wenzako walishaaga michuano kitambo.
 
Morali gani unazungumzia.ulishawai kucheza mashindsno gani hadi uone nafasi ya tatu wachezaji wanakua hawana morali.Hizi hisia zetu kwa sisi tulioshindwa kila kitu usifikiri iko kwa wote wenye moyo na jitihada zakupambana.Kwa wenzetu kila hatua moja juu ni mafanikio na ni kumbukumbu wanaweka ili watumie tena kama kioo mashindano mengine.Kwahiyo unachokiongea wewe ni hisia zako kwa wewe uliyeshindwa sio kwa wale wanaojua nini maana ya mashindano.
 
Wabongo kwa ujuaji huwezi, mechi ya jana watu wamecheza kama final, wenzetu hata friendly match wanakaza sijui anataka kuongea nini huyu
 
Back
Top Bottom